Pages

Subscribe:

Wednesday 22 January 2014

MAFURIKO MAKUBWA DUMILA, DARAJA LAKATIKA, HAKUNA MAWASILIANO DODOMA NA MOROGORO

BREAKING NEWS; 

Maafa makubwa yametokea eneo la Dumila wilayani Kilosa na eneo la Dakawa wilayani Mvomero, kutokana na mvua kubwa kunyesha katika maeneo mbalimbali ya Kilosa na kusababisha daraja la Dumila katika barabara kuu ya Dodoma na Morogoro kukatika.

Kwa sasa hali si shwari magari yanashindwa kupita na hivyo kusababisha msongamano mkubwa wa magari yanayotoka Dodoma kwenda Dar , na yanayotoka Dar kwenda Dodoma.

Taarifa zaidi tutawaletea punde.

0 comments:

Post a Comment