Pages

Subscribe:

Tuesday 27 May 2014

MANISPAA MORO LAWAMANI KWA KUGEUZA UWANJA WA JAMHURI KUWA SEHEMU YA DAMPOO LAKE.

 Richard Haule mwanakikundi cha kuzoa takataka katika manispaa ya Morogoro akisukuma mkokoteni wake kuelekea katika eneo la uwanja wa Jamuhuri ambao kwa sasa limegeuzwa kama dampoo la kutupia takataka.

 Richard Haule akiwa na mwenzake ambaye badae alitoweka wakisukuma mkokoteni huo.

 Hilo ni eneo la nyuma la uwanja wa jamuhuri linalopaka na uwanja wa golf likiwa limegeuzwa dampoo.

Baadhi ya wanafunzi waliokutwa wanasoma katika eneo hilo la uwanja wa Jamuhuri jirani kabisa na dampoo hilo huku harufu mbaya na moshi vikitanda katika eneo hilo.


Habari zaidi Soma hapo chini.

CHAMA cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Morogoro kimeitaka halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuacha kugeuza eneo la uwanja wa Jamuhuri kama sehemu ya Dampoo la kutupia takataka.
 
Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli alisema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu ya hali halisi ya uwanja huo unaomiliki na CCM.
 
Alisema Halmashauri hiyo kupitia vikundi vyake vya uzoaji wa taka vimekuwa vikitupa takataka wanazozoa katika mitaa mbalimbali ya  Kata ya Boma na kuzitupa hapo hali inayohatarisha maisha ya watu sambamba na kuharibu mandarin ya uwanja huo.
 
‘’ Tumeshawapa taarifa ili wazoe takataka zote walizomwaga katika eneo la uwanja huo tunasubiri utekelezaji, hii ni mara ya pili sasa awali walishawahi kufanya hivyo wakazoa naona sasa wanarudia tena’’ Alisema.
 
Alisema uwanja huo ambao unategemewa kwa shughuli mbalimbali za mkoa na kitaifa unatakiwa kuwekwa katika mazingira safi na salama na sio kugeuzwa kama dampoo.
 
 Hata hivyo katibu huyo alisema wanatarajia kuboresha mazingira  yote yanayozunguka uwanja huo kwa kukata miti iliozidi ovyo .
 
Alisema sambamba na hilo pia wanatarajia kufanya ukarabati katika jingo hilo maeneo ya nje ya uwanja kwa kupiga plasta na kupaka rangi ili uweze kuvutia zaidi.
 
‘’ Tunataka uwanja wa Jamuhuri uwe kivutio cha watu kuja kupumzika na kuvuta hewa safi, tunataka kupanda miti ya maua na matunda na kuweka bustani nzuri za maua’’ Alisema.
 
Hata hivyo katibu huyo alisema wanamshukuru mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Morogoro Paskari Kihanga kwa kuwasaidia kupata kisima katika uwanja huo ambacho kitasaidia kuwa na maji ya uhakika.
 
Mmoja wa wanakikundi wanaozoa takataka katika kata ya Boma alidai kuwa yeye alipewa maelekezo ya kumwaga takataka hapo na bosi wake aliyemtaja kwa jina moja la Mama  Sanga.
 
Richard alisema  kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakimwaga takataka hapo na badae kulipia manispaa kwaajili ya kuzizoa na kwamba anaona ni utaratibu sahihi. 
 
'' Kwanza mimi nasngaa sijui nani kaamua kuzichoma hizi takataka hapa, maana baada ya kujaa huwa tunalipia manispaa alafu wanakuja kuzichoma'' alisema.
 
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika eneo jirani na dampoo hiyo walidai wanapata adha kubwa kutokana na harufu mbaya na kwamba wanaomba serikali kuchukua hatua ili kuepuka magonjwa ya milipuko yanayoweza kuwapata.
 
'' wanazidi kuzijaza mwisho zitafika hadi eneo la hosteli yetu pale, maisha yetu yapo hatarini alisema mmoja wa wanafunzi ambaye hakutaka jina lake litajwe.


0 comments:

Post a Comment