Pages

Subscribe:

Saturday 29 March 2014

PINDA, MAKAMO WA RAIS WAHUDHURIA MAZISHI WA RC MARA MAREHEMU TUPA

 Jeneza lililobeba mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara John Tupa baada ya kuwasili nyumbani kwake wilayani Kilosa mkoani Morogoro Tayari kwa mazishi.
 Waziri mkuu Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza la mwili wa marehemu Tupa nyumbani kwake Kilosa.
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni mwenyekiti wa wakuu wa mikoa nchini Abas Kandoro akitia saini katika kitabu cha wageni nyumbani kwa marehemu Tupa.

 Makamo wa Rais Gharibu Bilali akitoa heshima za mwisho kwa alieyekuwa Rc mara mara baada ya kumalizika kwa ibada takatifu nyumbani kwake Kilosa.

 Makamo wa Rais Dk Bilali akisalimiana na askofu wa jimbo katoriki la Morogoro Telesphori Mkunde katika ibada ya mazishi.

 Familia ya Marehemu Tupa wakisikiliza ibada ya misa ya mazishi ya mpendwa wao Tupa.

 Watoto wa Marehemu tupa wakisindikizwa kuaga mwili wa marehemu baba yao.
 Mjane wa marehemu Tupa Akiaga mwili wa mumewe  mara baada ya kumalizika ibada nyumbani kwao Kilosa.
 Waziri mkuu Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Tupa
 katibu mkuu wa UWT Amina Makilaki akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la RC Tupa
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro Inocent karogeries akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza la mwili wa marehemu Tupa
 katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romul akiwa katika foleni ya kwenda kuaga mwili wa marehemu Tupa.
 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu , Ana Tibaijuka na mkuu wa mkoa wa tabora fatuma Mwasa wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu Tupa.
 Mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Morogoro Mecktridic Mdaku a na Juliana mwenda mjumbe wa kamati wa Siasa ya mkoa wa Morogoro wakitoa heshima za mwishi kwenye jeneza la mwili wa marehemu Tuapa.

 IGP msataafu Omary mahita akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Tupa
 Mkuu wa wilaya ya Tanga Halima Dendego akitoa heshima za mwisho
 mwenyekiti wa CCM wilaya ya Morogoro Fikiri Juma akitoa heshima za mwisho
 Viongozi wa CCM mkoa wa Morogoro  wakitoa heshima za mwisho
 Mke wa marehemu akisindikizwa kuaga mwili wa mume wake marehemu Tupa
 Mke wa marehemu Tupa akitoa heshima za mwisho
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Morogoro na mikoa mingine waliohudhuria mazishi hayo wakifutilia ibada ya misa takatifu ya kumwombea marehemu Tupa.

Thursday 27 March 2014

MFUKO WA PENSHENI WA LAPF WATOA FAO LA UZAZI KWA WANACHAMA ZAIDI YA 3000

 Abubakhar Nduwate meneja wa mafao wa Mfuko wa LAPF akiongea na waandishi wa habari juu ya baadhi ya mifuko ya Pensheni wanavyofanya hujuma kurubuni wafanyakazi wapya kwa kuwadanganya aina za mafao ambayo hawatoi katika mifuko yao na hivyo kusababisha wafanyakazi hao kujutia  badae, fao moja wapo ni la Uzazi.
 Magambo Fotnatus angalizi mkuu wa fedha katika mfuko wa pensheni wa LAPF akiongelea jinsi mfuko huo ulivyojiimarisha katika miradi yake kwa lengo la kuboresha mafao kwa wanachama wake
 Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Morogoro  waliohudhuria mkutano huo wa waandishi wa habari na viongozi wakuu wa mfuko huo
Waandishi wa habari wa mkoa wa Morogoro wakiwa katika mkutano huo

habari kamili soma hapo chini.





JUMLA ya wanachama 3,252 wamenufaika na fao la uzazi kupitia mfuko wa pensheni wa LAPF ambapo kiasi cha shilingi 2,271, 756,1017.72 zililipwa na mfuko huo kwa kiwango cha asilimia 129 ya mshahara  katika kipindi cha miaka 3.

Hayo yalisema jana na meneja wa mafao wa mfuko huo Abubakar Nduwate wakati akiongea na waandishi wa habari katika ofisi ya mfuko huo ilipo steni kuu ya mabasi ya Msamvu.

Alisema kuwa Fao hilo ni muhimu sana kwa wafanyakazi kwani katika kipindi  hicho mwanachama anakua na mahitaji muhimu hivyo hupata nafuu.

Hata hivyo alisema kuwa wanatarajia kuanzisha fao la elimu na mikopo ya SACCOS kwa wanachama wake  ifikapo mwezi Julai mwaka huu.

