Meneja wa FINCA Ben Mwanyapu akikabidhi msaada wa chakula kwa waathirika wa mafuriko katika kambi ya Magole wilayani Kilosa na kuahidi kuwafutia madeni waathirika hao,
Afisa afya wa mkoa wa Morogoro Lymo akionyesha kichanja cha kuhifadhia vyombo ili kuepuka magonjwa mbalimbali kwa wahanga hao
Wanafunzi waliofika katika godauni la mkoa la kuhifadhia chakula cha msaada katika eneo la dakawa kwaajili ya kupata msaada huo
Baadhi ya waathirika wa mafuriko wakiwa katika foleni ya kusubiri
Habari zaidi soma hapa chini
KAMPUNI ya fedha ya FINCA tawi la Morogoro imesema inawafutia deni la zaidi ya milioni
30 zilizokopwa na wanachama wake ambao walipatwa na Mafuriko wilayani Kilosa
mkoani hapa ili waweze kujipanga na kukopa tena kwaajili ya kuendelza biashara
zao.
Meneja wa kampuni ya FINCA tawi la Morogoro Ben Mwanyapu
alisema hayo jana wakati alipotembela kambi
ya waathirika wa mafuriko hayo katika eneo la Magole wilayani Kilosa na
kutoa msaada wa unga wa mahindi na maharage
yenye thamani ya shilingi milioni 1.2.
Alisema kuwa kwa sasa wanachofanya ni kuhakiki wanachama hao
na kwamba taratibu hizo zikikamilika watafanya zoezi hilo.
Aliwataka waathirika hao kujipanga upya kwaajili ya shughuli
za kujikwamua kiuchumi badala ya kukataa tamaa kutokana na mafuriko hayo
yaliowatia hasara kubwa.
Hata hivyo aliwahakikishia wanachama hao kuwa akiba zao zipo
hivyo watazitumia kwaajili ya kukopa mikopo yao
hiyo.
Aliwataka kuwa wavumilivu
katika kipindi hiki kigumu na kwamba janga hilo sio liwafanye wakate
tamaa ya maisha na badala yake wafikirie jinsi ya kujikwamua na kurudia katika
hali yao ya zamani.
Kwa upande wao waathirika hao walishukuru kampuni hiyo kwa
kuwathamini na kuwasamehe deni hilo ambalo lilikuwa ni mzigo mzito uliotokana
na kuzolewa kwa mali zao zote zikiwemo biashara zao.
‘’ Tulikuwa tunafikiria jinsi gani tutalipa fedha hizo,
maana mitaji yetu yote imeondoka na maji, lakini sasa tumeingia na matumaini
mapya’’ Alisema Joseph Simoni.
Kwa upande wao wanawake waliopo katika kambi hiyo
wamalalamikia kukosa haki yao ya msingi ya kupata unyumba kutokana na kulala
kwa jinsia moja na hivyo kushindwa kulala na waume zao.
‘’ Kwa kweli hali hii ni ngumu kweli, wanaume zetu wanakuwa
wakali, wakija wanakukalipia nipikie uji, kumbe tatizo ni tendo la ndoa, na
wakati mwingine tunalazimika kufanya tendo la ndoa usiku machakani hali ambayo
inahatarisha maisha yetu,, Alisema Asha Mohamed.
Naye afisa maendeleo ya jamii wa wilaya ya Kilosa alisema kuwa kwa sasa chakula
wanachopata kinawasaidia kudumua kwa siku 34 hvyo tatizo la chakula sio kubwa.
Aliomba wasamalia
wema wanaoweza kuwasaidia misaada pia wasaidie aina tofauti za mboga kama dagaa
,chumvi na mafuta ili wahanga hao waweze
kubadilisha mlo
0 comments:
Post a Comment