Pages

Subscribe:

Tuesday 27 May 2014

BILIONI 1.5 KUTUMIKA KWAJILI YA SHUGHULI ZA UPIMAJI WILAYA YA MVOMERO

 Waziri wa ardhi nyumba na makazi Anna Tibaijuka akiangalia mabango yalioshikwa na wanafunzi wakimpongeza kwa juhudi zake za kuwapimia ardhi katika kijiji cha Lukenge Tarafa  ya Turiani wilayani Mvomero  kijiji ambacho mwaka jana  yalitokea mapigano baina ya wakulima na wafugaji kugombea ardhi na kusababisha vifo vya watu sita , na sasa kijiji hicho kimefanywa ni cha kihistoria na cha mfano.

 Waziri Tibaijuka akizindua masijala ya ardhi ambayo itatumika kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali za masuala yote ya ardhi kwa kijiji hicho.

 Wanafunzi  walimpokea waziri huyo kwa mabango yenye ujumbe mbalimbali ulioashiria kushukuru waziri huyo na watumishi wa wizara hiyo kwa kuwapimia kijiji hicho.

 Waziri huyo akionyeshwa ramani mbalimbali za kijiji hicho ambazo kwa sasa zinapatikana kijijini hapo.

 Waziri Tibaijuka akionyeshwa ramani katika eneo la Mkindo pamoja na kupewa malezo ya alama za mipaka ya mawe yanayoweka kwa sasa ambayo ni mita moja kwenda juu tofauti na yale yaliozoeleka yanayojengewa chini, mawe hayo yanaokana kwa urahisi, yanatenganisha mipaka ya kijiji na kijiji na yanakuwa yameandikwa majina ya kijiji husika.

 Mwenyekiti wa kijiji cha Lukenge Sakayo Ole Kosiando akitoa maelezo kwa waziri huyo jinsi yeye alivyoanza kulima shamba la mfano la nyasi za malisho ya Ng'ombe ambapo aliahidi ifikapo Desemba mwaka huu atakuwa amepanda nyasi hizo ekari 10,000  kwaajili ya malisho ya ng'ombe zake ili kuepusha mifugo yake kuzurula hovyo na kuingia katika mashamba ya watu hali inayosababisha migogoro baina yao na wakulima, alidai wafugaji wenzake wanambeza hawataki kulima nyasi.

 Waziri Tibaijuka akitoa hatimiliki za kimila kwa wakazi wa kijiji hicho ambao wengi wao wamejiandikisha  umiliki wa watu wawili kama mke na mume kwa lengo la kuondokana na mfumo dume.

 mama na mwanae wakipokea hatimiliki yao ya mila kutoka kwa waziri huyo.

 Wanakijiji hao wakiwa katika picha ya pamoja na waziri huyo mara baada ya kupokea hatimiliki hizo.

 Waziri huyo akikagua shamba la mfano la mwenyekiti wa kijiji hicho Sakayo  alilopanda nyasi  za malisho ya mifugo.

 Wafugaji jamii ya wamasai wakimsikilia kwa makini waziri huyo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.

 


MANISPAA MORO LAWAMANI KWA KUGEUZA UWANJA WA JAMHURI KUWA SEHEMU YA DAMPOO LAKE.

 Richard Haule mwanakikundi cha kuzoa takataka katika manispaa ya Morogoro akisukuma mkokoteni wake kuelekea katika eneo la uwanja wa Jamuhuri ambao kwa sasa limegeuzwa kama dampoo la kutupia takataka.

 Richard Haule akiwa na mwenzake ambaye badae alitoweka wakisukuma mkokoteni huo.

 Hilo ni eneo la nyuma la uwanja wa jamuhuri linalopaka na uwanja wa golf likiwa limegeuzwa dampoo.

Baadhi ya wanafunzi waliokutwa wanasoma katika eneo hilo la uwanja wa Jamuhuri jirani kabisa na dampoo hilo huku harufu mbaya na moshi vikitanda katika eneo hilo.


