Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi taifa Abdalla Bulembo akizindua Website ya jumuiya hiyo Mkoa wa Morogoro.
Hiyo ndio muonekano wa website hiyo baada ya kuzindulika jana.
Bulembo akisalimiana na wajumbe wa baraza la wazazi mkoa wa Morogoro mara baada ya kuwasili katika hotel ya Nashera jana ambapo baraza hilo lilifanyika.
Viongozi wa jumuiya ya wazazi wakiwa katika picha ya pamoja eneo la Tungi wakisubiri kumpokea mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya hiyo.
Habari zaidi soma hapa.
MWEMYEKITI
wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Abdallah Bulembo amewaonya viongozi wa jumuiya hiyo kuacha tabia ya kujihusisha na utengenezaji wa
makundi ya Urais,Wabunge na madiwani ndani ya chama hicho muda wa kampeni haujafika.
Alisema kwani kufanya hivyo kunasababisha kuwepo na
mpasuko na hivyo kushindwa kutekelezaji ilani ya chama hicho.
Bulembo alitoa onyo hilo jana wakati akifungua mkutano mkuu wa
baraza la wazazi Mkoani hapa ambapo alisema kuwa chama hicho hakina makundi na
kwamba kundi lao ni moja ambalo kiongozi wake Rais Jakaya Kikwete.
Bulembo
alisema chama hicho kina utaratibu wa kuwapata viongozi wake kwa vikao na
kwamba kiongozi anayetakiwa kuungwa mkono ni Yule atakayechaguliwa na CCM muda
na wakati ukifika.
‘’
Mwanachama au kiongozi yeyote atakayebainika kufanya hivyo hatutasita
kumchukulia hatua’’ Alisema.
Hivyo
aliwataka viongozi hao kutekeleza majukumu yao ya kuboresha jumuiya ya wazazi
kuanzia ngazi ya chini ikiwa ni pamoja na kuwajibika katika kufanya kazi na
kuacha kuwakatisha tamaa viongozi ambao bado wako madarakani.
Akizungumzia
suala la katiba mwenyekiti huyo alisema kuwa msimamo wa chama chake ni kuwa na
serikali mbili ambazo zilikuwepo kwa miaka 50 na kwamba zimedumu ndani ya
muungano.
Hata hivyo
alisema kuwa suala la muugano ni la watanzania wote hivyo ni wajibu wa kila
mtanzania kuudumisha ikiwa ni pamoja na kufanya marekebisho ya changamoto
zilizopo ambapo alisema kuwa ndani ya miaka 50 kumekuwepo na marekebisho mengi
ambayo yamefsnyika.
Hivyo
aliwataka watanzania kuendelea kuutetea na kuulinda muungano huo mpaka mwisho.
Kwa upande
wake katibu wa wazazi Mkoa wa Morogoro Shaweji Mkumbula alisema kuwa jumuiya
hiyo inakabiliwa na changamoto ambazo jumuia hiyo inaendelea kuzifanyia kazi .
Alizitaja
changamoto hizo kuwa ni kutofanyika kwa vikao katika ngazi ya chini kwa mujibu
wa kanuni ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi kama kadi kanuni DCR
pamoja na usafiri kwenye baadhi ya maeneo ya Wilaya.
Nyingine ni
Viongozi ngazi ya kata na matawi kushindwa kuhamasisha wanachama kulipa ada zao
kwa kuzingatia maelekezo ya kanuni.
Ufunguzi
wa mkutano huo ulienda sambamba na uzinduzi wa tovuti ya jumuiya hiyo pamoja na
ugawaji zawadi kwa Wilaya zilikamilisha ujenzi wa Ofisi ya wazazi ambapo Wilaya
ya Morogoro iliibuka mshindi na hivyo kujishindia kombe pamoja na
zawadi ya sh.laki 3
0 comments:
Post a Comment