CHAMA cha
Mapinduzi CCM mkoa wa Morogoro kimesema kitawachukulia hatua za kisheria kwa kuwafikisha mahakamani wapangaji wake wote ambao
wanamadeni sugu sambamba na kupitia upya
mikataba kuona kama iko sahihi.
Katibu wa
CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli alisema hayo jana wakati akiongea na Uhuru
ofisini kwake ambapo alisema kazi hiyo
ni utekelezaji wa maagizo ya baraza la wadhamini.
‘’ Tumeanza
kufutilia wapangaji wetu wote wenye madeni sugu ili waweze kulipa , vinginevyo
watakaokaidi tutawachukulia hatua za kisheria’’ Alisema
Romuli
alisema hatua za kisheria watakazochukua ni pamoja na kuwafungia biashara zao na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Alisema pia
wanafanya mapitio ya kodi za wapangaji wao kuona kama zinalingana na mazingira
na wakati sahihi kwa lengo la kuhakikisha miradi hiyo inakuwa na tija kwa
chama.
Aidha
alisema wakati huo huo wanapitia
mikataba ya wapangaji wao kuona kama iko sahihi na kwamba wale wote ambao
hawana mikataba kuwataka kujaza mikataba ili kuweza kufanya kazi nao.
‘’ Wapo
baadhi ya wapangaji wetu ambao hadi sasa hawana mikataba, kwa sasa ni lazima
kila mpangaji akawa na mkataba’’ Alisema
Hata hivyo
alisema lengo la kufanya hivyo ni pamoja
na kuhakikisha wanaiboresha miradi hiyo ili iweze kukidhi mahitaji ya sasa
kulingana na eneo husika.
Alisema
Kwa sasa walianza kufanya ukarabati katika jengo la ofisi ya CCM mkoa
na kwamba kila ilipo miradi yao itaboreshwa ili ilingane na mazingira
halisi .
0 comments:
Post a Comment