Pages

Subscribe:

Monday 28 April 2014

UTUMISHI YANYAKUA KOMBE NA KUTOA MFUNGAJI BORA MPIRA WA PETE MEI MOSI 2014

SAM_0156Mabingwa wapya wa Mei Mosi 2014,  Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakiwa katika mazoezi mepesi kabla ya mchezo ambao waliifunga Uchukuzi na kunyaukua kombe la Mei Mosi 2014 iliyochezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
SAM_0192Mchezaji wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Sophia Komba akijiandaa kumdhibiti mchezaji wa Uchukuzi (C) (mwenye mpira) katika mechi ya fainali iliyochezwa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. 

Sunday 27 April 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00207GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.959 BMM AINA YA TOYOTA L/CRUISER 110 LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA FARAHAD ABDUL (26) MWARABU – MSIMAMIZI WA KAMPUNI YA KUCHENGUA DHAHABU YA PIRBAKISH MKAZI WA CHUNYA LILIPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA SEIF MOHAMED (27) MKAZI WA NZEGA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 27.04.2014 MAJIRA YA SAA 22:45 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAKONGOLOSI, KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, BARABARA YA MAKONGOLOSI/MKWAJUNI, WILAYA YA CHUNYA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WAWILI WALIJERUHIWA 1. FARAHAD ABDUL (26) DEREVA WA GARI HILO AMBAYE AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA RAYMOND SIKAONA (29) MFANYAKAZI KATIKA HALMASHAURI YA MJI MDOGO WA MAKONGOLOSI AMBAYE ALIKUWA ABIRIA NA AMELAZWA HOSPITALI YA  MWAMBANI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA JAPO KUWA AMELAZWA.

VETA YAENDESHA SEMINA KWA WABUNGE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII JUU YA MRADI WA KUONGEZA SIFA ZA KUAJILIWA – EEVT LEO JIJINI DAR


Mh Jenista Mhagama (Kushoto) akiongea na baadhi ya wabunge kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na baadhi ya wafanyakazi wa VETA kutoka Makao Makuu na VETA Kanda ya Kusini wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA   Kwaajili ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii juu ya mradi wa Kuongeza sifa za kuajiliwa – EEVT iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki wa Kuu ya Tanzania, Jijini Dar Es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Magreth Sitta na Kulia ni Steven Ngonyani.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mh Magreth Sitta (Katikati) akiongea wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA kwaajili ya Kamati hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania leo Jijini Dar Es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa VETA Tanzania, Mh Mhandisi Zebadiah Moshi(kulia) akifungua semina iliyoandaliwa na VETA kwaajili ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Kijamii loe katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Mh Mhandisi Zebadiah Moshi akiongea wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA kwaajili ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii leo
Mkurugenzi wa Soko la Ajira, Mipango na Maendeleo Kutoka VETA, Bw Enock Kibendela akitoa mada juu ya mchango mkubwa unaotolewa na VETA Katika kukuza sekta ya ajira kwa vijana wanaopata mafunzo ya ufundi stadi wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA kwa wabunge wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii leo katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
Baadhi ya wabunge wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii pamoja na wafanyakazi wa VETA waliohudhuria semina iliyoandaliwa na VETA Kwaajili ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii juu ya mradi wa Kuongeza sifa za kuajiliwa – EEVT.

Friday 25 April 2014

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YATAKA GAZETI LA TANZANIA DAIMA LIKANUSHE HABARI WALIOTOA YA UONGO KUHUSU WAHUDUMU WA WIZARA HIYO WAWE NA DIGRII YA UDHAMILI

           Msemaji wa wizara ya nishati na madini Badra Masoud aliyevaa shati la drafti akinukuu masuala muhimu katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo uliofanyika mjini Morogoro kwa siku mbili Aprili 23 na 24 mwaka huu.

Habari zaidi soma hapa chini.



