Pages

Subscribe:

Friday 28 February 2014

AJALI MBAYA YATOKEA JIONI HII MWEKA ,MOSHI VIJIJINI YAHUSISHA VX NA DALADALA

Ajali imehusisha gari ya abiria aina ya hiace inayofanya safari zake kati ya Mweka na moshi mjini  na landcruiser VX iliyokuwa  imewabeba  wanafunzi wa chuo cha usimamizi na uhifadhi wa wanyama pori Mweka kilichopo Mweka , Moshi vijijini.Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyobwana Fred Mushi amesema kuwa gari aina ya landcruiser VX iligonga daladala  hiyo  iliyo kuwa imesimama kupakia abiria kwenye kituo kimoja maarufu kwa jina la Kona. Ajali hiyo imetokea muda wa saa 10.30 jioni hii

MTOTO Adolotea Njavike(1.4) anaomba msaada wa matibabu kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufanyiwa upasuaji kutokana na Kichwa na Kiwiliwili kuungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.

MTOTO Adolotea Njavike(1.4) ambae Kichwa na Kiwiliwili vimeungana baada ya kupata na ajali ya Moto akiwa na mama yake Mzazi.



Mama Mkubwa wa Mtoto huyo, Salome Kiegu(35) mkazi wa Mtaa wa Maendeleo Iyunga Jijini Mbeya anasema Mtoto huyo akiwa na mama yake walipata janga la moto katika mazingira ya kutatanisha waliangukia kwenye moto ambapo Mtoto huyo aliungua vibaya.

Wednesday 26 February 2014

MBUNGE AOKOA MAISHA YA DEREVA TAXI ALIYEKUA ANATAKA KUWAWA NA WANANCHI BAADA YA KUMGONGA BODA BODA

Wananchi  wa Tanangozi  katika  wilaya ya Iringa wakimsaidia kijana mwendesha boda boda  asiye na viatu baada ya  kugongwa na taxi  yenye  namba T 6338 AWV  mbele 

Hili  ndilo gari  lilolomgonga  mwendesha boda  boda  likiwa limezuiliwa na  wananchi 
Mbunge wa  jimbo la  Ludewa Deo Filikunjombe  kushoto akiwatuliza vijana  wen ye hasira  kali  ambao  walitaka  kuliharibu kali hilo na kumpiga dereva wake 

Tuesday 25 February 2014

UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA : CCM WAENDELEA NA KAMPENI

Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu akimnadi mgombea ubunge kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mdogo wa Kalenga, Godfrey Mgimwa

Mgombea ubunge jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa akiwasili katika kijiji cha Mgera hii leo
Akiwapokea baraka kutoka kwa wazee

ANGALIA PICHA DAKTARI FEKI AKAMATWA MUHIMBILI


Hospitali ya taifa ya Muhimbili imemkamata mtu mmoja anae sadikiwa kuwa daktari feki ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa akitapeli wagonjwa wanaoenda kutibiwa katika hospitali hiyo ya taifa kwa namna  mbalimbali  Daktari huyo aliyejulikana kwa jina la Kitano Mustafa Kitani mwenye umri miaka 51 anadaiwa kuwa alikuwa anajitambulisha kama daktari upande wa akina mama katika hospitali ya Muhimbili.

Hospitali ya taifa ya Muhimbili mbali na utaratibu wa kutumia vitambulisho kwa wafanyakazi ili kuondoa tatizo kama hili, bado tatizo hili limeendelea kujitokeza

TAARIFA KAMILI SAKATA LA MADIWANI WA CHADEMA KUJIUZULU SHINYANGA

Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Shinaynga kimepata pigo kubwa baada ya madiwani wake wawili katika manispaa ya Shinyanga kutangaza kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na madai kuwa  viongozi ngazi ya taifa  wa chama hicho kundekeza  majungu,migogoro ,kudhalilisha baadhi ya viongozi  pamoja na  kuwapa majina ya wasaliti wa chama.

MBUNGE ABOOD AMWAGA MISAADA KWA VIKUNDI VYA VIKOBA NA VIJANA MORO

 Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Aziz Abood akitoa jezi kwa wachezaji wa timu ya  maskani Fc iliopo kata ya Mjimpya mjini hapa.

 Mbunge huyo akisalimia na diwani wa kata ya Mindu Hamis Msasa akiteta jambo na mbunge huyo nje ya ofisi ya mbunge huyo jana.

 Mbunge wa jimbo la Morogoro Aziz Abood akitoa hundi kwa kikundi cha wanawake cha vikoba cha mjini hapa.


 Viongozi wa kikundi cha vikoba cha wanawake polisi cha mjini hapa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupokea hundi shilingi 300,000 kwaajili ya kutunisha mfuko wao kutoka kwa mbunge wa Morogoro mjini.


 mbunge huyo akitoa hundi kwa kikundi hicho cha wanawake polisi
 kikundi cha wanawake cha kupika cha Mazimbu mjini hapa wakipokea vyombo  vya kufanyika kazi kutoka  kwa mbunge huyo

 Habari zaidi soma hapa


MBUNGE wa jimbo l a Morogoro mjini Abdullazizi Abood ametoa msaada wa fedha na vitu mbalimbali vyenye thamani ya  shilingi milioni  2.53 kwa vikundi vya wanawake nane vilivyopo katika manispaa ya Morogoro ikiwa ni kuelekea siku ya wanawake duniani.

