MWENYEKITI wa Halmashauri ya wilaya ya Mvomero Jonas Zee Land
amelalamikia kutishiwa na baadhi ya
wanasiasa katika wilaya hiyo kuwa watambambikizia kesi kufutia mgogoro
uliokuwepo baina ya madiwani wa wilaya hiyo na mwenyekiti wa umoja wa vijana
UVCCM Paskari Boga wilaya hiyo.
Alisema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari juu
ya vitisho anavyopata kupitia ujumbe uonaotumwa katika mitandoa ya simu za
mkononi.
‘’ Nimetumiwa ujumbe ,’’Suala la madiwani na mwenyekiti wa
UVCCM unachochewa na Jonas na nimemwagiza Lule ahakikishe Jonas na wapambe wake wote tunawavuruga
na kuwabambizia kesi mambo mengi
nitawapa napita hapo jumapili tukutane’’ alisema
Alisema kuwa kwa muda sasa wilaya hiyo imegubikwa na mgogoro
baina ya mwenyekiti huyo na madiwani baada ya mwenyekiti huyo kuwaita madiwani
hao mizigo.
Alisema ameamua kuweka wazi vitisho hivyo ili jamii na
vyombo vya usalama vijue na kongeza kuwa tayari alishatoa taarifa polisi dhidi
ya vitisho hivyo.
Alisema mgogoro uliokuwepo baina ya mwenyekuti huyo wa UVCCM
na balaza la madiwani ni kwamba aliwaita madiwani wa wilaya hiyo kuwa ni
mizigo, viwete na kuwataka vijana kutowachagua kutokana na kushindwa kusimamia
asilimia 10 ya mapato ya halmashauri
inayotakiwa kupewa mikopo kwa vijana na wanawake.
Jonas alisema baada ya matamshi hayo walikaa balaza la
madiwani na kutoa maazimio wapeleke
taarifa hizo kwenye chama ili hatua za kinidhamu zichukuliwe ikiwa ni pamoja na
kumtaka akanushe ndani ya siku 14 kama atashindwa kuthibitisha juu ya usemi
wake.
Kwa upande wake katibu wa chama wilaya ya Mvomero Sadani
Kimath alikiri kupokea barua ya mwenyekiti huyo
pamoja na ujumbe huo wa simu uliotumwa kwa mwenyekiti huyo.
Alisema hawezi kuzungumza lolote juu ya suala hilo kwa kuwa
utaratibu wa chama hoja zote zinapelekwa
kujadiliwa katika vikao na kwamba kesho ndio wanakaa kikao na watatoa maamuzi
juu ya taarifa hizo.
0 comments:
Post a Comment