Meneja huyo aliwataka waajiri kuwapa fulsa ya kutoa elimu kwa wafanyakazi  hususani walimu wanaotarajiwa kuajiriwa hivi karibuni ili wachague mfuko wanaotaka kutokana na mafao watakayoona ni bora kwao.

‘’ ipo baadhi ya mifuko ambayo imekuwa ikiwarubuni wafanyakazi wanaoajiriwa sasa hivi kuwa wanatoa mafao ya uzazi lakini kumbe fao hilo halipo jambo ambalo linawafanya kuingia katika mifuko na badae kujutia’’ Alisema

Alisema  wamepata taarifa juu ya baadhi ya watu wenye nia ya kuhujumu mifuko mingine ambao wamejipanga kwaajili ya kuuliza masawali ya kubomoa mifuko mingine ambao sio walimu , katika kipindi hicho cha ajira mpya za walimu.

Alisema kuwa mfuko huo kamwe hautotumia njia za mitandao ya simu kuwasajiri wanachama na badala yake ni lazima wawapatie elimu kabla ya kuwasajiri ili waweze kuingia wakati wakiujua vizuri mfuko huo na kwamba wanazo ofisi kila mkoa hapa nchini ambazo zitafanya shughuli hizo na kutoa vitambulisho papo hapo.

Naye Magambo Fotnatus ambaye ni mwangalizi mkuu wa fedha wa mfuko huo alisema LAPF imejipanga vizuri katika kuhakikisha miradi yake inakuwa imara kwa lengo la kuboresha mafao ya wanachama wake.




Wednesday 26 March 2014

Matukio mbalimbali yaliyojiri leo mjini Dodoma linakoendelea Bunge Maalum la Katiba

habari
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Dkt. Fenella Mukangara (kulia) na Anne Kilango Malechela(kushoto) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma mara baada ya kuharishwa kwa kikao cha Bunge hilo.

MTOTO ALIYEJERUHIWA KATIKA SHAMBULIO KANISANI AFIKISHWA NAIROBI KWA MATIBABU


 
Mtoto Satrin akiwa amebebwa na baba yake mzazi Benson Osinya ndani ya ndege kuelekea jijini Nairobi kwa matibabu.

MTOTO Satrin Osinya aliyejeruhiwa na risasi iliyomuua mama yake katika shambulio la kigaidi lililofanywa kwenye kanisa la Joy of Jesus huko Likoni, Mombasa nchini Kenya Jumapili iliyopita, jana amefikishwa jijini Nairobi kwa matibabu.

Monday 24 March 2014

ANGALIA NAFASI MPYA ZA KAZI SERIKALINI

PRESIDENT’S OFFICE
PUBLIC SERVICE RECRUITMENT SECRETARIAT
Ref. Na EA.7/96/01/G/02
VACANCIES ANNOUNCEMENT
On behalf of the, Tea Board of Tanzania (TBT), the Public Service Recruitment
Secretariat invites qualified Tanzanians to fill 1 vacant post in the above public
institutions.
NB: GENERAL CONDITIONS
i.All applicants must be Citizens of Tanzania and not above 45 years old, however,
should also observe the age limit for each position where indicated.
ii. Applicants must attach an up-to-date current Curriculum Vitae (CV) having
reliable contact postal address, e-mail address and telephone numbers.
iii. Applicants should apply on the strength of the information given in this
advertisement.
iv. The title of the position and institution applied for should be written in the
subject of the application letter and marked on the envelope; short of which
will make the application invalid.
v. Applicants must attach their detailed relevant certified copies of Academic
certificates:
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma transcripts.
- Form IV and Form VI National Examination Certificates.
- Computer Certificate
- Professional certificates from respective boards
- One recent passport size picture and birth certificate.
vi. FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS ARE STRICTLY NOT ACCEPTED
vii. Testimonials, Partial transcripts and results slips will not be accepted.
viii. Presentation of forged academic certificates and other information in the
CV will necessitate to legal action
ix. Applicants for senior positions currently employed in the public service should
route their application letters through their respective employers.
x. Applicants for entry levels currently employed in the Public Service should
not apply, they have to adhere to Government Circular Na. CAC.
45/257/01/D/140 dated 30th November, 2010.
xi. Applicants who have/were retired from the Public Service for whatever reason
should not apply.
xii. Applicants should indicate three reputable referees with their reliable contacts.
xiii. Certificates from foreign examination bodies for ordinary or advanced level
education should be certified by The National Examination Council of
Tanzania (NECTA)
xiv. Certificates from foreign Universities should be verified by The Tanzania
Commission for Universities (TCU)
xvi. Applicants with special needs/case (disability) are supposed to indicate
xvii. Women are highly encouraged to apply
xviii. Only short listed candidates will be informed on a date for interview
xix. Application letters should be written in Swahili or English
xx. APPLICATION LETTERS SHOULD BE POSTED TO THE FOLLOWING

