Balozi wa amani Nchini Risasi Mwaulanga akiwa na familia yake langoni mwa hifadhi ya Taifa ya Mikumi wakati wa Ziara yake katika hifadhi hiyo.
Moja ya nyumba za kumbukumbu za rasilimali za wanyama katika hifadhi ya Mikumi Morogoro.
Pundamilia ni muongoni mwa wanyama walioko katika hifadhi ya Mikumi kama wanavyoonekana wakiwa katika harakati ya kujitafutia riziki.
Mwaulanga akiwa na familia yake katika hifadhi ya Mikumi wakati wa ziara yake.
Balosi Mwaulanga akiwa na kaimu muhifadhi mkuu wa hifadhi ya Mikumi Dattomax Selanyika ofinini kwa muhifadhi huyo.
Kundi la twiga waliokuwa katika hifadhi hiyo
Twiga akiwa katika malisho yake, mnyama huyo hupendelea kula majani ya juu kutokana na maumbile yake kama anavyoonekana.
Risasi Mwaulanga akiwa katika moja ya mahojiano na waandishi wa habari katika ziara yake Mikumi.
Swala wakia katika malisho yao katika hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro.
Kwa habari zaidi soma hapa,
Kwa habari zaidi soma hapa,
BALOZI wa amani nchini,
Risasi Mwaulanga amezishauri
kampuni zote za Umma zinazotumia nembo za wanyama na rasilimali nyingine za
taifa kuwa na wajibu katika suala zima la ukuaji katika sekta ya utalii Nchini.
Balozi huyo alisema hayo juzi wakati alipofanya ziara ya
kuhamasisha utalii wa ndani katika hifadhi ya Taifa ta Mikumi iliopo wilyani
Kilosa mkoani Morogoro.
Alisema kuwa yapo makampuni mengi yanayotumia nembo za
wanyama huku akitolea mfao kama Twiga na
Tembo na kwamba makampuni hayo yangeweza kuwa jukumu la kuhakikisha wanatumia fulsa hiyo kuwatangaza wanyama hao
kwaajili ya kukuza utalii.
‘’ Kwa mfano Benk ya CRDB wamekuwa wakifanya matamasha mengi
kuhamasisha biashara zao, lakini wanayo huduma ya tembo kadi hivyo wangeweza
kutumia fulsa hiyo kufika katika mbuga za wanyama kama Mikumi na kufanya
matamasha kama hayo kwa kumwagalia mnyama huyo porini hiyo ingesaidia kukuza
utalii wetu wa ndani’’ Alisema
Alisema badala ya sherehe za familia na zinginezo kuzifanyia
mijini kila wakati wangeweza kutumia muda wao na familia zao kufika katika
hifadhi za wanyama kwaajili ya kufanya utalii wa ndani.
Hata hivyo alisema vita dhidi ya ujangili ingeweza
kusaidiawa na makampuni kama hayo kwa kutoa motisha kwa rai wema wanaotoa taarifa
dhidi ya majangili badala ya kuiachia wizara husika peke yake huku nao
wakinufaika na nembo ya mnyama huyo.
‘’ Vita dhidi ya majangili ni jukumu la kila Mtanzania
kuhakikisha anapiga kelele kutokomeza, haipendezi vizazi vijavyo vikute mapori
na kuhadihthiwa kuwa hapa kulikuwa na wanyama na badala yake waendelee kuwepo
kama ambavyo babu zetu waliweza kuwahifadhi’’ Alisema
Kwa upande mwingine aliwataka Watanzania kujenga tabia ya
kutumia muda wao wa mapumziko kutembelea hifadhi za taifa kwaajili ya kufanya
utalii wa ndani badala ya kuona wanyama katika TV na kumbukumbu mbalimbali.
Kwa upande wake kaimu muhifadhi mkuu wa hifadhi ya Mikumi
Datomax Selanyika alisema idadi ya watalii wa ndani katika hifadhi hiyo ni
ndogo ukilinganisha na watalii wan je.
Alisema kwa kipindi cha mwaka mmoja watalii wanaotembelea
hifadhi hiyo ni 55,000 hadi 60,000 ambapo kati ya hao watalii wa ndani ni
19,000 hadi 20,000 tu.
Alisema kuwa mbuga ya Mikumi ni mbuga iliojirani na
inafikika kwa urahisi ukilinganisha na mbunga nyingine na kwamba watanzania
wangeweza kuwa wengi zaidi katika suala zima la utalii.
0 comments:
Post a Comment