Waziri mkuu Mizengo Pinda akitembelea eneo la Dumila ambako daraja
limekatika na kusababisha kukosekana kwa mawasiliano kati ya Dodoma na
Morogoro baada ya mvua nyingi zilizonyesha na kusababisha mafuriko
makubwa yaliopelekea maafa makubwa katika wilaya ya Kilosa na Mvomero
mkoani Morogoro.
Maelfu wa wananchi wa Dumila wakimsubiri waziri mkuu kufutia mafuriko hayo.
Viongozi wa serikali na chama wakiteta jambo mara baada ya waziri mkuu
kumaliza kuzungumza na wananchi katika eneo la Magole wilayani
Kilosa.
Watoto waliokuwa wakijaribu kuvuka kutoka sehemu moja kwenda nyingine katika eneo la Mvomero.
Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli akiwa na sekretariliati ya mkoa mara baada ya kuagana na waziri mkuu.
Moja ya nyumba katika eneo la Mvomero ikiwa imezingirwa na maji
Shamba la miwa likiwa limezolewa na kuachwa tupu huku likiwa na mabaki ya maji huko Dumila.
Mkazi wa eneo la Magole Kilosa akijaribu kuondoa maji yalioingia katika nyumba yake.
Mtoto akijaribu kuzoa maji yalioingia ndani kwao.
Wanawake waliokuwa katika eneo la Magole ambao walidai vitu vyote na chakula vimezolewa na maji, na hawajala tangu jana.
Viongozi wa CCM walipotembelea eneo la Mvomero kujionea mafuriko hayo
Maroli yanayosafirisha mizigo uelekeo wa Dodoma yakiwa yamekwama kusubiri hatma ya daraja hilo.
Ni maroli yaliojaza barabara ya Morogoro na Dodoma katika eneo la dakawa hadi Dumila.
Katibu wa CCM mkoa akizungumza na madiwani katika ofisi za CCM wilaya
ya Mvomero waliokuwa katika ziara ya kutembelea eneo la mafuriko Dumila.
0 comments:
Post a Comment