Habari zaidi Soma hapo chini.

CHAMA cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Morogoro kimeitaka halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuacha kugeuza eneo la uwanja wa Jamuhuri kama sehemu ya Dampoo la kutupia takataka.
 
Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli alisema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya hali halisi ya uwanja huo unaomiliki na CCM.
 
Alisema Halmashauri hiyo kupitia vikundi vyake vya uzoaji wa taka vimekuwa vikitupa takataka wanazozoa katika mitaa mbalimbali ya  Kata ya Boma na kuzitupa hapo hali inayohatarisha maisha ya watu sambamba na kuharibu mandarin ya uwanja huo.
 
‘’ Tumeshawapa taarifa ili wazoe takataka zote walizomwaga katika eneo la uwanja huo tunasubiri utekelezaji, hii ni mara ya pili sasa awali walishawahi kufanya hivyo wakazoa naona sasa wanarudia tena’’ Alisema.
 
Alisema uwanja huo ambao unategemewa kwa shughuli mbalimbali za mkoa na kitaifa unatakiwa kuwekwa katika mazingira safi na salama na sio kugeuzwa kama dampoo.
 
 Hata hivyo katibu huyo alisema wanatarajia kuboresha mazingira  yote yanayozunguka uwanja huo kwa kukata miti iliozidi ovyo .
 
Alisema sambamba na hilo pia wanatarajia kufanya ukarabati katika jingo hilo maeneo ya nje ya uwanja kwa kupiga plasta na kupaka rangi ili uweze kuvutia zaidi.
 
‘’ Tunataka uwanja wa Jamuhuri uwe kivutio cha watu kuja kupumzika na kuvuta hewa safi, tunataka kupanda miti ya maua na matunda na kuweka bustani nzuri za maua’’ Alisema.
 
Hata hivyo katibu huyo alisema wanamshukuru mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Morogoro Paskari Kihanga kwa kuwasaidia kupata kisima katika uwanja huo ambacho kitasaidia kuwa na maji ya uhakika.
 
Mmoja wa wanakikundi wanaozoa takataka katika kata ya Boma alidai kuwa yeye alipewa maelekezo ya kumwaga takataka hapo na bosi wake aliyemtaja kwa jina moja la Mama  Sanga.
 
Richard alisema  kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakimwaga takataka hapo na badae kulipia manispaa kwaajili ya kuzizoa na kwamba anaona ni utaratibu sahihi. 
 
'' Kwanza mimi nasngaa sijui nani kaamua kuzichoma hizi takataka hapa, maana baada ya kujaa huwa tunalipia manispaa alafu wanakuja kuzichoma'' alisema.
 
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika eneo jirani na dampoo hiyo walidai wanapata adha kubwa kutokana na harufu mbaya na kwamba wanaomba serikali kuchukua hatua ili kuepuka magonjwa ya milipuko yanayoweza kuwapata.
 
'' wanazidi kuzijaza mwisho zitafika hadi eneo la hosteli yetu pale, maisha yetu yapo hatarini alisema mmoja wa wanafunzi ambaye hakutaka jina lake litajwe.


Sunday 25 May 2014

MAAJABU MENGINE YAIBUKA NYUMBANI KWA MAMA MKUBWA WA MTOTO ALIEYAKAA KATIKA BOX MIAKA 4

 Nasra akiwa na mama anayemlea kwa sasa Josephin Joel kutoka kambi ya ya wazee ya Fungafunga iliopo mjini hapa, akiwa katika chumba cha ICU  hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu baada ya kufichwa katika box kwa miaka 4 na mama yake mkubwa Mariam Said baada ya mama yake mzazi kufariki mwaka 2010.
 Hali ya Narsa kwa sasa imezidi kutengemaa ,kunawili na kuonekana kama mtoto mwenye nuru kama anavyoonekana tofauti na alivyookolewa kutoka katika box siku tano zilizopita hapo mama  huyo mlezi akimpatia chakula iana ya wali na samaki anaopendelea Nasra.

