MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Morogoro
Inocent Karogeries amemlaumu spika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Anna Makinda kukubali kumweka mwenyekiti
wa tume ya kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji Ole Sendeka wakati yeye hana sifa kushika
wasidhifa huo kwa sababu yeye ni miongoni mwa wafugaji wakubwa hapa nchini.
Alisema hayo jana wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya
mkoa wa Morogoro RCC iliofanyika mjini Morogoro.
Alisema kuwa wabunge wanatambua kuwa mwenyekiti wa kamati ya
kudumu ya kilimo na mifugo ni mbunge wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Profesa
Petter Msolwa ambaye ndiye alipaswa kuwa mwenyekiti wa kamati teule ya
kushugulikia migogoro ya wakulima na wafugaji.
‘’ Tumeshangaa kuona spika amemchagua Ole Sendeka kuwa
mwenyekiti wa katati teule wakati yeye ni miongoni mwa wafugaji wakubwa hapa
nchini’’ Alisema
Alisema kuwa katika migogoro kama hiyo ili haki itendeke ni
lazima apatikane mtu ambaye hafungamani na upande wowote ili aweze kutenda haki
wakati wa maamuzi.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa CCM alisema kuwa kilichotokea
katika utekelezaji wa kamati hiyo kwa mkoani wa Morogoro ni kwamba kamati hiyo
haikushirikisha kiongozi hata mmoja wa chama wa Serikali na badala yake
walikwenda wenyewe jambo ambalo linaashiria kutofanya kazi zake kikamilifu
kwani wenyewe wanaojua vyanzo vya migogoro ya maeneo husika hawakushirikishwa.
‘’ Sisi kama viongozi wa Morogoro Kusini tulijipanga kushirikia
vizuri katika ziara hiyo lakini chaajabu kamati hiyo ilipofika iliwakataa, mimi
kama mbunge wa jimbo la Morogoro kusini nililazimisha nikaongozana nao lakini
sikupewa hata nafasi ya kusema chochote badala yake ni kujitambulisha tu’’
Alisema
Alisema kuwa baadhi ya viongozi wakubwa hapa nchini wamekuwa
wakimiliki mifugo na kwamba ndio
wanakwamisha zoezi la kuwaondoa wafugaji kwa kuandika ujumbe kwa watendaji ili
waache mifugo yao.
Hata hivyo mbunge huyo alisema kuwa kama mkoa kwa kutumia kamati hiyo teule wanahakika kuwa
tatizo la migogoro ya ardhi haiwezi kutatuliwa na badala yake kuna kila sababu
ya kuhakikisha wanaainisha mashamba makubwa ambayo ni mapori na kwenda kwa Rais
ili ayafute.
‘’ Mimi nawambie watendaji kwa zoezi hili kwa kuwa mmegusa
maeneo ya wakubwa hao tegemeeni mara baada ya taarifa ya tume hiyo kusoma hapo
mwezi juni mwaka huu, tegemeeni kuhukumiwa katika kazi zenu, lakini niwahakikishie kazi
nzuri mmefanya sisi kama CCM tutahakikisha tunawatetea hadi , Alisema
Viongozi wa wilaya ya Mvomero wakifutilia kwa makini mkutano huo
0 comments:
Post a Comment