WIZARA ya Nishati na madini imekanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la Tanaznia Daima la Aprili 24 mwaka huu kwamba waziri wa wizara hiyo Profesa Sospetter Muhongo amesema ni lazima watumishi wote  wakiwemo wahudumu wa wizara hiyo kuwa na kiwango cha elimu ya digrii ua udhamili jambo ambalo si sahihi.

Msemaji wa wizara hiyo Badra Masud alisema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari mjini hapa baada ya kumalizika kwa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo.

Alisema mwandishi wa habari wa gezeti hilo aliandika taarifa hizo kwa mtazamo wake na sio kwa kufuta yale yaliongelewa na waziri huyo wakati wa kufungua baraza la wafanyakazi Aprili 23 mwaka huu.

Msemaji huyo wa wizara alisema kilichongelewa na waziri ni kuwataka maafisa wa wizara hiyo kutumia fulsa za kusoma na angalao wawe na kiwango cha elimu cha digrii ya udhamili na sio kwa watumihi wote  wakiwemo wahudumu kama ilivyoandika gazeti hilo la Tanzania Daima.

Alitaka gazeti hilo kukanusha taarifa hizo kabla ya kuchukua hatua za kisheria  kutokana na kupotosha habari hiyo.

‘’ Mwandishi wa gazeti hilo alikuwa na ajenda yake na ndio maana aliandika kwa kuongeza chumvi, ni lazima waandishi wakawa makini vinginevyo wanwaweza kusababisha vyombo vyao kuingia katika matatiz  na hata  kusababisha mtafaruko na chuki katika ya jamii’’ Alisema

Wanapoandika taarifa mbalimbali wawe makini na kama hawajaelewe ni vema wakauliza na kuongeza kuwa kazi ya uandishi wa habari ni kuhabarisha na kutoa taarifa sahihi kwa jamii na sio kupotoshwa.

Badra alisema siku ya ufunguzi huo yeye mwenyewe alikuwepo na kilichoongelewa sio hicho kilichoandikwa katika gazeti hilo na kuongeza kuwa  alitoa fulsa kwa waandishi hao kuuliza masawali  na badala yake alisimama mwenyeki  wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro Ida Mushi  na kusema wameelewa na kwamba hawana maswalilabdla kwa wakati mwingine.





Wednesday 23 April 2014

UJUMBE KUTOKA NCHI WANACHAMA WA SADC UNAOSHUGHULIKA NA MAFUNZO YA UANGALIZI WA AMANI KIMATAIFA WATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA MAGEREZA LEO, JIJINI DAR ES SALAAM

imageKamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(Meza Kuu) akifanya mazungumzo rasmi na Ujumbe Maalum toka Nchi Wanachama wa SADC unaoshughulika na Mafunzo ya Uangalizi wa Amani Kimataifa walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza. Jeshi la Magereza Nchini limeteuliwa na Kituo cha Mafunzo ya Uangalizi wa Amani – SADC kuwa mwenyeji wa Mafunzo ya Uangalizi wa Amani wa Kimataifa yatakayofanyika hivi karibuni Nchini Tanzania.image_1Makamishna wa Jeshi la Magereza Nchini wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati Ujumbe toka Nchi Wanachama wa SADC unaosimamia Mafunzo ya Uangalizi wa Amani Kimataifa ulipotembea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni Kamishna Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(katikati) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga.

VIJANA WATAKIWA KUJITOKEZA MBIO ZA WAZALENDO

Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Sixtus Mapunda akiwa na Omar Said Ng'wanang'waka Mkuu wa Utawala UVCCMKatibu Mkuu wa UVCCM Taifa Sixtus Mapunda akiwzungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kushoto ni Omar Said Ng’wanang’waka Mkuu wa Utawala UVCCM
Frank Mvungi-Maelezo
VIJANA wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mbio za wazalendo zitakazofanyika Ijumaa wiki hii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya  miaka 50 ya muungano  wa Tanganyika na Zanzibar.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  (UVCCM) Sixtus Mapunda wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Mapunda alisema mbio hizo zitaanzia Ofisi ya CCM Vijana, Kinondoni hadi ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere uliopo Posta jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa lengo la mbio hizo ni kuwahamasisha vijana kuweka mbele uzalendo na maslahi mapana ya Taifa hasa katika kipindi hiki cha Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI ACHARUKA APIGA MARUFUKU WATENDAJI WAKE KUSAINI MIKATABA NJE YA NCHI NA NJE YA OFISI ZA WIRAZA.

