Pages

Subscribe:

Wednesday 29 January 2014

MAKONDA ANAMAWENGE, ANATAKA KUTUVURUGA UVCCM

 Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM kupitia kundi la vijana Jonas Nkya akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Morogoro juu ya kauli za katibu wa chipukizi na hamasa Taifa Paul Makonda za kusema waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa  hafai kuwa kiongozi, wala mwenyekiti wa CCM taifa na hata pia kuwa amirijeshi mkuu  akimtuhumu kuwa fisadi ambapo  MNEC huyo amejia juu kusema kuwa amekurupuka na kauli  na kwamba sio msemaji wa UVCCM wanamshangaa.
Kama maisha ya Mjini yamemshinda aje vijijini tumpe shamba alime sio kuuza maneno ili apete fedha za kuishi, Lowasa alikuwa kiongozi kabla ya Makonda kuzaliwa, amekurupuka kuaongea kitu asichokijua na wala hana ridhaa ya kusema hayo,atolewe UVCCM atatuvuruga, Ni MNEC mwingine wa UVCCM Ramadhani Kimwaga akiongea na waandishi wa habari mjini Morogoro.

JUMUIYA ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM mkoa wa Morogoro  Imemtaka katibu wa chipukizi na hamasa Taifa Paul Makonda kuaomba radhi waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa , wazee, vijana na viongozi wa dini  kwa kauli aliotoa  za uchochezi na  za kukigawa chama.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM NEC  kupitia kundi la vijana    Jonas Nkya na Ramadhani Kimwaga walisema kuwa kauli hizo si za  UVCCM ni za Makonda binafsi.
 
Nkya alisema kuwa vijana wa mkoa wa Morogoro wamehuzunishwa na matamshi ya Makonda aliotoa juzi wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kumshutumu Lowasa kuwa hafai kuwa kiongozi wan chi hii, wala kuwa amrijeshi mkuu sambamba na mwenyekiti wa CCM  Taifa.
 
‘’ UVCCM hatupo kwaajili ya kutengeneza Marais, na si jukumu letu, na wakati wake haujafika hivyo tunamshangaa Makonda kuanza kuzungumzia masuala ya Urasi  na kuwachanganua nani anafaa  na nani hafai wakati sio kazi yake na aingii katika kikao chochote cha maamuzi ya kumteua mgombea Urais’’ Alisema.
 
Alisema kuwa hakuna kikao chochote cha baraza kilichokaa na kutoa tamko kama hilo na kwamba utaratibu wa UVCCM na CCM kwa ujumla maamuzi yote hutoka katika vikao halali.
 
‘’Sisi UVCCM hatutaki kuingiza masuala binafsi na  jumuiya yetu ambayo yatapelekea kukigawa chama na jumuiya zake, hivyo vijana lazima tubadirike’’ Alisema
 
Aliwataka viongozi wa dini, vijana mbalimbali aliowatamka  pamoja na Lowasa kupuuzia kauli hiyo na kwamba UVCCM wako pamoja  viongozi wa dini, vijana mbambali na hata waziri mkuu mstaafu.
 
Kwa upande wake Kimwaga alisema kuwa kauli ya makonda ya kusema kuwa lowasa hafai kuwa kiongozi ni kukitukana chama kwa kumteua kugombea ubunge jimbo la Monduli na pia kumteua kugombea ujumbe wa NEC nafasi ambazo ni nyeti  katika chama.
 
‘’ Lowasa amekuwa kiongozi wa muda mrefu katika CCM hata kabla makonda hajazaliwa na hadi sasa, hivyo kauli za Makonda zinaonyesha ni mtu mwenye  kuweweseka na hastaili kuwa kiongozi, hivyo hakuna budi kuenguliwa katika nafasi hiyo kutokana na kushindwa kuitumikia’’ Alisema
 
Alisema kuwa kuendelea kuwepo katika nafasi hiyo makonda kutasababisha kugawa UVCCM pamoja na kukivuruga chama .
 
‘’ Mtu ukimtuhumu kuwa fisadi mla rushwa ni lazima uwe na ushahidi na kama anao basi aende kushitaki mahakamani sambamba na katika vyombo husika kama takukuru, na kama hajui aje tumwelekeze ofisi zao zilipo’’ Alisema
 
Alimshauri makonda kuja vijijini  ili wamtafutie shamba  la kulima kuliko kukaa mjini kwaajili ya kuuza maneno ili apate fedha za kumwezesha kuishi.


3 comments:

Unknown said...

yale yaleeeeeeeee.vijana wa morogogoro''UMUIYA ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM mkoa wa Morogoro Imemtaka katibu wa chipukizi na hamasa Taifa Paul Makonda kuaomba radhi waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa , wazee, vijana na viongozi wa dini kwa kauli aliotoa za uchochezi na za kukigawa chama.'' sasa hapa nani msemaji wa UVCCM morogoro?

A.J.MLANZI said...

Kwa hiyo mtakuwa mnaburuzwa bila kujielezea yaliyokuwa moyoni.maaana ya kuwa mwanachama wa chama cha kisuasa ni kuweza kukosoa na kukosolewa.ukimkosoa kiongozi sio dhambi.wake up vijana

Unknown said...

Vijana wa siku hizi wana mawazo kuwa Wazee Wakati wao umekwisha au kwa lugha nyingine wamepitwa na wakati. Tabia ya namna hii ya tamaa ya kutaka watambuliwe na kujiona wenye akiri nyingi sana KUWAZIDI WAKUBWA itawaponza kukosa radhi za wakubwa hususani wazee. Kwenye mafundisho ya Dini tunaaswa kuwaheshimu wazee ili tupate Mibaraka. Lakini wazee nao wanakumbushwa kutowachokoza watoto au kutoa ishara ya kuunga maovu wanayotenda watoto. Kwa tabia ya namna hii ya UVVCCM hamtafika na sio rahisi tukawapa Nchi.

Post a Comment