Pages

Subscribe:

Tuesday 28 January 2014

MTIBWA KUANZA KULIPA WAFANYAKAZI JANUARI 30 MWAKA HUU

 Yaani siwezi kuwa mpumbavu kuwaruhusu eti mkatandike mikeka katika kiwanda cha Mtibwa mkidai fedha zenu, Ni mkuu wa wilaya ya Mvomero Antoni Mtaka wakati akiongea na wafanyakazi, wastaafu,  na wakulima wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa wilayani humo ambao walitaka kujua muafaka wa madai yao.

 Ni lazima tujadiliane kwa makini tupate ufumbuzi, anayesema maneno yangu ni siasa, siasa haziko hapa ziko huko. Ni Dc Mtaka akiwajibu wakulima hao waliomwambia kuwa anayoongea ni siasa na kwamba hakuna utekelezaji.


 Tunachotaka hapa leo ni kulipwa fedha zetu na sio vinginavyo, ni mmoja wa wakulima wa miwa  Mtibwa Turiani akiongea katika mkutano huo wa maelfu ya watu.

Tufanye hivi leo ni Jumanne, hawa watu tuanze kuwalipa ifikapo Alhamisi au unasemaje? meneja msaidizi Kiula akinong'ona na meneja mkuu wa kiwanda hicho Hamad Yahaya.

0 comments:

Post a Comment