 Hapo Nasra akiwa ameshika kikombe kwa mikono yake mwenyewe ilioonekana awali kutokuwa na nguvu baada ya kuomba maji ya kunywa
Petter Mwita Mtetezi wa haki za watoto mkoa wa Morogoro akiwa na Nasra katika kitanda anacholala mtoto huyo kwenye wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa  ya mkoa wa Morogoro. alishukuru vyombo vya habari kwa kutoa habari zilizofanya Nasra kupatiwa misaada mbalimbali.

 Habasi zaidi Soma hapo Chini.




 SAKATA la Mtoto  aliyeishi katika box kwa miaka 4 sasa limechukua sura mpya baada ya  nyumbani kwa mama mkubwa wake Mariam Said kukutwa  kuna  shimo kubwa lililojaa maji hali inayozidi kuwachanganya wakazi wa mjini hapa.

 Wakiongea na mwandishi wa habari hizi  mwenyekiti wa mtaa wa Azimio  anakoishi mama huyo , Tatu Mgagala alisema Mei 22 polisi walifika mtaani hapo wakiwa na mtuhumiwa huyo  na kukuta mlango umefungwa na kuamua  kuvunja  ili waweze kuingia ndani kuangalia mazingira ya nyumba hiyo.

Alisema baada ya kuingia ndani ya chumba cha Mariam walikuta kuna giza nene kutokana na chumba hicho kuzibwa na mabox na hivyo kutoa mabox hayo .

Alisema baada ya kutoa mabox hayo waliona  shimo kubwa lenye maji karibu na eneo  lilipo box alikokuwa  akiishi mtoto huyo  na alipoulizwa mama huyo kulikoni na  kuacha maji ndani huku akijua kuna ugonjwa wa Dengue alidai  maji hayo huyatumia kunawa miguu na mikono usiku kabla ya kulala.

‘’ Ndani ya nyumba hiyo sehemu zote zimesakafiwa isipokuwa eneo hilo ambalo lilichimbwa shimo hilo’’ alisema. Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo imebainika kuwa mariamu na mumewe kwa muda mrefu walikuwa hawajaoga na hivyo kulazimishwa kuoga wakiwa mbaroni .

Kwa upande  wake  mtetezi wa haki za  watoto Petter Mwita alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mei 26 mwaka huu  ni Mariam ,mumewe Mtonga Omari  na baba mzazi wa mtoto huyo Rashid Mvungi.

Alisema  ndani ya nyumba ya mama huyo zikukutwa picha ambazo zinaonyesha kuwa mtoto huyo alikzaliwa akiwa hana ulemavu na kwamba inadaiwa ulemavu huo alipata kutokana na ukatili alikofanyiwa na walezi hao

‘’ Vitendo walivyofanya wote hawa watatu ni vya kikatili na vinatakiwa kupigwa kwa nguvu zote nah ii itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hii.

Alisema baadhi ya mitandao ya kijamii ilivumisha kuwa mtoto huyo alinyanyasika na mama yake mkubwa huyo kwa madai kuwa mama yake mzazi alikufa na ugonjwa wa Ukimwi  ambapo alisema suala hilo kwa mtoto huyo halipo kwani tayari alishafanyiwa kipimo hicho na kubaini hana ugonjwa huo.

Hata hivyo alisema kwa sasa wamemtafuta mama mlezi wa Mtoto huyo kwaajili ya kumuhudumia katika huduma zote na anlipwa kwa kazi hiyo.

Naye Josephina Joel mama ambaye kwa sasa ndiye anamlea mtoto huyo alidai yeye amechukuliwa kutoka katika kambi ya kulelea wazee Fungafunga ya mjini hapa na kwamba anajua uchungu wa watoto hivyo kwake anaona hakuna changamoto zozote anazopata kwa mtoto huyo.

