UONGOZI wa Jumuiya na Taasisi za kislamu mkoa wa Morogoro,umeikataa kamati ya haki jinai iliyoundwa na Jeshi la polisi nchini kwajili ya kuchunguza tukio linalodaiwa kupigwa risasi kwa Mwenyekiti wa jumuiya na taasisi hiyo nchini Sheikh Issa Ponda.
Mwenyekiti
wa jumuiya na taasisi hiyo mkoa wa
Morogoro Sheikh Ayubu mwinge salumu alisema
hayo baada ya kuitwa na tume hiyo katika ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa
morogoro ambako tume iliweka kambi kwajili ya kuhoji na kusikiliza ushahidi wa
tukio hilo kwa waumini wa dini hiyo ambao walikuwepo katika tukio hilo.
Akizungumza
na Waandishi wa habari mara baada ya kugoma kutoa ushahidi kwa kamati
hiyo,Sheikh Salum alisema kuwa hawapo tayari kutoa ushahidi huo kwakuwa hawana
imani na kamati hiyo kwakuwa kamati hiyo haipo huru kama walivyotarajia.
Alisema kuwa
wao ndio waliomba kuundwa kwa tume hiyo na kutaka iwe huru lakini wameshangazwa
tume hiyo kuundwa na jeshi hilo la polisi ambalo ndio linalolalamikiwa kutokana na tukio hilo.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa wao wanaushahidi wa kutosha kuhusiana na tukio hilo lilotokea
Agosti 10 mwaka huu mara baada ya Sheikh Ponda kumaliza kuhutubia kongamano la
waadhiri lilofanyika katika uwanja wa shule ya msingi kiwanja cha ndege.
Alisema kuwa
watakuwa tayari kutoa ushahidi katika kamati hiyo wajumbe wake watapatikana nje
ya Serikali na wengine nje ya nchi.
Hata hivyo
mwenyekiti huyo alisema kuwa kamati hiyo inayoundwa na kamishna wa jeshi hilo
Isaya Mngullu imekubali maombi yao na kuyapeleka makao makuu ya jeshi hilo.
Alisema kuwa
hivi sasa wanawasilina na uongozi wa taifa wa Jumuiya na Taasisi za kislamu
Taifa ili kujua ni viongozi gani wataongezewa katika kutoa ushahidi katika
kamati itakayokuwa huru kushunguza tukio la Sheikh Ponda.
Naye naibu
mwenyekiti wa Jumuiya na Taasisi za kislamu mkoa wa Morogoro,Sheikh Chaulembo
Ally,alisema kuwa polisi ndio wamekuwa chanzo cha matukio ya waislam kufanyiwa
vurugu katika makongamano yao.
Alikumbushia
tukio la muumini wao Hamis Dibagula lilotokea mwaka 2001 ambapo walimkamata na
kuhukumiwa mashtaka na kufungwa miezi 18 kwa madai kuwa alifanya uchochezi.
0 comments:
Post a Comment