Mh:Mwigulu
Nchemba akisaidia Kupandisha Udongo kwa Mafundi wakati alipotembelea
Kukagua Ujenzi wa Maabara ya Kisasa Shule ya Sekondari Ntwike hii leo
Jimboni Kwake Iramba.Jengo Jipya la Maabara ya Kisasa kwa Sekondari ya Ntwike.Mh:Mwigulu
Nchemba akicheza Ngoma ya asili na Wananchi wa Kijiji cha Mingela
wakati amewasili kwaajili ya Mkutano wa Hadhara wa Maendeleo.Mh:Lusinde(Mbunge wa Mtera) akibadilishana Mawazo na Mh:Mwigulu Nchemba kwenye Mkutano wa hadhara kijiji cha Mingela.
Mh:Mwigulu Nchemba akisikiliza neno Kutoka kwa Mwananchi wa Kijiji cha Mingela kata ya Ntwike.
Mh:Mwigulu
NChemba Mbunge wa Iramba akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mingela
hii leo Alipokwenda kutoa mrejesho wa ahadi yake ya Maji na Umeme,Maji
yameshaanza Kupatikana Kupitia Mradi Mkubwa wa Kisima kilichochimbwa kwa
Mfumo wa Kisasa ndani ya Kijiji hicho,Pia Kijiji hicho kipo kwenye
Mpango wa Kupatiwa Umeme kabla ya Mwezi wa sita Mwaka 2015.Mh:Mwigulu
Nchemba akiwaonesha Gari Wananchi wa Kijiji cha Nkongilangi
aliyowanunulia kwaajili ya Huduma za Afya kwenye Tarafa yao ya
Shelui.Gari hiyo ya Wagonjwa itatumika Bure kwa Wananchi bila
Kuchangishwa Mafuta.
Sehemu
ya Mamia ya Wananchi wa Kijiji cha Nkogilangi waliofika kwenye Mkutano
wa Hadhara wa Kupokea habari njema za Maendeleo ndani ya Kata yao kutoka
kwa Mh:Mwigulu Nchemba Mbunge wao.
Wananchi wa Kijiji cha Nsusu ambao wanategemea Kupata Umeme
wakishangilia baada ya Kusikia Juhudu hizo za Mbunge wao Mh:Mwigulu
Nchemba.
Mh:Diwani wa Kata ya Ntwike akitoa Mrejesho wa Maendeleo kwa Wananchi mbele ya Mbunge wa Iramba
Mh:Mwigulu Nchemba,Kubwa ni Ujenzi wa Barabara ya Kutoka Nsusu kuelekea
Kiomboi kukatisha Mlimani,Pia Ujenzi wa Maabara ya Kisasa kwa Sekondari
ya Ntwike.Pia Diwani ametoa Ushuhuda namna Kata yake inavyonufaika na
Mfuko wa Jimbo,Mh:Mwigulu Nchemba ametoa fedha mara kadhaa kusaidia
Maafa ya Kuezuliwa Shule na Makazi ya Watu ndani ya Kata ya Ntwike.Hapo
awali Wananchi na Viongozi walikuwa hawajui Mfuko wa Jimbo na Matumizi
yake,Wamejua hilo baada ya Mh:Mwigulu Nchemba kuwa Mbunge.Kada
Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi Kutoka Kitengo cha Uhamasishaji wa UVCCM
Bi.Juliana Shonza akiwasalimia Wananchi wa Kijiji cha Nsusu.
Wananchi
wanapofurahia Kukutana na Mbunge wao baada ya Kupokea habari Njema za
Maendeleo ndani ya Kata yao,Maji,Umeme,Afya na Barabara vyote
vimeshaanza kutekelezwa kwa Vitendo na Wananchi wanashuhudia Utekelezaji
huo.Wananchi wakitafuta Kila Namna kuhakikisha Wanamuona Mbunge wao,Hapa ni Kijiji cha Nkogilangi kata ya Ntwike.
Kwa
herini Wananchi Wangu"Msitamani sana Kuniona mimi kwenye Kata
yenu,Tamaa Yenu ielekezeni kuona Shughuli za Maendeleo zinaonekana na
Kufanyika kwa Ufanisi ndani ya Jimbo letu"Mwigulu Nchemba.
0 comments:
Post a Comment