Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(Meza Kuu) akifanya mazungumzo rasmi na Ujumbe Maalum toka Nchi Wanachama wa SADC unaoshughulika na Mafunzo ya Uangalizi wa Amani Kimataifa walipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza. Jeshi la Magereza Nchini limeteuliwa na Kituo cha Mafunzo ya Uangalizi wa Amani – SADC kuwa mwenyeji wa Mafunzo ya Uangalizi wa Amani wa Kimataifa yatakayofanyika hivi karibuni Nchini Tanzania.Makamishna wa Jeshi la Magereza Nchini wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani) wakati Ujumbe toka Nchi Wanachama wa SADC unaosimamia Mafunzo ya Uangalizi wa Amani Kimataifa ulipotembea Makao Makuu ya Jeshi la Magereza(wa kwanza kulia) ni Kamishna Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(katikati) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(kushoto) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kulia) akisalimiana na Ujumbe Maalum toka Nchi Wanachama wa SADC toka Kituo cha Mafunzo ya Uangalizi wa Amani Kimataifa walipotembelea leo Aprili 23, 2014 Ofsini kwake Jijini Dar es Salaam.Wawakilishi toka Nchi Wanachama wa SADC wanaosimamia Uendeshaji wa Mafunzo ya Uangalizi wa Amani Kimataifa wakimsikiliza Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) walipotembelea Ofsini kwake leo Aprili 24, 2014(wa kwanza kushoto) ni Naibu Mkufunzi Mkuu wa Kituo cha Mafunzo ya Uangalizi wa Amani – SADC, Col. Sambulo Ndlovu(katikati) ni Mkufunzi wa Kituo cha Mafunzo ya Uangalizi wa Amani – SADC, SP. Edward Njovu(kulia) ni Afisa Mwandamizi wa Utawala na Fedha katika Kituo cha Mafunzo ya Uangalizi wa Amani – SADC, N. RajabBaadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia mazungumzo rasmi yaliyofanyika Ofsini kwa Kamishna Jenerali wa Magereza kufuatia Ujumbe toka Nchi Wanachama wa SADC( wa kwanza kulia) ni Kamishna Msaidizi wa Magereza, Charles Novat(kushoto) ni Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Ahmad Mwidadi (katikati) ni Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Hamis Lisu ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu katika Kitengo cha Mahusiano ya Kimataifa Ndani ya Jeshi la Magereza(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
0 comments:
Post a Comment