Pages

Subscribe:

Thursday 10 April 2014

KILOMBERO KUFANYA MATEMBEZI YA KUMUENZI PRINCE BERNHALD

 Balozi wa amani nchini Risasi Mwaulanga aliyebeba mtoto mgongoni, akiwa na watalii waliotembelea maporomoko ya hifadi ya Udzungwa yaitwayo Sanje.


 Hayo ni maporomoko ya Sanje katika hifadhi ya Udzungwa wilayani Kilombero mkoani Morogoro. ni mita zipatazo 1000 kutoka usawa wa bahari, umbali wa kilomita 5.

 Hotel ya Twiga inayomilikiwa na hifadhi hiyo ya Udzungwa.

 Mbega mweusi ambaye anapatikana katika hifadhi hiyo.

 Mbega mwekundu anapatikana katika hifadhi hiyo pekeee.

 Watalii wakiwa katika moja ya njia ya utalii wa kutembea kwa miguu, katika hifadgi ya Udzungwa utalii unaofanyika zaidi ni wa kutembea kwa miguu kutokana na maeneo mengi ya vivutio vyake vya utalii viko milimani.

 Maporomoko ya Sanje katika hifadhi hiyo.

 Balozi wa amani Nchini Risasi Mwaulanga akiwa na familia yake baada ya kumaliza kupanda mlima huo kwa takribani masaa mawili .


 Baadhi ya watalii wakipita katika moja ya daraja la asili kuelekea katika maporomoko ya Sanje.

Maporomoko madogo ambayo unatembea kwa umbali wa kilomita 2 ni ya prince Bernhard na kwamba hayo yanafikika kwa urahisi kutokana na kutokuwa na milima mirefu.

 Kwa habari zaidi soma hapa.


BALOZI wa Amani nchini risasi Mwaulanga amesema anampango wa kuandaa matembezi ya mshikamano ya kumshukuru aliyekuwa mume wa  Malkia wa Uholanzi Prince Bernald kwa kugundua na kuhifadhi hifadhi ya Udzungwa katika wilaya ya Kilombero mkoani hapa.


Alisema hayo juzi wakati alipotembelea maporomoko ya Prince Bernald yaliopo ndani ya hifadhi ya Udizungwa wakati wa ziara yake maalumu ya kutangaza utalii wananchi.

Alisema aliona ipo haja ya kuandaa matembezi hayo kwa lengo la kumshukuru kiongozi huyo ambaye ameacha historia kubwa hapa nchini ambayo kwa sasa imekuwa kivutio kikubwa kwa watalii.

Alisema kuwa matembezi hayo yatashirikisha wananchi Uholanzi na Tanzania kwa lengo la kuonyesha mshikamano katika kumuenzi Prince Bernald  sambamba na kuweka mahusiano mazuri baina ya nchi hizo ili kudumisha utalii.

‘’ Kwa kufanya hivyo kutasaidia watalii wengi kutoka nchi hiyo kuja kutalii na hivyo nchi yetu itaongeza uchumi wake,, alisema

Awali akitoa taarifa juu ya hifadhi hiyo muhifadhi mkuu wa  hifadhi ya Udzungwa Uruka Mtui  alisema hifadhi hiyo ilipandishwa hadhi mwaka 1992 kutoka kutoka msitu wa hifadhi na kuwa hifadhi ya taifa.

Alisema wakati ikiwa msitu wa hifadhi ilikuwa chini ya ufadhili wa mfuko wa hifadhi ya mazingira Duniani (WWF) ambapo Prince Bernald alikuwa ndiye mwanzilishi wa mfuko huo na kwamba wakati hifadhi hiyo inaanzishwa yeye ndiye alikuwa mgeni rasmi na ndipo eneo hilo la maporomoko likapewa jina lake.
Mkuu wa idara ya Utalii katika hifadhi ya Udzungwa Happyeness kihemi alisema katika hifadhi hiyo wanatembelewa na watalii zaid ya 7000 kwa mwaka huku watalii wengi wakiwa kutoka nchi za Ulaya.



0 comments:

Post a Comment