Pages

Subscribe:

Wednesday, 19 March 2014

WAANDISHI WA HABARI MORO KUJIUNGA NA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF

 Mwenyekiti wa Club ya waandishi wa  habari mkoani Morogoro Ida Mushi akifungua semina ya siku moja kwa waandishi wa habari juu ya uendeshwaji wa mfuko wa pensheni  LAPF jana mkoani haoa
 Katibu wa club ya waandishi wa habari mkoani Morogoro  Adeid Dogoli akitoa neno la utangulizi katika semina hiyo.

   Meneja ya Mashariki wa Kanda wa mfuko Lulyaya Sayi wakati akitoa mada  juu ya uendeshaji wa mfuko wa LAPF kwa waandishi wa habari mkoani Morogoro.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifutilia semina hiyo kwa makini


MFUKO  wa Penshen wa LAPF (Local Authorities Pensions Fund) umekusanya jumla ya shilingi bilion 119.2 kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 na kutumia kiasi cha cha shilingi bilioni 56.8 kulipa wanachama wake pensheni
   Meneja ya Mashariki wa Kanda wa mfuko huo,Lulyaya Sayi,alisema kuwa mfuko wa LAPF una uwezo kifedha wa kijiendesha wenyewe zaidi ya miaka 100 bila kuterereka kutokana na kuwa na mfumo imara wa uwekezaji.
Sayi alisema mfuko huo umekuwa ukifanya vizuri katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo bila kupata ushindani kutoka kwa mifuko mingine ya kijamii inayotoa pensheni kama wao na bado wanaendelea kufanya vizuri katika miaka inayokuja na kuongeza ubora wa ufanisi wa kazi
Alisema mfuko unakabiliwa na changamoto nyingi  ilia kutokana na utendaji wao wanakabiliana nazo na kuweza kuzipatia ufumbuzi,changamoto hizo ni ufinyu mdogo wa wanachama kuhussu mfuko,propaganda za watu wengine kusemea mfuko na kusababisha wanachama kwenda katika mifuko mingine
Alisema   mfuko umekuwa ukiingia mkataba na serikali katika ujenzi wa miradi mbalimbali ndani ya nchi,hivi sasa wameingia mkataba na manipsaa ya morogoro katika ujenzi wa hoteli ya kisasa katika stendi kubwa ya mabasi ya mkoa iliyopo eneo la msamvu ambayo itagharimu kiasi cha shilingi bilioni 35 kwa kipindi cha miezi 18
Kwa upande wake Afisa Matekelezo wa mfuko wa LAPF Kanda ya Mashariki Charles Mahanga alisema kuwa kutokana na sheria ya mifuko ya umma mtumishi wa serikali ana uwezo wa kuchagua mfuko wowote unaoupenda ila imetokea hivi sasa baadhi ya watu ama waajiri kumlazimisha mtumishi kuingia mfuko fulani kutokana na masalahi yake
Mahanga alisema sekta ambayo imekuwa tatizo kwa muda mrefu ni walimu ambao idadi yao ni kubwa na wepesi sana kupotoshwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya walimu ama walimu waliowatangulia kazini kujiunga katika mifuko mingine kutokana na mazoe waliyokuwa nayo toka kipindi cha nyuma ambacho kulikuwa na mfuko mmoja tu wa PSPF
Hata hivyo alisema kuwa mfuko umejipanga kutumia vyombo vya habari kutoa elimu kwa wanachama wake,kupita katika vyuo mbalimbali,katika warsha,lengo ni kuhakikisha wanachama wanapata uelewa wa kutosha kuhusu mfuko,wanaongeza idadi ya wanachama na kudumisha utendaji bora wa kazi.

0 comments:

Post a Comment