 Waziri wa Nishati na Madini Prof Sosipeter Muhongo akizungumza kwa hisia kali kwenye mkutano wa siku mbili wa wajumbe wa baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo unaoendelea kwa sasa kwenye Hotel ya Nashera Mkoani hapa


           Wajumbe wa mkutano huo

 Baada ya kufungua nmkutano huo Waziri Muhongo alipiga picha ya pamoja na wajumbe hao.
 Vile vile Waziri Muhongo alipiga picha na waandishi wa habari,niongoni mwa waadishi hao ni Mwandishi wa Mtandao huu[wanne kushoto mwenye kamera shingoni]
 Waziri huyo akiondoka baada ya kufungua mkutano huo.
                         Na Dustan Shekidele,Morogoro.
WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amewataka watendaji wa Wizara hiyo kuacha mara moja tabia ya kusaini mikataba inayohusu Wiraza hiyo nje ya Nchini ama nje ya ofisi za watendaji hao na kwamba mtendaji yoyote atakaye kaidi agizo hilo atimtimu kazi.

Prof Muhongo alitoa karipio hilo leo asubuhi alipofungua mkutano wa siku mbili wa baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Kitalii ya Nashera iliyopo barabara ya Boma mkoani hapa.

" Niudhaifu mkubwa kwa mtendaji wa Wizara kwenda kusaini mikataba ya Wizara nje ya Nchini au nje ya ofisini ya tendaji, kuanzia sasa ni marufuku mtendaji wa wizara yangu kufanya hivyo na atakaye kaidi nitamuondoka kazini mara moja"alisema Waziri huyo kwa hisia kali.

Vile vile Prof Muhongo amewataka wajumbe wa mkutano huo kujadini namna ya kuinua upya shilika la Tanesco,Madini na Ges.

 "Wizara yetu ni nyeti katika uchumi wa taifa letu ambapo  asilimi 75 ya uchumi wa taifa letu inategemea Wizara yetu kwamba kama umeme si wa uhakika viwanda na shughuri nyingine zitasimama pia tukishindwa kuzalisha gesim kwa wingi na kuchimba madini pato la taifa litashuka''alisema Waziri huyo ambaye sehemu kubwa ya hotuba yake aliwapiga vijembe watendaji wa wizara hiyo.

Monday 21 April 2014

DC MVOMERO ASEMA WANAOWATUKANA WAASISI WA CHINI WAMEVURUGIKIWA

 Mkuu wa wilaya ya Mvomero Antoni Mtaka akiongea na umoja wa  wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu wenye imani ya Kipentekoste wakati wa mahafari ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari na vyuo ( TAYOMI)iliofanyika melela wilayani Mvomero.


 Mkuu huyo wa Wilaya akimtunuku cheti mwanafunzi wa chuo kikuu cha mzumbe Caroline Ndosi katika mahafari hayo ya kidini.


 Wanafunzi hao wakisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mtaka.

Wanafunzi hao wakiwa katika picha ya pamoja na DC huyo
Habari zaidi
soma hapa chini

MKUU wa wilaya ya Mvomero Antoni Mtaka amewatahadharisha vijana  wasomi kutoruhusu kukanyaga historia ya waasisi wa Nchi  kwani waliweza kufanya mambo makubwa na wanatakiwa kuenziwa.

Alisema hayo jana wakati akiongea  katika kongamano  la umoja wa wanafunzi walioko shuel za msingi, sekondari na vyuo vya kati  na vyuo vikuu walio na msingi wa imani ya Kipentekoste  (TAYOMI) iliofanyika  Milela wilayani Mvomero.

