Baadhi ya washiriki wa mchezo huo wakifanya mazoezi kabla ya kuanza kwa shindano hilo linalofanyika katika ukumbi wa Magunila Kihonda Mjini Morogoro.
Wahsiriki wa shindano hilo kutoka mikoa mbailimbali wakiwa katika ukumbi huo wakishuhudia pambano hilo.
Irene Kihupi mchezaji kutoka mkoa wa Dar es Salaam akiwa katika pambano hilo.
Joyce Laize mchezaji kutoka mkoa wa Arusha akiwa katika pambano hilo.
Mwenyekiti huyo wa Dats akizindua mchezo huo ili kuruhusu pambano kuanza rasmi.
Baadhi ya wachezaji wakiwa katika pambano hilo
Frolida Namajojo katibu wa Dats mkoa wa Morogoro akiwa katika mazoezi kabla ya kuanza mchezo huo.
Habari zaidi soma hapo chini.
WANACHAMA wa chama cha Darts Taifa (TADA) wameyaomba makampuni
yanayodhamini michezo mbali mbli nchini kuwekeza kwenye chama hicho ili kuweza
kukuza uchumi,michezo pamoja na kuongeza pato la taifa.
Wanachama hao waliyasema hayo Mei 24 mwaka huu kwa nyakati
tofauti watika wa mashindano ya mabingwa
wa chama hicho yanayofanyika mkoani hapa.
Walisema kuwa mchezo huo ni mzuri lakini
unachangamoto ya gharama ambapo alisema kuwa mara zote yanapoandaliwa
mashindano hayo kila mwanachama anatakiwa kujitegemea mwenyewe.
Aidha waliwaomba kopa Coca Cola kuandaa utaratibu wa
kupeleka mchezo huo mashuleni ili kuweza kuibua vipaji vya mchezo huo kuanzia
ngazi ya shule.
Kwa upande wake katibu mkuu wa chama hicho Kale
Mwigonja alisema kuwa shindano hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Safari
Lager linalenga kunua mchezo huoikiwa I pamoja na kujiandaa na Afrika Mashariki
linalotarajia kufanyika mwezi juni mwaka huu Mkoani Dodoma.
Alisema kuwa mashindano hayo yanashirikisha virabu
32 kutoka katika mikoa mbali mbali nchni ambapo alisema kuwa washindi watapata
zawadi mbalimbali ikiwemo ikombe pamoja na zawadi za pesa taslimu ambapo alisema
kuwa mshindi wa kwanza atapata sh.laki 6 na kikombe ,wa pili laki 4 na kikombe
na watatu laki 3.
0 comments:
Post a Comment