Akitoa hundi ya fedha kwa vikundi hivyo Abood aliwataka wanawake hao kuhakikisha wanatumia msaada huo wa fedha kwa manufaa ya kujikomboa kiuchumi na kuondokana na utegemezi.

Aidha Abood alisema kuwa kuwapo kwa vikundi vya wanawake katika maeneo mbalimbali nchini kunalenta maendeleo ya dhati na hata wanawake kuthaminiwa na waume zao kutokana na kuongezeka kwa kipato katika familia zao.

“Misaada ninayotoa kwamba nina fedha sana ila najua majukumu waliyonayo wanawake nchini hasa katika jimbo langu kwani nimeweza kufanya ziara jimbo langu lote na kujionea matatizo ya wanawake yanayowakabili,na nia yangu ni kuhakikisha wanajikwamua na umaskini na kuweza kujitegemea wenyewe”alisema.

Mwenyekiti wa kikundi cha Polisi Slab vikoba Ukende Ugula akizungumza kwa niaba ya wenzake alimuomba mbunge huyo kuendelea kutetea haki za wanawake na ,watoto na kuhakikisha masuala ya wanawake yaliyopo katika rasimu ya katiba yanaingizwa katika katiba mpya.

Pia alisema kuwa bado kunatatizo la wanawake wengi hasa wa vijiji kutojua haki zao,na kumtaka mbunge huyo kutokata tamaa ya kusaidia wanawake hasa katika mkoa wa Morogoro.

Vikundi vilivyopatiwa msaada ni Tushikamane,Polisi Slab vikoba,Dirisha la maendeleo kutoka chuo cha maendeleo morogoro,Tujishike,Changamka,Ushindi,Tushikamane bigwa na kikundi cha mapishi cha Modeco kilichopatiwa vifaa vya kupikia na kugawa chakula.


Sunday 23 February 2014

ANGALIA AJALI YA GARI NDOGO LAGONGANA NA PIKIPIKI LA KUJERUHI

ANGALIA PICHA ZAIDI AJALI YA MIKESE ILIYOUA DEREVA WA LORI LA MAFUTA

Lori la mafuta baada ya kuteketea kwa moto kijiji cha Fulwe, Mikese mkoani Morogoro.

ANGALIA PICHA AJALI MBAYA YATOKEA MIKESE MOROGORO LEO ASUBUHI.

 Ankle habari. Leo asubuhi eneo la Mikese, Morogoro, tumekutana na na ajali  mbaya sana ya magari mawili, moja la mafuta, kugongana uso kwa uso na kutumbukia mtaroni na yote kushika moto. Inasadikiwa mtu mmoja ambaye ni dereva wa magari hayo kateketea kabisa kwa moto. Picha na Mdau Sixmund

 Hakuna cha kufanyika kutokana na moto mkubwa na moshi mwingi wakati magari hayo yakiteketea

ANGALIA PICHA MAUWAJI YA USTADHI NA MTOTO JAMALI SALUM L MBAGARA CHARAMBE

mwili wa maremu mtoto Jamali aliechinjwa na ustadhi mbagala charambe mianzini
mwili wa marehem ustadhi mohamed kurangwa aliemchnja mtotoukishushjwa katika hospitali ya Temeke

Saturday 22 February 2014

ROLI LAWAKA MOTO MORO




ROLI LIMEWAKA MORO KATIKA ENEO LA MIKESE WILAYA YA MOROGORO, KATIKA BARABARA YA MOROGORO NA DAR ES SALAAM. GARI HILO LIMEZIBA NJIA NA KUZUIA MAGARI MENGINE KUPITA. HABARI ZAIDI TUTAWALETEA HIVI PUNDE

ASKOFU MORO AOMBA SERIKALI KUWAONDOLEA KODI KATIKA VIFAA VYA HUDUMA ZA AFYA

 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha afya cha Mtakatifu Thomas kilichopo kata ya kilakala manispaa ya Morogoro.
 Askofu wa jimbo katoriki la Morogoro Telesphori Mkude akizungumza katika hafla hiyo

 Mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amazni naye alipata fulsa ya kuzungumza katika hafla hiyo.

 Diwani wa kata ya Kilakala akielezea jinsi walivyofarijika kupata kituo hicho.

 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Bendera akiwa na viongozi wenzake katika picha ya pamoja.

 Mkuu wa shirika la damu takatifu sista Claudia Maria akielezea historia ya kituo hicho.

 Hii ni moja ya wodi ya wanaume katika kituo hicho.

 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizunguka kukagua mazingira ya kituo hicho

 Wauguzi na wananchi wa eneo la jirani na kituo hicho wakifurahia katika uzinduzi huo.

 Ulifika wakati wa kufungua muziki, viongozi hao waliondoka na miondoka ya mfano wa nyimbo za kabila la Kichaga wanaoshikana mikono .

