WAZIRI wa Nchi ofisi ya makamo wa Rais (Mazingira) Binilith
Malenge alipotembelea kiwanda cha Twenty Firts Centuary kuangalia matumizi ya makaa ya mawe badala ya magogo ya miti waliokuwa wakitumia zamani na kupigwa marufuku na serikali.
Waziri huyo akiangali maeneo mbalimbali ya mabwa ya maji katika kiwanda hicho.
Waziri huyo akiangali maji yanayotoka kiwandani humo ambayo yanakemikali yanaingia katika mto Ruvu ambayo yanamadhara kwa binadamu.
WAZIRI wa Nchi ofisi ya makamo wa Rais (Mazingira) Binilith
Malenge amekiagiza kiwanda cha Twenty first centuary kuhakikisha ifikapo mwezi
Agosti mwaka huu wawe wamebadilisha mfumo wa maboiler ya kutumia nishati ya
magogo ya miti na kuingia katika mfumo wa makaa yam awe.
Alisema hayo jana wakati alipotembela kiwandani hapo
kuangalia jinsi ya uendeshaji wa kiwanda na kujionea mfumo mzima wa uhifadhi wa
mazingira kiwandani hapo.
Alisema kuwa pamoja na juhudi walizofanya kiwanda hicho
kuacha kutumia magogo ya miti ambayo yalikuwa yakiharibu mazingira na kuingia
katika mfumo wa makaa ya mawe lakini bado mfumo wa vifaa vya kuchemshia maji upo katika mfumo wa
kutumia magogo.
Alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha kuwepo kwa vumbi
linalosambaa hewani na hivyo kusababisha kero kwa wananchi wa maeneo jirani na
hapo.
‘’ sasa ni lazima ikifika mwezo wa nane mbadilishe maboiler
yenu yawe katika mfumo wa makaa yam awe ili kuondokana na usumbufu’’ Alisema
Waziri huyo.
Hata hivyo waziri huyo alishauri faini zinazotozwa na NEMC
zingetumika kuboresha mabwawa ya maji yanayotumiwa na viwanda vya nguo na ngozi
vya mjini hapa ili kuweka mazingira safi.
‘’ Mimi naona hizi faini mnazotoza mngezipeleka kuhakikisha
mnaboresha mabwawa hayo ili kuondokana na adha ya maji kujaa na kufurika nje ya mabwawa na kusababisha
adha kwa wananachi wa karibu na hata
kuingia mtoni na badae kuleta madhara kwa watumiaji wa mto huo ‘’ Alisema
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Morogoro Said Amanzi
alipongeza juhudi zilizofanywa na vyombo vya habari mkoani hapa za kuhakikisha
wanaripoti btaarifa juu ya matumizi ya magogo ya miti kwa kiwanda hicho hadi
kufikia sasa matumizi hayo yamechwa.
‘’ Kweli serikali kwa kushirikiana na Vyombo vya habari kuhakikisha zoezi la matumizi ya magogo limesitishwa sasa’’ alisema Amanzi.
0 comments:
Post a Comment