Alisema wapo baadhi ya watu ambao wamefilisika kimawazo na fikra wanatumia muda wao mwingi kujadili na kutukana mambo waliofanya waasisi hao badala ya kujadili masuala ya katiba yaliopo sasa.

‘’ Unakuta wapo watu wanadiliriki kumtukana Nyerere bila kujali kuwa ndiye aliyetuletea uhuru wan chi hii, nchi nyingi za  Afrika zimekuwa zikimuenzi Nyerere  kwa kutambua mchango wake katika kupatikana kwa uhuru wan chi zao’’ Alisema

Alisema kama nchi  hizo zinatambua umuhimu wake na kumuenzi inashangaza na watangaaa kuona watanzania hawathamini mchango wake na badala yake wanamtukana.
Alisema Nyerere na waasisi wengi wan chi hii walifanya mambo makubwa sana nay a kihistoria hivyo kwa vijana wanayo kila sababu ya kuyaenzi kwa heshima zote na kuwapuuza watu hao wanaobeza mchango wao viongozi hao.
Mkuu huyo wa wilaya aliwataka vija hao wasomi kutumia muda mwingi kufutilia suala zima la mchakato wa katiba na kupembua vipengele muhimu ili ikifika wakati wa kupiga kura iwe rahisi kwao .
‘’ Watu wengi wamejipatia umaarufu kupitia katiba mpya wakidhani katiba ile inaishia bungeni tuu, kumbe katiba ile mchakato wake itarudi tena kwa wananchi na kupigiwa kura’’ Alisema
Kwa upande wake Philipo Abiud Mratibu wa TAYOMI wa mkoa wa Morogoro alisema wamekuwa na utaratibu wa kufanya makongamano kama hayo wakati wa sherehe za Pasaka kwa kuwakusanya  wanafunzi hao na kuwafundisha masuala mbalimbali ya maadili.
Alisema suala kubwa wanalosisitiza ni kujiepusha na madawa ya kulevya kwa vijana hao sambamba na tabia zote zinazopelekea kutumbukia katika vitendo viovu na kuongeza kuwa wanawafundisha kufanya juhudi na maarifa wakiwa shuleni ni waweze kufanikiwa katika maisha yao.

 


Friday 18 April 2014

TUJIKUMBUSHE, UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

 Ilikuwa siku ya uhuru wa vyombo vya habari  2013 waandishi wa habari mkoa wa Morogoro walipoungana na waandishi wengine nchi nzima kupinga vikali watu wanaozuia  waandishi kufanya kazi zao kwa uhuru, na hapo walilengwa zaidi polisi kufutia  tukio la mauji ya Mwangozi kule Iringa wakati akiwa kazini.

Nicksoni Mkilanya akiwa na bango lake lenye ujumbe huo kwa polisi.


Nimeamua kukumbusha hayo kwa makusudi kutokana na baadhi ya watu hususani viongozi ambao sio wazalendo bado wamekuwa  na urasimu wa kutoa habari kwa madai kuwa wao sio wasemaji.

Mimi naamini kuwa kila mtu ni mtoa habari kwa nafasi yake, urasimu ambao umekuwa ukifanya na baadi ya viongozi ni kutaka kuficha maovu na kukumbatia maovu kwa faida yao.

Hii leo nimeamua kusema hayo ni baada ya kuongea na kiongozi mmoja wa CCM wilaya ya Mvomero ambaye ni mtendaji mkubwa kutaka kujua juu ya mgogoro uliopo baina ya balaza la madiwani na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya hiyo lakini majibu ambayo amenipa hajaridhishi kwa kiongozi kama yule na kwa chama kinachotawala. 
Tulitegemea majibu kama hayo watoe watu ambao labda wamekata tamaa na uongozi au vinginevyo.
labda tukumbushane tu kuwa kwa mwandishi wa habari akiwa kazini, kila utakachomjibu ni habari kwake na kwamba ukizingatia amekupa nafasi ya wewe kutoa amaoni kwa uapande wako.