ZAIDI YA BILIONI 12 ZIMEIDHINISHWA KATIKA BARABARA NA MADARAJA MKOA MOROGORO MWAKA 2014
JUMLA ya shilingi bilioni 12.527.888 zimeidhinishwa kutumika kwaajili ya kazi za matengenezo ya
barabara na madaraja mkoani Morogoro
katika mwaka wa fedha 2013/2014.
Meneja wa wakala wa barabara mkoa wa Morogoro Injinia Doroth Mtenga alisema hayo wakati
akitoa taarifa katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika Januari 9 mwaka
huu mjini Morogoro.
Aidha alisema kuwa fedha hizo zinaunganishwa na shilingi bilioni 11.277.885 za mwaka wa fedha
wa 2012/2013 kukiwa na ongezeko la shilingi bilioni 1,250,000 sawa na asilimilimia 11.08.
Alisema kuwa fedha hizo ni kwaajili ya sehemu korofi ,
matengenezo ya muda maalumu, matengenezo makubwa ya madaraja, matengenezo ya kawaida ya barabara
na madaraja.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa
wa Morogoro ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini alisema kuwa
pamoja na kupewa fedha hizo lakini pia ni lazima kuweka mikakati ya
kudhibiti uharibifu wa miundombinu ya
barabara.
Alilalamikia tatizo la wafanyabishara wanaoweka bishara zao
barabarani na kusababisha magari kusimama hovyo na kuharibu barabara kuwa
uchukuliwe hatua.
Hata hivyo alisema kuwa jeshi la polisi kupitia idara ya
usalama wa barabarani waangalie uwezekano wa kuwa na maeneo maalumu ya
kusimamisha magari ili kuepuka kusimamisha hovyo na nivyo kupelekea kuharibu
barabara.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa bodi ya barabara wakiwa katika mkutano wa 30 uliofanyika Janurai 9 mwaka huu mjini hapa.
Baadhi ya wajumbe wakifutilia mkutano wa bodi ya barabara.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mvomero Jonas Van Zeelanda akizungumza katika mkutano huo.
Wabunge , Mustapha Mkullo wa Kilosa kati, Dk Haji Mponda Ulanga
Magharibi, na Abdusalamu Sasi wakifutilia mkutano hu o kwa makini sana.
Mwenyekiti wa CCM Inocent Karogeries katikati, Celina Kombani mbunge wa
Ulanga mashariki, na meya wa manispaa ya Morogoro Amini katika mkutano
huo.
Wajumbe wa bodi ya barabara wakifutilia kikao hicho.
0 comments:
Post a Comment