VIONGOZI wa dini mbalimbali nchini wametakiwa kutohubiri
chuki na badala yake wahubiri amani na utulivu bila kujali mitazamo ya
mathehebu tofauti.
Katibu wa jimbo Katoriki Morogoro padre Luitfuid Makseyo
alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika semina ya
viongozi wa dini katika kuchangia amana na utulivu nchini ilioandaliwa na
kamati ya Kitaifa ya kuzuia mauaji ya Kimbari, uharifu wa kivita/uharifu dhidi
ya binadamu na ubaguzi.
Aidha alisema kuwa kazi kubwa ya viongozi wa dini ni
kubawabilisha watu kutoka katika matendo maouvu na kuwa na mioyo safi na hivyo
kuepuka matendo ya kiarifu yanayosababisha uvunjifu wa amani.
‘’ Kazi ya viongozi wa dini ni kuhakikisha mwajambazi, wezi,
mafisadi na waarifu wa aina zote wanabadilika na kumcha Mungu kupitia maandiko
matakatifu’’ Alisema
Naye Nabii Joshua Aram wa kanisa la Sauti ya Uponyaji ya
mjini hapa alisema kuna kila sababu kwa viongozi wa dini kuwa na
mshikamano bila kujali mathehebu
wanayotoka sambamba na kukaa pamoja kuombea nchi ili izidi kuwa na amani na
utulivu.
Alisema kuwa ni kazi ya viongozi wa dini kujenga tabia ya
kuwashauri viongozi wa dola katika masuala mbalimbali muhimu ambayo yatasaidia kudumisha amani ya
nchi na maendeleo kwa ujumla.
Kwa upande wake Sheikh Thabit Nouman Jongo kutoka wizara ya
katiba na sheria Zanzibar alisema kuwa amani na utulivu ni muhimu katika dini
zote kwani ikipotea hakuna mtu anayeweza kuabudu.
Alipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutoa uhuru wa kuabudu
kwa kila dini kwani pasipokuwa na uhuru wa kuabudu amani haipo.
‘’ hata katika vitabu vya dini yapo maandiko yanaoelezea amani na utulivu,
bila amani uhuru wa kuabudu haupo’’ Alisema.
Awali akifungua semina hiyo mkuu wa wilaya ya Morogoro Said
Amanzi alisema kuwa Serikali inaheshimu imani za dini zote na ndio maana imetoa
uhuru wa kuabudu bila kujali dini.
Alisema kuwa ni vema madhehebu ya dini kila moja likaheshimu
imani ya waumini wengine kwani kufanya hivyo kunajenga amani na utulivu.
Mwenyekiti wa kamati hiyo felista Mushi alisema kuwa
Tanzania ni moja ya nchi 12 za maziwa makuu zilizosaini mkataba wa kimataifa wa hitifaki
ya kuzuia mauaji ya Kimbari yaliotokea mwaka 1994 nchini Rwanda na kwamba
katika mkataba huo kila nchi ilitakiwa kuunda kamati hizo.
Alisema kuwa lengo la kuwapatia semina viongozi wa dini ni
kutokana na kwamba wanagusa imani za watu wengi na kwamba kupitia wao suala la
amani likihubiriwa vizuri kamwe haiwezi kupotea na nchi haiwezi kuwa na
machafuko ya aina yeyote.
0 comments:
Post a Comment