CHADEMA YAPATA PIGO, MWENYEKITI WA VIJANA NA VIJANA 100 WILAYANI ARUMERU WAHAMIA CHADEMA

 picha ikionyesha baadhi ya wanachama wapya waliojiunga na CCM, wakila kiapo, katikati ni aliyekuwa Mwenyekiti  wa Vijana CHADEMA kata ya Orturumenti Thomasi Kivuyo.
 Mwenyekiti wa vijana chadema kata ya Orturumenti akiwa anatoa mkono kwa katibu wa siasa uenezi Jonasi Kitoro mara baada ya kukabidhiwa kadi ya ccm

 katibu wa vijana wilaya ya arumeru  akiwa Boniface Mungaya akionyesha baadhi ya kadi zilizorudishwa na wanachama wa chadema.

ANGALIA PICHA RISASI ZA MOTO NA MABOMU HUKO NZEGA,DKT KIGWANGALA ALIVYOKAMATWA NA WACHIMBAJI WADOGO WA NZEGA WALIVYOTAWANYWA NA POLISI


Hivi ndivyo Mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora Dkt Hamis Kiwangala(mwenye shati jeupe) alivyokamatwa wakati wa maandamano ya wachimbaji wadogo machimbo ya Mwashina wilayani Nzega mkoani Tabora,huku wananchi wakikimbia hovyo kwani polisi walitumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya.
Polisi wakikabiliana na wachimbaji wadogo wa madini wilayaniNzega

Pichani ni mmoja kati ya waandamanaji hao aliyekuwa karibu na Dkt Kigwangala akiwa chini baada ya kujeruhiwa na polisi
Mlipuko wa mabomu kwa mbali

Friday 21 March 2014

HOTUBA YA JK,WAKATI WA KULIHUTUBIA BUNGE MAALUM LA KATIBA




Mheshimiwa Samuel Sitta, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba;Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar;Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa ZanzibarMheshimiwa Anne Semamba Makinda; Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano; Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba ; Mheshimiwa Rashid Othman Chande, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;Mheshimiwa Othman Makungu, Jaji Mkuu wa Zanzibar; Viongozi Wakuu Wastaafu; Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba; Waheshimiwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba; Wageni waalikwa; Mabibi na Mabwana; Pongezi Nakushukuru sana Mheshimiwa Mwenyekiti kwa kunipa fursa ya kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wajumbe wa Bunge letu Maalum la Katiba katika siku hii muhimu na ya kihistoria kwa nchi yetu. Nimekuja kuwatakia heri na naungana na Watanzania wenzetu wote kuwaombea baraka za Mwenyezi Mungu, ili muweze kuifanya kazi yenu kwa utulivu, hekima, umakini mkubwa na kuimaliza kwa salama na kwa mafanikio yanayoyatarajiwa na Watanzania. Natoa pongezi nyingi kwako na kwa Makamu wako kwa kuchaguliwa kwenu kuongoza Bunge hili maalumu na la kihistoria. Ushindi mkubwa mliopata ni kielelezo tosha cha imani kubwa na matumaini waliyonayo Wajumbe wenzenu kwenu. Matumaini yao ndiyo matumaini ya Watanzania wote, kwamba mtaliongoza vizuri Bunge hili, ili liweze kutimiza kwa ufanisi mkubwa jukumu lake muhimu sana katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mheshimiwa Mwenyekiti;Niruhusu pia niwapongeze kwa dhati Wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba kwa bahati ya aina yake waliyopata ya kutunga Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Fursa hii hutokea mara chache sana katika historia ya nchi yo yote na watu wake. Mkifanikiwa kuipatia nchi yetu Katiba nzuri majina yenu yataandikwa kwa wino wa dhahabu, katika kumbukumbu za historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni matarajio ya Watanzania kuwa mtatunga Katiba itakayokubalika na wengi. Katiba inayotekelezeka.

Wednesday 19 March 2014

WAANDISHI WA HABARI MORO KUJIUNGA NA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF

 Mwenyekiti wa Club ya waandishi wa  habari mkoani Morogoro Ida Mushi akifungua semina ya siku moja kwa waandishi wa habari juu ya uendeshwaji wa mfuko wa pensheni  LAPF jana mkoani haoa
 Katibu wa club ya waandishi wa habari mkoani Morogoro  Adeid Dogoli akitoa neno la utangulizi katika semina hiyo.

