RAIS wa shirikisho la riadha Tanzania RT Antoni Mtaka amemshukuru waziri wa mambo ya nje Bernard
Membe kwa kufadhili wanariadha 40 kwenda nchi za China Uturuki na Kenya
kwaajili ya mafunzo.
Mtaka ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Mvomero alisema hayo
Februari 21 mwaka huu wakati akiongea na waandishi wa habari mjini hapa.
Alisema kuwa mafunzo hayo ni maandalizi ya mashindano ya
jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika mwezi Julai mwaka huu nchini
Glassgon nchini Scotland.
Alisema kuwa wanariadha 20kati ya hao watakwenda nchini
China, wengine 10 watakuwa nchini
Uturuki, na 10 watakwenda nchini
Ethiopia sambamba na makocha 6 ambao nao
wanakwenda kupata uzoefu.
Alisema kuwa wanariadha 2 watakwenda nchini Kenya kwa ofa ya
waziri wa habari utamaduni na michezo Finela Mkangala ambaye alitoa ofa hiyo
wakati wa mbio za kifimbo cha malkia Elizabeth.
Alisema kuwa wanariadha wengine 35 watakuwepo hapa nchini
katika mikoa ya Dodoma na Manyara ambao watachujwa na hao watakaotoka nje na
kwenda katika mashindano hayo ya jumuiya ya Madola.
Alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuboresha mchezo huo na
kuweza kuleta ushindi hapa nchini badala ya kubakia kuwa kama washiriki au
watalii kama ilivyokuwa hapo awali.
‘’ Hatutaki kubakia kama watalii au washiriki sasa, tunataka
kuwa washindi, watakaokwenda ni wale tu wanaokidhi vigezo’’ Alisema
Pia Mtaka alitoa wito kwa wadau na viongozi mbalimbali kuiga
mfano huo kwa kuwasaidia wanariadha hapa nchini ili kukuza mchezo huo.
Alisema kuwa mbio hizo zitakazoshindaniwa ni pamoja na mbio
fupi, mbio za kati na mbio ndefu sambamba na marathon , miruko na mitupo.
0 comments:
Post a Comment