Pages

Subscribe:

Tuesday, 13 August 2013

WAKULIMA WAFANYA SHEREHE NYINGINE YA NANENANE MVOMERO


Kutokana na sherehe za sikukuu ya wakulima NANE NANE kuadhimishwa mjini na kuacha wakulima walio wengi vijijini, wakulima wa wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wameadhimisha sikukuu hiyo August 12 mwaka huu kwa lengo la kuwathamini wakulima wadogo ili kuleta maendeleo endelevu kwa wakulima.
Sherehe hiyo  imefanyika katika kijiji cha Mvomero ambayo imeandaliwa na wakulima wataalam kutoka vikundi 88 vyenye wanachama zaidi ya 2500 wa tarafa ya Mvomero na Turiani wakiwa na kauli mbiu isemayo “kuleta maendeleo endelevu ni lazima kuwajali na kuwathamini wakulima wadogo”ambapo katika sherehe hiyo wakulima wamenufaika na elimu ya kilimo kutoka kwa wataalam wa kilimo na kutumia furusa hiyokuiomba serikali kutoa pembejeo za kilimo kwa wakati.


Afisa masoko wa mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania MVIWATA  Ikunda Terry ambao ndio wamedhamini sherehe hiyo amesema kupitia sikukuu hii wakulima watahamasika kujiunga katika vikundi vya uzalishaji kwa kuwa wakulima wa vijijini wanashindwa kufika katika viwanja vya maonyesho ya wakulima vilivyopo mijini na kupata elimu huku mkurugenzi wa wilaya ya Mvomero Walece Kalia amesema migogoro ya wakulima na wafugaji wilayani humo inasababishwa na viongozi wa serikali za mitaa kupokea rushwa  hivyo wananchi wanapaswa kutoa taarifa ngazi za juu ili kpatiwa msaada
Sherehe hiyo ni ya pili tangu ilipoanzishwa mwaka jana ikilenga kutoa elimu ya kilimo kwa wakulima wadogowadogo wanaoshindwa kufika mjini katika viwanja vya maonyesho ya  sikukuu ya wakulima kwa kigezo cha umbali.

0 comments:

Post a Comment