   Meneja ya Mashariki wa Kanda wa mfuko Lulyaya Sayi wakati akitoa mada  juu ya uendeshaji wa mfuko wa LAPF kwa waandishi wa habari mkoani Morogoro.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifutilia semina hiyo kwa makini


MFUKO  wa Penshen wa LAPF (Local Authorities Pensions Fund) umekusanya jumla ya shilingi bilion 119.2 kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 na kutumia kiasi cha cha shilingi bilioni 56.8 kulipa wanachama wake pensheni
   Meneja ya Mashariki wa Kanda wa mfuko huo,Lulyaya Sayi,alisema kuwa mfuko wa LAPF una uwezo kifedha wa kijiendesha wenyewe zaidi ya miaka 100 bila kuterereka kutokana na kuwa na mfumo imara wa uwekezaji.
Sayi alisema mfuko huo umekuwa ukifanya vizuri katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo bila kupata ushindani kutoka kwa mifuko mingine ya kijamii inayotoa pensheni kama wao na bado wanaendelea kufanya vizuri katika miaka inayokuja na kuongeza ubora wa ufanisi wa kazi
Alisema mfuko unakabiliwa na changamoto nyingi  ilia kutokana na utendaji wao wanakabiliana nazo na kuweza kuzipatia ufumbuzi,changamoto hizo ni ufinyu mdogo wa wanachama kuhussu mfuko,propaganda za watu wengine kusemea mfuko na kusababisha wanachama kwenda katika mifuko mingine
Alisema   mfuko umekuwa ukiingia mkataba na serikali katika ujenzi wa miradi mbalimbali ndani ya nchi,hivi sasa wameingia mkataba na manipsaa ya morogoro katika ujenzi wa hoteli ya kisasa katika stendi kubwa ya mabasi ya mkoa iliyopo eneo la msamvu ambayo itagharimu kiasi cha shilingi bilioni 35 kwa kipindi cha miezi 18
Kwa upande wake Afisa Matekelezo wa mfuko wa LAPF Kanda ya Mashariki Charles Mahanga alisema kuwa kutokana na sheria ya mifuko ya umma mtumishi wa serikali ana uwezo wa kuchagua mfuko wowote unaoupenda ila imetokea hivi sasa baadhi ya watu ama waajiri kumlazimisha mtumishi kuingia mfuko fulani kutokana na masalahi yake
Mahanga alisema sekta ambayo imekuwa tatizo kwa muda mrefu ni walimu ambao idadi yao ni kubwa na wepesi sana kupotoshwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya walimu ama walimu waliowatangulia kazini kujiunga katika mifuko mingine kutokana na mazoe waliyokuwa nayo toka kipindi cha nyuma ambacho kulikuwa na mfuko mmoja tu wa PSPF
Hata hivyo alisema kuwa mfuko umejipanga kutumia vyombo vya habari kutoa elimu kwa wanachama wake,kupita katika vyuo mbalimbali,katika warsha,lengo ni kuhakikisha wanachama wanapata uelewa wa kutosha kuhusu mfuko,wanaongeza idadi ya wanachama na kudumisha utendaji bora wa kazi.

ATHARI ZA MGOMO WA DALADALA MANISPAA YA MOROGORO

Wanafunzi wa shule mbalimbali za Manispaa ya Morogoro wakisubiri usafiri wa kwenda shule bila mafanikio katika kituo cha mabasi kilichopo Mkoani Morogoro.

Wanafunzi wa shule mbalimbali za Manispaa ya Morogoro wakiwa kwenye lori baada ya mgomo wa madereva daladala leo.

ANGALIA PICHA ZA MGOMO WA DALADALA LEO MKOANI MOROGORO



wakazi wa Morogoro ambao leo asubuhi walilazimika kutumia usafiri wa vyombo visivyo rasmi kusafirisha abiria, ili kuwahi makazini

Tuesday 18 March 2014

CHAMA KIPYA CHA ACT WAGAWA KADI ZA CHAMA BURE MOROGORO



Leo hi BUSTANI YA HABARI ilibahatika kukutana na tukio la ugawaji kadi katika kijiwe kikongwe cha siasa mkoani Morogoro kinachofahamika kwa jina la TAHARIRI SQUARE.Watu kadhaa wamejiunga na chama hicho baada ya kupigwa darasa la nguzo za chama hicho ambazo zimeandikwa nyuma ya kadi.

Angalia Tweet ya Januari Makamba baada ya warioba kuhutubia bunge

Baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kuhutubia Bunge hii leo…Januari Makamba ambeye ni mjumbe wa bunge hilo la katiba, kupitia ukurasa wake wa twitter kaandika hivi

ANGALIAHOTUBA YA JAJI JOSEPH SINDE WARIOBA ALIOWASILISHA RASIMU YA PILI YA KATIKA BUNGENI LEO