WATU 12
wamefariki dunia papo hapo na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya basi
walililkuwa wakisafiria la Kampuni ya Aljabir kugonga treni eneo la Kiberege
Ifakara Wilaya ya Kilombero.
Thursday, 6 November 2014
Wednesday, 5 November 2014
Monday, 29 September 2014
JAMBAZI LAUWAWA MORO, NI BAADA YA KUKUTWA NA BUNDUKI AINA YA SMG, RISASI, IRIZI NA NGUO YA JWTZ.
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro Leonald Paul akionyesha suruari inayofanana na sare ya jeshi la JWTZ ilikouwa ikitumika katika matukio ya ujambazi na Mwantui Anton Msangai.
Jambazi huyo alifariki dunia baada ya kupata kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali Septemba 29 mwaka huu majira ya saa 12.45 huko katika eneo la njia panda ya Kilosa.
Kwa mujibu wa kamanda huyo jambazi huyo alikuwa anaelekea wilayani kilosa kwaajili ya kufanya matukio ya uharifu.
inadaiwa Septemba 26 jambazi huyo na wenzake walivamia duka moja wilayani Mvomero na kupora 700,00 na vocha za simu na kupiga risasi juu baada ya wananchi kutaka kuwakimbiza,
Kamanda huyo alisema jambazi huyo ni miongoni mwa majambazi watano waliokamatwa na polisi baada ya kufanya matukio ya uharifu mkoani Dodoma na Morogoro.
Kamanda huyo alisema jambazi huyo alikuwa na tabia ya kutumia makundi tofauti ya watu kufanya nao uharifu katika maeneo mbalimbali kisha kutoweka na kuelekea sehemu nyingine.
Kamanda huyo akionyesha bunduki aina ya SMG aliokamatwa nayo Jambazi huyo ikiwa na magazine 2 pamoja na risasi za SMG 47.
Pia jambazi huyo alikutwa na irizi ambayo inasadikiwa alikuwa akitumia katika matukio ya ujambazi kwa imani za kishirikina.
WAKATI HUO HUO

MTU mmoja
Joseph Ngasa anashikiliwa na polisi mkoani hapa ,kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mtoto wa miaka 7 na kumsababishia
kifo chake.
Kamanda wa
polisi mkoani hapa Leonald Paul alisema tukio hilo limetokea Septemba 27 mwaka
huu huko eneo la Bilo, tarafa ya Ngohelanga wilayani Ulanga.
Alisema mtuhumiwa huyo alikwenda katika nyumba hiyo
kutembea na kwamba siku ya tukio alikuwa
nje, ambapo mtoto huyo alimuaga mama yake anakwenda chooni kujisaidia.
Alisema kijana
huyo aliposikia hivyo alimfuata mtoto huyo chooni na kumfanyia kitendo hicho
ambapo mtoto huyo alifariki dunia muda mfupi badae.
Alisema
mtuhumiwa huyo anadaiwa alifanya kitendo hicho kwa imani za kishirikina, na
kwamba anashikiliwa na polisi
atafikishwa mahakamani mara baara ya uchunguzi kukamilika.
Sunday, 28 September 2014
MAZISHI YA MEHTOD MENGI KUFANYIKA ALHAMISI SEPTEMBA 2 MWAKA HUU MJINI MOROGORO
Marehemu Method Mengi |
Mke wa Marehemu katikati akiwa na majonzi |
Vitu vilivyotolewa na Watanzania kwa ajili ya mnada |
MC James Shemdoe |
Mwili wa marehemu Method Mengi mkazi wa Kilakala manispaa ya Morogoro ambaye alikuwa akiishi na kufanya kazi nchini Marekani unatarajiwa kuwasili hapa nchini Jumatano Septemba mosi mwaka huu ukitokea nchini Marekani.
Mdogo wa marehemu ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kilakala Ribon Mkali ,alisema baada ya mwili huo kuwasili ndugu na jamaa wanaoishi Jijini Dar es Salaam watapata fulsa ya kuaga mwili huo katika uwanja wa ndege wa Dar kisha kuanza safari kuelekea mjini Morogoro.
Aidha alisema ratiba ya mazishi itaanza saa 5 asubuhi nyumbani kwao Kilakala kwa chakula, saa 7 kuaga mwili huo saa 8itafanyika ibada ya kuombea mwili huo katika kuu la mtakatifu Patric mjini hapa na badae kuelekea katika makaburi ya Kola hili kwaajili ya kukamilisha mwili taratibu za kuhifadhi mwili huo.
Hata hivyo Riboni alipoulizwa juu ya uvumi uliotawala juu ya Marehemu huyo kuuwawa alisema kwa sasa hawezi kuzungumza chochote hadi ripoti ya uchunguzi juu ya kifo cha marehemu huyo itakapokabidhiwa kwa familia.
Marehemu Method alizaliwa Julai 4,19 72 mkoani Morogoro
alifariki Septemba 17 mwaka huu nchini Marekani,
Marehemu ameacha mke na watoto watatu,
Mungu ametoa na Mungu ametwaa kazi yake haina makosa, roho ya marehemu ipate rehemu kwa mungu , apumzike kwa amani, Ameen.
Subscribe to:
Posts (Atom)