‘’ Mimi niliachwa na mume wangu naishi  Fungafunga nalelewa na Ustawi wa jamii kwangu kumlea mtoto huyo nachukulia kama mjukuu wangu na nafurahia na sioni shida yeyote’’ Alisema.

Aidha alisema mtoto huyo hupendela kula chipsi mayai, wali nyama au samaki pamoja na juice huku akionyesha kukataa ugali wala maziwa.

Mtoto huyo kama kitu hataki anafumba macho, kwa mfano ukimwambia nikupe ugali anakataa, au maziwa , lakini pia hapendi kuoga na ukimwambia kuoga au kula vyakula asivyotaka anakwambia badae’’ Alisema

Mwandishi wa habari hizi alifanikiwa kufika nyumbani kwa  Mvungi Kihonda eneo la Maduka kumi anakoishi na mkewe wa ndoa  kwa lengo la kutaka kujua jinsi huyo mke  alivyochukulia jambo hilo na kuwafukuza waandishi wa habari kwa madai ya kuwa wakaandike wanavyojua wao.

‘’ Ehe waandishi wa habari mnataka nini tena kwangu uwiiii, mimi sijui chochote, ondokeni,  huku akiondoka kueleka sebuleni waliko mgeni wake aliyemtmbulisha kama wifi yake huku akimwambia kwa lugha ambayo ilisikika kwa neno   lililoashiria wandishi wa habari hao’’ Alisema


 Hata hivyo  waandishi wa habari walifika nyumbani hapo   nao wakiwa nyuma yake wakarudi naye hadi eneo alipo  wifi yake na kujaribu kudadisi zaidi jambo  bila mafanikio zaidi ya kutawala kimya kwa muda wa dadki kumi na ndipo alipoohoji tena kuwa wanataka nini.

Hata hivyo mama huyo ambaye anaonekana ni mjamzito alionekana kupandisha pumzi na kushusha hali iliosababisha kushindwa kuongea na hivyo waandishi hao kuamua kuondoka kurejea mjini.

Kamanda wa polisi mkoani hapa alithibitisha kukamatwa kwa baba wa Nasra Said  na kwamba yuko nje kwa dhamana na aatafikishwa mahakamani pamoja na watuhumiwa wezake Mei 26 mwaka huu.

CCM MORO KUWABURUZA MAHAKAMANI WAPANGAJI WAKE WENYE MADENI SUGU.

CHAMA cha Mapinduzi CCM mkoa wa Morogoro kimesema kitawachukulia hatua  za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani  wapangaji wake wote ambao wanamadeni sugu  sambamba na kupitia upya mikataba kuona kama iko sahihi.

Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli alisema hayo jana wakati akiongea na Uhuru ofisini kwake  ambapo alisema kazi hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya baraza la wadhamini.

‘’ Tumeanza kufutilia wapangaji wetu wote wenye madeni sugu ili waweze kulipa , vinginevyo watakaokaidi tutawachukulia hatua za kisheria’’ Alisema

Romuli alisema hatua za kisheria watakazochukua ni pamoja na kuwafungia biashara zao  na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

Alisema pia wanafanya mapitio ya kodi za wapangaji wao kuona kama zinalingana na mazingira na wakati sahihi kwa lengo la kuhakikisha miradi hiyo inakuwa na tija kwa chama.

Aidha alisema  wakati huo huo wanapitia mikataba ya wapangaji wao kuona kama iko sahihi na kwamba wale wote ambao hawana mikataba kuwataka kujaza mikataba ili kuweza kufanya kazi nao.

‘’ Wapo baadhi ya wapangaji wetu ambao hadi sasa hawana mikataba, kwa sasa ni lazima kila mpangaji akawa na mkataba’’ Alisema

Hata hivyo alisema  lengo la kufanya hivyo ni pamoja na kuhakikisha wanaiboresha miradi hiyo ili iweze kukidhi mahitaji ya sasa kulingana na eneo husika.

