Pages

Subscribe:

Wednesday, 23 April 2014

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI ACHARUKA APIGA MARUFUKU WATENDAJI WAKE KUSAINI MIKATABA NJE YA NCHI NA NJE YA OFISI ZA WIRAZA.

 Waziri wa Nishati na Madini Prof Sosipeter Muhongo akizungumza kwa hisia kali kwenye mkutano wa siku mbili wa wajumbe wa baraza la Wafanyakazi wa wizara hiyo unaoendelea kwa sasa kwenye Hotel ya Nashera Mkoani hapa


           Wajumbe wa mkutano huo

 Baada ya kufungua nmkutano huo Waziri Muhongo alipiga picha ya pamoja na wajumbe hao.
 Vile vile Waziri Muhongo alipiga picha na waandishi wa habari,niongoni mwa waadishi hao ni Mwandishi wa Mtandao huu[wanne kushoto mwenye kamera shingoni]
 Waziri huyo akiondoka baada ya kufungua mkutano huo.
                         Na Dustan Shekidele,Morogoro.
WAZIRI wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amewataka watendaji wa Wizara hiyo kuacha mara moja tabia ya kusaini mikataba inayohusu Wiraza hiyo nje ya Nchini ama nje ya ofisi za watendaji hao na kwamba mtendaji yoyote atakaye kaidi agizo hilo atimtimu kazi.

Prof Muhongo alitoa karipio hilo leo asubuhi alipofungua mkutano wa siku mbili wa baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Kitalii ya Nashera iliyopo barabara ya Boma mkoani hapa.

" Niudhaifu mkubwa kwa mtendaji wa Wizara kwenda kusaini mikataba ya Wizara nje ya Nchini au nje ya ofisini ya tendaji, kuanzia sasa ni marufuku mtendaji wa wizara yangu kufanya hivyo na atakaye kaidi nitamuondoka kazini mara moja"alisema Waziri huyo kwa hisia kali.

Vile vile Prof Muhongo amewataka wajumbe wa mkutano huo kujadini namna ya kuinua upya shilika la Tanesco,Madini na Ges.

 "Wizara yetu ni nyeti katika uchumi wa taifa letu ambapo  asilimi 75 ya uchumi wa taifa letu inategemea Wizara yetu kwamba kama umeme si wa uhakika viwanda na shughuri nyingine zitasimama pia tukishindwa kuzalisha gesim kwa wingi na kuchimba madini pato la taifa litashuka''alisema Waziri huyo ambaye sehemu kubwa ya hotuba yake aliwapiga vijembe watendaji wa wizara hiyo.

0 comments:

Post a Comment