Meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo wakifurahia jambo na naibu
meya lidya Mbiaji baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kupitisha
bajeti ya shilingi bilioni 56,477,265,443 katika mwaka wa fedha
2014/2015
Diwani wa kata ya Mbuyuni Samuel Msuya akitoa hoja katika kiao hicho cha bajeti.
Robon Mkali diwani wa kata ya Kilakala akitoa hoja katika kikao hicho cha bajeti.
Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Simbeye akisoma taarifa katika kikao hicho.
Wajumbe wa baraza la madiwani la manispaa ya Morogoro wakifutilia kwa makini taarifa ya bajeti hiyo
Madiwani wa manispaa ya Morogoro wakiwa katika kikao maalumu cha bejeti ya mwaka wa fedha 2014/2015.
Baadhi ya wajumbe wa baraza la madiwani katika halmashauri ya manispaa ya Morogoro wakiwa katika kikao maalumu cha bajeti.
Wajumbe wa baraza la madiwani wakifutilia kwa makini kikao cha bajeti.
Meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.
Meya wa Manispaa ya Morogoro Amiri Nondo wakati akiingia katika kikao hicho cha bajeti..
Halmahsuari ya manispaa ya Morogoro inakisia
kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 56,477,265,443 ikiwa ni ongezeko la
shilingi bilioni 12, 828,572, 796 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya fedha.
Meya wa manispa ya Morogoro Amiri Nondo
amesema hayo Januari 13 mwaka huu wakati wa kikao maalumu cha bajeti cha baraza
la madiwani la halmashauri ya manispaa hiyo.
Amevitaja vyanzo hivyo kuwa ni
Halmashauri yenyewe, mapato kutoka serikali kuu pamoja na wahisani mbalimbali
sambamba na michango ya wananchi katika miradi ya maendeleo ambayo ni shilingi
63,089,832.
Hata hivyo alisema kuwa ongezeko hilo linatokana na kuboreshwa kwa ukusanyaji wa mapato ya stendi kuu ya mabasi ya Msamvu,ongezeko la viwango vya tozo ya kodi na ushuru mbalimbali kwenye masoko, mabango, vibali vya ujenzi na idadi ya mauzo ya viwanja.
Hata hivyo alisema kuwa ongezeko hilo linatokana na kuboreshwa kwa ukusanyaji wa mapato ya stendi kuu ya mabasi ya Msamvu,ongezeko la viwango vya tozo ya kodi na ushuru mbalimbali kwenye masoko, mabango, vibali vya ujenzi na idadi ya mauzo ya viwanja.
Alisema kuwa katika mapato hayo jumla ya
shilingi 1,765, 706, 400 zitatumika kwaajili ya uchangiaji wa miradi ya
maendeleo sawa na asilimia 37.75 ya makisio, na shilingi 40,473,600 zitalipwa
mishahara kwa watumishi wasiopata ruzuku na matumizi mengineyo ni
22,765,786,000sawa na asilimi 65.30.
Pia alisema kuwa kiasi cha shilingi
105,000,000 zitatumika katika vituo vya afya na zahanati mbalimbali katika
manispaa hiyo.
Meya huyo alisema kuwa katika mwaka wa fedha
2014/2015 halimashauri hiyo itatoa kipaumbele katika mambo makuu saba,
ambayo ni mapato, usafi wa mji, utawala bora, elimu, miundombinu na maji
0 comments:
Post a Comment