HALMASHAURI
ya manispaa ya Morogoro imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 50 kwa wafanyabaishara walikokuwa wakiendesha
biashara zao bila leseni.
Afisa habari
wa manispaa hiyo Liliani Henerico
alisema hayo jana wakati akitoa taarifa ya oparesheni ilioendeshwa na
mansiapaa hiyo katika nyumba za kulala
wageni na maduka mjini hapa.
Alisema
oparesheni hiyo ilifanywa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Aprili mwaka
huu na kwamba jumla ya biashara 54 zilifugiwa kutokana na kushindwa kulipa
faini hizo.
Alisema
katika zoezi hilo faini za leseni zilikuwa ni shilingi 4,540,000 ambapo mapato ya ada za leseni yalikuwa ni 45,786859
n hivyo kufanya jumla ya makusanyo hayo kuwa ni shilingi milioni 50,326,859.
Aidha afisa habari huyo alisema zoezi hilo
linaendelea kuhakikisha wafanyabiashara wote wanafata taratibu na kuepuka
kukwepa kodi.
Kwa upande
mwingine afisa habari huyo alisema manispaa hiyo ilianza zoezi la kukagua
nyumba katika manipaa hiyo kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama.
Alisema utekelezaji
wa zoezi hilo la usafi wa mazingira hadi sehemu za makazi ya wananchi ni agizo
la mkuu wa mkoa la kutaka halmashauri zote kuhakikisha zinakuwa safi ili mkoa
wa Morogoro uweze kupata tunzo ya usafi kitaifa.
Sambamba na
hilo alisema agizo hilo pia ni kutaka kujenga mazingira ya kuepuka maradhi ya
mlipoko kwa wakazi wa mkoa wa Morogoro.
0 comments:
Post a Comment