Abubakhar Nduwate meneja wa mafao wa Mfuko wa LAPF akiongea na waandishi wa habari juu ya baadhi ya mifuko ya Pensheni wanavyofanya hujuma kurubuni wafanyakazi wapya kwa kuwadanganya aina za mafao ambayo hawatoi katika mifuko yao na hivyo kusababisha wafanyakazi hao kujutia badae, fao moja wapo ni la Uzazi.
Magambo Fotnatus angalizi mkuu wa fedha katika mfuko wa pensheni wa LAPF akiongelea jinsi mfuko huo ulivyojiimarisha katika miradi yake kwa lengo la kuboresha mafao kwa wanachama wake
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Morogoro waliohudhuria mkutano huo wa waandishi wa habari na viongozi wakuu wa mfuko huo
Waandishi wa habari wa mkoa wa Morogoro wakiwa katika mkutano huo
habari kamili soma hapo chini.
JUMLA ya wanachama 3,252 wamenufaika na fao la uzazi kupitia
mfuko wa pensheni wa LAPF ambapo kiasi cha shilingi 2,271, 756,1017.72
zililipwa na mfuko huo kwa kiwango cha asilimia 129 ya mshahara katika kipindi cha miaka 3.
Hayo yalisema jana na meneja wa mafao wa mfuko huo Abubakar
Nduwate wakati akiongea na waandishi wa habari katika ofisi ya mfuko huo ilipo
steni kuu ya mabasi ya Msamvu.
Alisema kuwa Fao hilo ni muhimu sana kwa wafanyakazi kwani
katika kipindi hicho mwanachama anakua
na mahitaji muhimu hivyo hupata nafuu.
Hata hivyo alisema kuwa wanatarajia kuanzisha fao la elimu
na mikopo ya SACCOS kwa wanachama wake
ifikapo mwezi Julai mwaka huu.
Meneja huyo aliwataka waajiri kuwapa fulsa ya kutoa elimu
kwa wafanyakazi hususani walimu
wanaotarajiwa kuajiriwa hivi karibuni ili wachague mfuko wanaotaka kutokana na
mafao watakayoona ni bora kwao.
‘’ ipo baadhi ya mifuko ambayo imekuwa ikiwarubuni wafanyakazi
wanaoajiriwa sasa hivi kuwa wanatoa mafao ya uzazi lakini kumbe fao hilo halipo
jambo ambalo linawafanya kuingia katika mifuko na badae kujutia’’ Alisema
Alisema wamepata
taarifa juu ya baadhi ya watu wenye nia ya kuhujumu mifuko mingine ambao
wamejipanga kwaajili ya kuuliza masawali ya kubomoa mifuko mingine ambao sio
walimu , katika kipindi hicho cha ajira mpya za walimu.
Alisema kuwa mfuko huo kamwe hautotumia njia za mitandao ya
simu kuwasajiri wanachama na badala yake ni lazima wawapatie elimu kabla ya
kuwasajiri ili waweze kuingia wakati wakiujua vizuri mfuko huo na kwamba wanazo
ofisi kila mkoa hapa nchini ambazo zitafanya shughuli hizo na kutoa
vitambulisho papo hapo.
Naye Magambo Fotnatus ambaye ni mwangalizi mkuu wa fedha wa
mfuko huo alisema LAPF imejipanga vizuri katika kuhakikisha miradi yake inakuwa
imara kwa lengo la kuboresha mafao ya wanachama wake.
0 comments:
Post a Comment