Pages

Subscribe:

Friday, 31 January 2014

MANISPAA MORO YAANZA ZOEZI LA KUNG'OA MABANGO YANAYODAIWA

 Halmashauri ya manispaa ya Morogoro imeanza zoezi la kuondoa mabango yote ambayo hayajalipiwa na kampuni zao, zoezi hilo limekuja baada ya manispaa hiyo kudai zaidi ya milinini 400 katika makampuni mbalimbali yakiwemo ya Cocacola, Tigo, PPF na TBL
 Moja ya bango lilolokuwa katika eneo  ya kona ya Kilakala likiwa limefutwa kwa rangi nyeusi
 Dawa ya deni ni kulipa na si vinginevyo, tunafuta hata maandishi yalioandiskwa ukutani
 Moja ya bango lililokuwa nje ya hotela ya Hilax , bango la matangazo ya bia ya kampuni ya TBL likichanwa na mfanyakazi wa manispaa wakati wa zoezi hilo.
 Meneja tumekuja nyie pia mnadaiwa hela ya bango, '' Hilo dogo kwa benk kama hii, tupeni madai yetu tunawandikia  hundi sasa hivi, meneja wa CRDB Mapunda akimwambia mkuu wa kitengo cha mabango katika manispaa ya Morogoro Lina
 Hili ni bango la PPF likiondolewa na wafanyakazi wa Manispaa ya Morogoro kutokana na kudaiwa kodi ya bango hilo.
bango la PPF likipakiwa katika gari la manispaa kwajili ya kupelekwa yadi hadi hapo watakapolikomboa.

0 comments:

Post a Comment