Pages

Subscribe:

Friday, 18 April 2014

TUJIKUMBUSHE, UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

 Ilikuwa siku ya uhuru wa vyombo vya habari  2013 waandishi wa habari mkoa wa Morogoro walipoungana na waandishi wengine nchi nzima kupinga vikali watu wanaozuia  waandishi kufanya kazi zao kwa uhuru, na hapo walilengwa zaidi polisi kufutia  tukio la mauji ya Mwangozi kule Iringa wakati akiwa kazini.

Nicksoni Mkilanya akiwa na bango lake lenye ujumbe huo kwa polisi.


Nimeamua kukumbusha hayo kwa makusudi kutokana na baadhi ya watu hususani viongozi ambao sio wazalendo bado wamekuwa  na urasimu wa kutoa habari kwa madai kuwa wao sio wasemaji.

Mimi naamini kuwa kila mtu ni mtoa habari kwa nafasi yake, urasimu ambao umekuwa ukifanya na baadi ya viongozi ni kutaka kuficha maovu na kukumbatia maovu kwa faida yao.

Hii leo nimeamua kusema hayo ni baada ya kuongea na kiongozi mmoja wa CCM wilaya ya Mvomero ambaye ni mtendaji mkubwa kutaka kujua juu ya mgogoro uliopo baina ya balaza la madiwani na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya hiyo lakini majibu ambayo amenipa hajaridhishi kwa kiongozi kama yule na kwa chama kinachotawala. 
Tulitegemea majibu kama hayo watoe watu ambao labda wamekata tamaa na uongozi au vinginevyo.
labda tukumbushane tu kuwa kwa mwandishi wa habari akiwa kazini, kila utakachomjibu ni habari kwake na kwamba ukizingatia amekupa nafasi ya wewe kutoa amaoni kwa uapande wako.


0 comments:

Post a Comment