Msemaji wa wizara ya nishati na madini Badra Masoud aliyevaa shati la drafti akinukuu masuala muhimu katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo uliofanyika mjini Morogoro kwa siku mbili Aprili 23 na 24 mwaka huu.
Habari zaidi soma hapa chini.
WIZARA ya Nishati na madini imekanusha taarifa zilizoandikwa
na gazeti la Tanaznia Daima la Aprili 24 mwaka huu kwamba waziri wa wizara hiyo
Profesa Sospetter Muhongo amesema ni lazima watumishi wote wakiwemo wahudumu wa wizara hiyo kuwa na
kiwango cha elimu ya digrii ua udhamili jambo ambalo si sahihi.
Msemaji wa wizara hiyo Badra Masud alisema hayo jana wakati
akiongea na waandishi wa habari mjini hapa baada ya kumalizika kwa baraza la
wafanyakazi wa wizara hiyo.
Alisema mwandishi wa habari wa gezeti hilo aliandika taarifa
hizo kwa mtazamo wake na sio kwa kufuta yale yaliongelewa na waziri huyo wakati
wa kufungua baraza la wafanyakazi Aprili 23 mwaka huu.
Msemaji huyo wa wizara alisema kilichongelewa na waziri ni
kuwataka maafisa wa wizara hiyo kutumia fulsa za kusoma na angalao wawe na
kiwango cha elimu cha digrii ya udhamili na sio kwa watumihi wote wakiwemo wahudumu kama ilivyoandika gazeti
hilo la Tanzania Daima.
Alitaka gazeti hilo kukanusha taarifa hizo kabla ya kuchukua
hatua za kisheria kutokana na kupotosha
habari hiyo.
‘’ Mwandishi wa gazeti hilo alikuwa na ajenda yake na ndio
maana aliandika kwa kuongeza chumvi, ni lazima waandishi wakawa makini
vinginevyo wanwaweza kusababisha vyombo vyao kuingia katika matatiz na hata kusababisha mtafaruko na chuki katika ya jamii’’
Alisema
Wanapoandika taarifa mbalimbali wawe makini na kama
hawajaelewe ni vema wakauliza na kuongeza kuwa kazi ya uandishi wa habari ni
kuhabarisha na kutoa taarifa sahihi kwa jamii na sio kupotoshwa.
Badra alisema siku ya ufunguzi huo yeye mwenyewe alikuwepo
na kilichoongelewa sio hicho kilichoandikwa katika gazeti hilo na kuongeza kuwa
alitoa fulsa kwa waandishi hao kuuliza
masawali na badala yake alisimama
mwenyeki wa chama cha waandishi wa
habari mkoa wa Morogoro Ida Mushi na
kusema wameelewa na kwamba hawana maswalilabdla kwa wakati mwingine.
0 comments:
Post a Comment