Pages

Subscribe:

Friday, 4 April 2014

NYALANDU AFUNGUA MKUTANO WA 21 WA BARAZA LA WAFANYAKAZI NA KUSISITIZA UADILIFU KWA WATUMISHI

IMG_8384Mheshimiwa Lazaro Nyalandu akipata utambulisho kutoka kwa Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi M.K. Tarishi(wa pili kushoto) kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. N. Kazimoto (katikati), Bi B. Nassib, Katibu wa Baraza la Wafanyakazi (wa pili kulia) na Bw. B. Urassa, Katibu Msaidizi w Baraza (kulia)IMG_8392 Mhe Lazaro Nyalandu akisalimiana na baadhi ya wajumbe katika Mkutano wa 21 wa Baraza la Wafanyakazi.IMG_8400Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bibi M.K. Tarishi akitoa salamu za kumkaribisha mgeni rasmi.
IMG_8434Mhe Lazaro Nyalandu akitoa nasaha kwa wajumbe wa baraza.
……………………………………………………..
Mkutano wa 21 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii umefunguliwa rasmi leo tarehe 4 Aprili 2014, Mjini Morogoro na Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Mhe Lazaro Nyalandu ambaye amewaasa wajumbe kujenga mazoea ya kufanya kazi kwa uadilifu na nidhamu ili kufikia malengo na vipaumbele vya Wizara. Alisema ‘malengo na vipaumbele hivyo tutavifikia, kwa kuwa na Wafanyakazi hodari, wabunifu, waadilifu na wenye nidhamu ya hali ya juu’.
Aidha Mhe Lazaro Nyalandu aliendelea kufafanua  kuwa Sekta ya Maliasili na Utalii ni muhimu katika uchumi wa nchi na ustawi wa jamii kwa kuwa shughuli zake zinagusa moja kwa moja maisha ya kila  siku ya jamii iwe mjini au kijijini.
Kutokana na umuhimu wa sekta hii kugusa maisha ya kila siku ya jamii, Mhe Nyalandu alisisitiza kuwa Baraza hili linatakiwa kujua kwa undani changamoto  zinazoikabili Wizara na kushauri njia za kuleta ufanisi na kutatua matatizo yanayojitokeza kwa kutumia sera na sheria za Wizara na za nchi kwa ujumla.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi M.K. Tarishi alimshukuru mgeni rasmi Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe L. Nyalandu kwa kutenga muda wa kuhudhuria mkutano huu na kutoa nasaha na baraka zake kwa wajumbe. Pia alisema anaamini nasaha na baraka hizo zitawafikia watumishi wote nchini kupitia uakilishi wa wajumbe wa Baraza.
Pamoja na kusisitiza uadilifu na nidhamu, Mhe L. Nyalandu pia aliongelea suala la ugonjwa wa UKIMWI ambapo alishauri kuwa ni vyema kwa Watumishi wote wa Wizara na kwa Watanzania wote achukue hatua za kujikinga na Janga la UKIMWI kwa sababu linamaliza rasilimaliwatu na hivyo kuathiri uchumi wa nchi kwa ujumla.
Aidha alisema Ukimwi unadhoofisha uwezo wa Mtumishi kutekeleza majukumu yake na hatimaye kupunguza nguvu kazi ya Wizara.
Mkutano wa 21 wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Maliasili na Utalii ambalo litakaa kwa siku mbili (4-5 Aprili 2014) litajadili Sera, Kanuni na Mkakati wa Kupambana na Ukimwi nchini; Makadirio ya Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2014/15; Rasimu ya Kanuni za Maadili na Mwenendo wa Wizara ya Maliasili na Utalii; na Mpango wa Mafunzo wa Wizara kwa kipindi cha mwaka 2013/14-2015/16; pamoja na utekelezaji wa Maazimio tuliojiwekea kwenye Mkutano wa 20. Vile vile litajadili Taarifa ya Utendaji wa Kazi za TUGHE, Tawi la Wizara; na Taarifa ya Mfuko wa Rambirambi Wizara ya Maliasili na Utalii (MRAMU).

0 comments:

Post a Comment