Mkuu wa wilaya ya Mvomero Antoni Mtaka akiongea na umoja wa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu wenye imani ya Kipentekoste wakati wa mahafari ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari na vyuo ( TAYOMI)iliofanyika melela wilayani Mvomero.
Mkuu huyo wa Wilaya akimtunuku cheti mwanafunzi wa chuo kikuu cha mzumbe Caroline Ndosi katika mahafari hayo ya kidini.
Wanafunzi hao wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mtaka.
Wanafunzi hao wakiwa katika picha ya pamoja na DC huyo
Habari zaidi
soma hapa chini
MKUU wa wilaya ya Mvomero Antoni Mtaka amewatahadharisha
vijana wasomi kutoruhusu kukanyaga
historia ya waasisi wa Nchi kwani
waliweza kufanya mambo makubwa na wanatakiwa kuenziwa.
Alisema hayo jana wakati akiongea katika kongamano la umoja wa wanafunzi walioko shuel za
msingi, sekondari na vyuo vya kati na
vyuo vikuu walio na msingi wa imani ya Kipentekoste (TAYOMI) iliofanyika Milela wilayani Mvomero.
Alisema wapo baadhi ya watu ambao wamefilisika kimawazo na
fikra wanatumia muda wao mwingi kujadili na kutukana mambo waliofanya waasisi
hao badala ya kujadili masuala ya katiba yaliopo sasa.
‘’ Unakuta wapo watu wanadiliriki kumtukana Nyerere bila
kujali kuwa ndiye aliyetuletea uhuru wan chi hii, nchi nyingi za Afrika zimekuwa zikimuenzi Nyerere kwa kutambua mchango wake katika kupatikana
kwa uhuru wan chi zao’’ Alisema
Alisema kama nchi
hizo zinatambua umuhimu wake na kumuenzi inashangaza na watangaaa kuona
watanzania hawathamini mchango wake na badala yake wanamtukana.
Alisema Nyerere na waasisi wengi wan chi hii walifanya mambo
makubwa sana nay a kihistoria hivyo kwa vijana wanayo kila sababu ya kuyaenzi
kwa heshima zote na kuwapuuza watu hao wanaobeza mchango wao viongozi hao.
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka vija hao wasomi kutumia muda
mwingi kufutilia suala zima la mchakato wa katiba na kupembua vipengele muhimu
ili ikifika wakati wa kupiga kura iwe rahisi kwao .
‘’ Watu wengi wamejipatia umaarufu kupitia katiba mpya
wakidhani katiba ile inaishia bungeni tuu, kumbe katiba ile mchakato wake
itarudi tena kwa wananchi na kupigiwa kura’’ Alisema
Kwa upande wake Philipo Abiud
Mratibu wa TAYOMI wa mkoa wa Morogoro alisema wamekuwa na utaratibu wa kufanya
makongamano kama hayo wakati wa sherehe za Pasaka kwa kuwakusanya wanafunzi hao na kuwafundisha masuala mbalimbali
ya maadili.
Alisema suala kubwa wanalosisitiza
ni kujiepusha na madawa ya kulevya kwa vijana hao sambamba na tabia zote
zinazopelekea kutumbukia katika vitendo viovu na kuongeza kuwa wanawafundisha
kufanya juhudi na maarifa wakiwa shuleni ni waweze kufanikiwa katika maisha
yao.
0 comments:
Post a Comment