Namie sikuwa mbali sanaa, hao wabibi nimekuwa nao tangu utoto wangu, tulikuwa tukisali pamoja katika kanisa la Kituo hicho, Tulikuwa wote katika Rejio Maria, nilifarijika sana nilipowaona nikaona niweke kumbukumbu.

Habari kamili soma hapa


ASKOFU wa jimbo Katoriki la Morogoro Teresphori Mkude ameomba serikali kuwasaidia kuwaondolea kodi  kwa vifaa vya huduma za afya  wanavyoingiza ili waweze kuboresha zahanati na vituo vya afya katika jimbo hilo.

Alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kituo cha afya cha St Thomas kilichopo kata ya Kilakala katika manispaa ya Morogoro.

Alisema kuwa wanafikiria zaidi kuboresha huduma ya afya hususani vijijini na kwamba ili wafanikiwe  hakuna budi kwa serikali kuangalia uwezekano wa kuwaondolea kodi hiyo.

Alisema kuwa tayari wameshaomba wafadhili kutoka nje kwaajili ya kuwasaidia vitanda vitatu kwaajili ya kujifungulia wajawazito  ili waweze kupeleka katika zahanati yao iliopo Maskati Turiani wilayani Mvomero.

Pia aliomba serikali ya wilaya ya Mvomero kuwaboreshea barabara ya kwenda Maskati ili iweze kufikika kwa nyakati zote na kuweza kuwasaidia wagonjwa kufika katika zahanati hiyo kwa urahisi.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo alisema kuwa  Serikali inafarijika kuona mashirika ya dini yanapotoa huduma hizo  ambapo aliwahakikishia kuwa nao bega kwa bega katika kufanikisha huduma hizo.

‘’ Tangu miaka ya zamani mashirika ya dini ndio yaliweza kutoa huduma bora zaidi za afya na elimu, na tunatambua mchango wenu ndio maana hata mnapohitaji watumishi hatusiti kuwapatia’’ Alisema

Naye mkuu wa shirika la damu takatifu linalomiliki Kituo hicho cha Afya sista Claudia Maria alisema kuwa kituo hicho kilianzishwa mwaka 1982 kama zahanati ambayo ilikuwa ikitoa huduma  kwa wagonjwa wa nje .

Alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa huduma hiyo kwa wananchi wa manispaa ya Morogoro waliamua kuboresha na kukipandisha hadi hadi kufikia kituo cha afya .

Alisema kuwa kwa sasa  wanampango wa kujenga chumba cha upasuaji ili wajawazito wanaopatwa na matatizo waweze kupata huduma hiyo hapo.

Alisema kuwa kituo hicho  kinahudumia wagonjwa 1074 kati ya hao 289 ni wa mfuko wa bima ya afya na kuongeza kuwa changamoto walionayo ni mfuko huo kuchelewesha malipo na  kusababisha upungufu wa dawa .




Friday 21 February 2014

RAIS WA SHIRIKISHO LA RIADHA NCHINI MTAKA AMFAGILIA MEMBE KWA KUFADHILI WANARIADHA 40 MAFUNZO NJE YA NCHI







RAIS wa shirikisho la riadha Tanzania RT  Antoni Mtaka  amemshukuru waziri wa mambo ya nje Bernard Membe kwa kufadhili wanariadha 40 kwenda nchi za China Uturuki na Kenya kwaajili ya mafunzo.

Mtaka ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Mvomero alisema hayo Februari 21 mwaka huu wakati akiongea na waandishi wa habari mjini hapa.

Alisema kuwa mafunzo hayo ni maandalizi ya mashindano ya jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu nchini Glassgon nchini Scotland.

Alisema kuwa wanariadha 20kati ya hao watakwenda nchini China,  wengine 10 watakuwa nchini Uturuki,  na 10 watakwenda nchini Ethiopia  sambamba na makocha 6 ambao nao wanakwenda kupata uzoefu.

Alisema kuwa wanariadha 2 watakwenda nchini Kenya kwa ofa ya waziri wa habari utamaduni na michezo Finela Mkangala ambaye alitoa ofa hiyo wakati wa mbio za kifimbo cha malkia Elizabeth.

Alisema kuwa wanariadha wengine 35 watakuwepo hapa nchini katika mikoa ya Dodoma na Manyara ambao watachujwa na hao watakaotoka nje na kwenda katika mashindano hayo ya jumuiya ya Madola.

Alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuboresha mchezo huo na kuweza kuleta ushindi hapa nchini badala ya kubakia kuwa kama washiriki au watalii kama ilivyokuwa hapo awali.

‘’ Hatutaki kubakia kama watalii au washiriki sasa, tunataka kuwa washindi, watakaokwenda ni wale tu wanaokidhi vigezo’’ Alisema

Pia Mtaka alitoa wito kwa wadau na viongozi mbalimbali kuiga mfano huo kwa kuwasaidia wanariadha hapa nchini ili kukuza mchezo huo.

Alisema kuwa mbio hizo zitakazoshindaniwa ni pamoja na mbio fupi, mbio za kati na mbio ndefu sambamba na marathon , miruko na mitupo.