Alisema Kwa sasa walianza kufanya ukarabati katika jengo la ofisi  ya CCM mkoa na kwamba  kila ilipo miradi yao itaboreshwa ili ilingane na mazingira halisi .

MANISPAAA MORO YAKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 50 KUTOKANA NA FAINI ZA LESENI ZA BIASHARA.

HALMASHAURI ya manispaa ya Morogoro imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 50  kwa wafanyabaishara walikokuwa wakiendesha biashara zao bila leseni.

Saturday 24 May 2014

MASHINDANO YA DATS YAANZA LEO, MIKOA TISA KUSHIRIKI, MSHINDI KUIBUKA NA KITITA CHA 600,000

 Mwenyekiti wa chama cha Dats Tanzania Gesase Waigama akiongea wakati wa ufunguzi wa mashindano ya mchazo huo unaoshirikisha mikoa  ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Kagera, Arusha na wenyeji wao Morogogoro ambapo katika mashindano hayo yaliodhaminiwa na bia aina ya Safari mshindi wa kwanza atatoka na kitita cha shilingi 600,000 hapo kesho.


 Baadhi ya washiriki wa mchezo huo wakifanya mazoezi kabla ya kuanza kwa shindano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Magunila  Kihonda Mjini Morogoro.


 Wahsiriki wa shindano hilo kutoka mikoa mbailimbali wakiwa katika ukumbi  huo wakishuhudia pambano hilo.


 Irene Kihupi mchezaji kutoka mkoa wa Dar es Salaam akiwa katika pambano hilo.


 Joyce Laize mchezaji kutoka mkoa wa Arusha akiwa katika pambano hilo.


 Mwenyekiti huyo wa Dats akizindua mchezo huo ili kuruhusu pambano kuanza rasmi.
 Baadhi ya wachezaji wakiwa katika pambano hilo
Frolida Namajojo katibu wa Dats mkoa wa Morogoro akiwa katika mazoezi kabla ya kuanza mchezo huo.



Habari zaidi soma hapo chini.

WANACHAMA wa chama cha Darts Taifa (TADA) wameyaomba makampuni yanayodhamini michezo mbali mbli nchini kuwekeza kwenye chama hicho ili kuweza kukuza uchumi,michezo pamoja na kuongeza pato la taifa.
 
Wanachama hao waliyasema hayo Mei 24 mwaka huu   kwa nyakati tofauti watika  wa mashindano ya mabingwa wa chama hicho yanayofanyika mkoani hapa.
 
Walisema kuwa mchezo huo ni mzuri lakini unachangamoto ya gharama ambapo alisema kuwa mara zote yanapoandaliwa mashindano hayo kila mwanachama anatakiwa kujitegemea mwenyewe.
 
Aidha waliwaomba kopa Coca Cola kuandaa utaratibu wa kupeleka mchezo huo mashuleni ili kuweza kuibua vipaji vya mchezo huo kuanzia ngazi ya shule.
 
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama hicho Kale Mwigonja alisema kuwa shindano hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Safari Lager linalenga kunua mchezo huoikiwa I pamoja na kujiandaa na Afrika Mashariki linalotarajia kufanyika mwezi juni mwaka huu Mkoani Dodoma.
 
Alisema kuwa mashindano hayo yanashirikisha virabu 32 kutoka katika mikoa mbali mbali nchni ambapo alisema kuwa washindi watapata zawadi mbalimbali ikiwemo ikombe pamoja na zawadi za pesa taslimu ambapo alisema kuwa mshindi wa kwanza atapata sh.laki 6 na kikombe ,wa pili laki 4 na kikombe na watatu laki 3.


Friday 23 May 2014

WASOMI WATAKIWA KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KUJIELIMISHA SIO TU KUJIBURUDISHA




 
WANAFUNZI  wa vyuo  vikuu wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwaajili ya  kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu masomo yao badala ya kutumia kwa kujifurahisha kama ambavyo wengi wamekuwa wakifanya hivyo.

