Meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo akipata maelezo kutoka kwa
mwalimu mkuu wa shule ya ujirani iliopo kata ya Kihonda Philemon Kibuja
wakati wa ziara ya kamati ya fedha ya manispaa hiyo.
Tumeleta milioni 10 kwaajili ya ujenzi wa madarasa katika shule hii,
ili wanafunzi wetu waweze kusoma vizuri. Amiri Nondo akiongea katika
ziara hiyo.
Wanafunzi wa shule ya msingi Ujirani wakiwa katika moja ya chumba cha madarsa katika shule hiyo.
Tumeleta milioni 600 katika Hospitali ya wilaya inayojengwa hapa Kiegea
ili kurahisisha huduma ya afya kwa wakazi wa huku na jirani. meya wa
manispaa ya Morogoro Amiri Nondo akitoa taarifa kwa kamati hiyo.
Meya huyo akiangalia moja ya nguzo inayojengwa katika Hospitali hiyo ya wilaya ya manispaa ya Morogoro.
Madiwani na watendaji wa manispaa ya Morogoro wakiongea na injinia wa
kampuni ya Mzinga inayofanya ujenzi katika hospitali hiyo ya wilaya.
Kwa kawaida ujenzi wa kampuni ya mzinga tunaukubali, ni maneno ya Maya Nondo.
Baadhi ya wagonjwa waliofika kupata huduma katika kituo cha afya cha Uhuru maarufu kama Nunge .
Diwani wa kata ya Kingo Fidelis tailo akimpa maelezo meya wa manispaa
ya Morogoro kuwa hospitali hiyo imeelemewa, . hakuna stoo, madaktari
wanatumia chumba kimoja wanne, huduma za usiri kwa wagonjwa hakuna.
Nimechelewa kidogo maana ratiba sikuipata vizuri, karibuni jamani
Mjimpya, ni diwani wa Mjimpya Wensilaus akiwakaribisha madiwani wenzake
waliotembelea stendi mpya ya magari yanayokwenda nje ya manispaa ya
Morogoro.
Hapa ndio yatapakia magari ya Mgeta, stendi hii itapunguza msongamano pale mjini .
0 comments:
Post a Comment