Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCm wilaya ya Morogoro mjini Fikiri Juma akiongea wakati wa kikao cha kawaida cha baraza la madiwani manispaa ya Morogoro.
Mwenyekiti huyo akisisitiza jambo kwenye kikao hicho
Wajumbe wa baraza la madiwani katika manispaa ya Morogoro wakiwa katika kikao cha kawaida cha baraza hilo juzi
Diwani wa kata ya Tungi Deogratias Mzeru akiwa na diwani mwenzake wa jirani Maria Kiamani nje ya ukumbi wa manispaa mara baada ya kumalizika kikao hicho.
Diwani wa kata ya Kilakala Ribon Mkali akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wake wa CCM wa matawi katika kata hiyo.
Habari zaidi Soma hapa Chini.
Meya wa manispaa ya Morogoro Amini Nondo ameagiza watendaji katika manispaa hiyo kuweka mipaka katika eneo la kata ya Kauzeni linalopakana na eneo la kambi ya jeshi ya Mzinga ili kuondokana na migogoro ya ardhi iliopo sasa.
Alilazimika kusema hayo baada ya mwenyekiti wa CCM Fikiri Juma kutaka mgogoro huo kushughulikiwa haraka ili kuepusha madhara kwa jamii hizo mbili.
Alisema kuna kisa sababu kwa watendaji hao kuhakiki mipaka katika eneo hilo ili kuweza kuweka mipaka hiyo.
Hata hivyo aliagiza wananchi katika manispaa hiyo kufuga mifugo kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo badala ya kufuga mifugo mingi.
Awalia mwenyekiti huyo wa CCM alisema hakuna sababu kwa jeshi hilo na raia kuwa na ugomvi kwani ni jamii inayohitaji kuishi kwa pamoja na kwa kushirikiana.
'' wananchi hawapaswi kuwa na ugomvi na jeshi letu, na jeshi halipaswi kuwa na ugomvi na wananchi hivyo niwaombe halmashauri mshughulikie tatizo hilo ambalo linalalamikiwa kwa muda mrefu sasa.
Mwenyekiti huyo alisema malalamiko kwa wananchi hao dhidi ya jeshi la mzinga ni wanadai kuwa wanajeshi hao wamekuwa na mifugo kupita kiasi hivyo hulazimika kuingiza ng'ombe zao kwwnye mashamba ya wananchi hali inayosababisha migogoro hiyo.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Ahmed Mazola alisema kuwa wananchi ndio walianza kuwa wakwanza kuishi katika eneo hilo ambapo badae ndipo lilikuja jeshi hilo.
Alisema kila kukicha wanajeshi hao wamekuwa wakichukua sheria mkononi kwa kuweka bicon bila ya utaratibu na hivyo kuvamia eneo la wananchi hao.
0 comments:
Post a Comment