 Hayo yalisemwa jana na  naibu  makamu  wa mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Profesa Josephat  Itika wakati wa kongamano la wanafunzi wanaosoma masomo ya uhasibu chuoni hapo.

Alisema mara nyingi wanafunzi hao wamekuwa wakitumia mitandao hiyo kwa kujiburudisha na kwamba  mitandao hiyo ingekuwa na manufaa kwao kama wangetumia kupata vitu vinavyowasaidia katika masomo yao.

“ Katika mitandao kuna fulsa nyingi za elimu, watumie fulsa hizo kuendeleza fani zao, wapunguze muda wa kuchati na meseji za kujifurahisha tu’’ Alisema.

Hata hivyo  alisema  katika kongamano hilo wanafunzi walipata fulsa ya kukutana na wataalamu mbalimbali  wa masuala yanayohusu uhasibu na kuweza kubadilisha uzoefu kwa lengo la kwenda na wakati.

Aidha alisema moja ya changamoto inayowakabili wasomi ni soko la ajira ambalo hubadilika kila siku hivyo ni lazima kuhakikisha wanakidhi mahitaji hayo.

‘’ Sisi kama waadhiri tunachofanya ni kufanya utafiti kila wakati na kujua nini kinahitajika katika soko la ajira na ndipo tunakuja kuwaletea wanafunzi wetu, sio kukazania kusoma vitabu tuu’’ Alisema.

Naye Hawa Tundui muhadhiri katika chuo hicho alisema kwa sasa wahitimu ni wengi hivyo soko la ajira  ni gumu ukilinganisha na miaka ya 1980 hivyo ni lazima kwa vyuo huria vikaangaia jinsi gani ya kuwafundisha wanafunzi wao kulingana na soko la ajira.

Alisema kongamano hilo linawabadilisha mtazamo wanafunzi hao kujua mbinu mbadala za kuweza kujiajiri badala ya kubakia na mtazamo wa kupata ajira.

Husen Maneno  mwanafunzi wa mwaka wa pili anayechukua masomo ya biashara katika chuo hicho alidai kumekuwa na ucheleweshaji wa kubadili mitala kwenda na wakati  hapa nchini na kwamba hiyo ni changamoto kubwa inayowakabili.



Wednesday 21 May 2014

MTU NA MKE WAKE WANASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA KUMFICHA MTOTO KATIKA BOX MIAKA 4, IMANI ZA KISHIRIKINA ZATAWALA

 Maria Said mama mkubwa wa Nasra, katikati ni  baba mzazi wa Nasra, Rashidi Mvungi, na kulia ni mume wa Mariam Said wakiwa katika ofisi za ustwawi wa jamii mjini Morogoro baada ya kukamatwa na kufikishwa polisi kwa tuhuma za kumficha mtoto huyo ndani ya box  kwa miaka  4 baada ya mama wa mtoto huyo kufariki dunia kwa ugonjwa wa malaria .
 Muuguzi katika Wodi ya watoto hospitali ya rufaa ya Morogoro akimuhudumia mtoto Nasra Said mara baada ya kufikishwa hopsitalini hapo kupatiwa matibabu.

Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa.



 Habari zaidi soma hapo chini.

 MUME na mke  wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa  tuhuma za kumficha mtoto kwa miaka 4 ndani ya Box .
 
Kamanda  wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema tukio hilo lilibainika Mei 20  mwaka huu majira ya saa 4.45  Asubuhi  katika eneo la mtaa Azimio kata ya Kiwanje Ndege Morogoro.
 
Alisema majirani walizingira nyumba ya mwanamke ajulikanae kwa jina la Maria Said na kutaka kuvunja ndipo polisi walipopata tarifa na kufika katika nyumba hiyo na kukuta mtoto huyo akiwa katika box.
 
Alimtaja mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Nasra Rashid Mvungi  mine na nusu  ambapo polisi ilichukua jukumu la kupeleka kesi hiyo Ustawi wa jamii ili kuendela nayo.
 
