Pages

Subscribe:

Monday 10 March 2014

MSAADA UNAHITAJIKA :JAMANI NAKUFA, NIOKOENI

Ngaweje Said anayeteseka na gonjwa asilolijua.

WANASEMA ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni, ni kweli! Ngaweje Said (39), mkazi wa Kijiji cha Zinga, Bagamoyo, Pwani anateseka na gonjwa asilolijua ambapo nyama kubwa imeota toka juu ya uso upande wa kushoto na kumwagikia kifuani, Uwazi lilikutana naye uso kwa uso. Akizungumza na mwandishi wetu akiwa nyumbani kwake kijijini hapo juzi, Ngaweje alisema:“Ugonjwa huu ulinianza nilipozaliwa tu mwaka 1975 pale Hospitali ya Bagamoyo. Kilianza kipele, lakini kadiri nilivyokuwa nikikua, kipele nacho kilikua.

“Sikujua kama itafikia hali hii. Hata wazazi wangu nao hawakujua, waliamini baada ya tiba kipele kitanywea, lakini wapi!

“Baadhi ya watu walishauri nipelekwe Hospitali ya Muhimbili ambako kuna madaktari bingwa. Kweli, mwaka 1979, baba alinipeleka Muhimbili ambako nilipata tiba na kurudi nyumbani lakini kipele kilizidi kukua.
“Mwaka 1995, mimi mwenyewe nilirudi tena Muhimbili. Safari hii madaktari waliniambia watanifanyia upasuaji kwa awamu.SOMA ZAIDI

0 comments:

Post a Comment