Afisa Ustawi wa jamii katika ofisi ya mkoa wa Morogoro Oswing Ngungamtitu alisema mtoto huyo alipelekwa hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa sababu alionekana kuwa na afya dhoofu.
 
Alisema alilazwa na kwamba kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii huku wakiwachukulia hatua za kisheria walezi wa mtoto huyo Mariam Said  na Mume wake Mtonga Omari.
 
 
 Baba mzazi wa mtoto huyo alisema  yeye ana mke na watato wengine wa ndoa na kwamba hakuwahi kumwambia mkewe kama ana mtoto wa nje hivyo ilikuwa vigumu kumchukua mtoto huyo na ndipo alipomkabidhi mama mkubwa wa mtoto huyo.
 
Alisema kila mara alikuwa akifika kumwona mtoto mama huyo alimwambia mtoto kalala na hivyo kushindwa kumwona na kujua hali halisi hadi siku ya tukio na kwamba alikuwa akimpatia matumizi ya mtoto huyo.
 
 
Ofisa mtendaji wa kata hiyo Dia Zongo alisema  akiwa katika kazi za kawaida katika Mtaa wa Azimio, alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mwanamke huyo, alimficha mtoto Nasra ndani ya boksi na kwamba hamfanyii usafi wala kumtoa nje.
 
Zongo alisema baada ya kupata taarifa hizo, alimtafuta Mwenyekiti wa mtaa huo, Tatu Mgagala na kuongozana naye hadi  kwenye nyumba hiyo na kuanza kumhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa akijibu kwa kubabaika na kushindwa kueleza ukweli juu ya kuwepo kwa mtoto huyo.
 
Zongo  alisema wakati mtuhumiwa akiendelea kujibu maswali, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa hali iliyowapa wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na kumkuta mtoto Nasrah akiwa ndani ya boksi nyuma ya mlango .
 
Ofisa mtendaji huyo alisema wakati wakimtoa mtoto huyo kutoka ndani ya nyumba ya mama yake huyo mkubwa, ghafla kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe, walianza kumshambulia mwanamke huyo, kitendo kilichomlazimisha (mtendaji)  kutoa taarifa polisi.
 
 
Baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi mwanamke huyo  alikiri kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa akiwa na umri wa miezi tisa na kwamba hatua hiyo ilikuja baada ya mama yake, kufariki dunia mwaka 2010.
 
 
Mtuhumiwa huyo alisema kwa mara ya mwisho, alimuogesha mtoto huyo Julai mwaka jana na kwamba alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi lililokuwa limewekwa nyuma ya mlango wa chumba cha mwanamke huyo.
 
   Hores Isaack Msaky  Dk Mshauri wa watoto katika hospitali ya mkoa wa Morogoro alikiri kumpokea mtoto huyo na kwamba tayari ameshaanzishiwa matibabu ya awali .
 
‘’ Tulimfanyia   vipimo vya awali mtoto amebainika kuwa na Nimoni pamoja na utapia mlo na sasa ameshaanza matibabu’’ Alisema
 
Alisema bado wanaendela na vipimo vingine vya XRay kubaini mtoto huyo alipata ulemavu kwa kupigwa au alizaliwa hivyo.
 
Alisema mtoto huyo anamaumivu makali sehemu ya mgongo na mikono na kwamba mwili wake pia ni mteke  kama wa mtoto mchanga hali inayowafanya kuendela kumfanyia uchunguzi wa kina zaidi.
 
Baadi ya mashuhuda wa tukio  hilo walidai kuwa mama wa mtoto huyo alifariki dunia miaka mine iliopita na kwamba  Mariamu Ni mama mkubwa wa mtoto huyo.
 
 Hata hivyo majirani hao walidai wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikina  kutokana na kwamba mama huyo anaakili timamu na analea watoto wake vema tofauti na mtoto huyo.