Mgombea udiwani kata ya Tungi manispaa ya Morogoro kwa tiketi ya Chama
cha Mapinduzi CCM Deogratias Mzeru akikabidhi fomu ya kuwania udiwani
kwa mtendaji wa kata hiyo Abuu Liwangira Januari 15 mwaka huu.
Mgombea Udiwani Mzeru akikabidhi fomu zake kwa mtendaji wa kata ya
Tungi mbela ya katibu wa CCm wilaya ya morogoro mjini Ali Isa.
Hongera Mzeru, tumekuja kukuunga mkono wenzako, ni wagombea udiwani wa kata ya Tungi Lusajo Manase na Godfrey Taiko .
Tuko pamoja na ushindi ni lazima, mimi niko CCM muda mrefu sana hivyo
lazima tuhakikishe CCM inashinda Tungi. Godfrey Taiko akimwambia mgombe
mwenzake Mzeru waliomsindikiza kuchukua fomu ya kuingia katika
kinyang'anyiro hicho.
Pamoja sana Mzeru, tumekuja kukusindikiza , CCM ushindi ni lazima.
katibu kata wa CCM kata ya Tungi Zulfa akiwa katika picha ya pamoja na wagombea udiwani wa kata hiyo.
Nani kasema imekaa vibaya, CCM imekaa vizuri, . Mzeru amekaa vizuri. jeshi la CCM ndani ya Tungi.
Mnajua sisi wanawake lazima tuhakikishe kinaeleweka hapa Tungi ama
sivyo jamani, katibu wa UWT Dotto akiwaambia wanawake wa manispaa ya
Morogoro
Vijana wa CCM wakia nje ya ofisi ya mtendaji wa kata ya Tungi wakisubiri mgombea udiwani Mzeru kurejesha fomu.
Hatutaki matusi, wala kejeri katika uchaguzi huu, kila chama kinadi
sera zake, wananchi wanahitaji sera na maendeleo na sio matusi, Mgombea
udiwani kata ya Tungi kwa tiketi ya chama cha Jahazi Asilia Ismail
Ismail . alipofika katika ofisi ya kata na kuongea na wanachama wa CCM.
Makada wa CCM wakijadiliana nje ya ofisi ya mtendaji kata ya Tungi
Viongozi wa CCM wilaya ya Morogoro mjini wakisubiri mgombea wao Mzeru kurejesha fomu nje ya ofisi ya mtendaji kata ya Tungi.
Wananchi wa kata ya Tungi waliomsindikiza mgombea wao Mzeru kurejesha fomu wakiwa katika picha ya pamoja.
CHAMA cha mapinduzi CCM wilaya ya Morogoro kimewataka
wagombea udiwani katika kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro ambao hawakuteuliwa
kushirikiana na mgombea aliyeteuliwa katika kukupatia ushindi wa kishindo.
Katibu wa CCm wilaya hiyo Ali Isa alisema hayo jana wakati
akiongea na baadhi ya wagombea hao katika kata ya Tungi mara baada ya Mgombe
udiwani aliyeteuliwa na CCM Deogratias Mzeru kurejesha fomu katika ofisi ya
mtendaji kata wa Tungi.
Alisema kuwa CCm inautaratibu katika mchakato wa kupata
viongozi na kwamba katika mchakato huo wagombea ambao hawakuteuliwa wasikate
tamaa.
Alisema kuwa CCM itaanza mikutano yake ya ndani Januari 16
mwaka hu na kwamba wanatarajia kuzindia kampeni rasmi januari 26 mwaka huu
ambapo mgeni Rasmi atakuwa Asha Rose Migiro ambaye ndio mlezi wa wilaya hiyo.
‘’ wagombea ambao hawakupata fulsa ya kuteuliwa nawaomba
washirikiane katika kumnadi huyo aliyeteuliwa ili CCM ishinde kwa kishindo’’
Alisema.
Kwa upande wao wagombea hao Godfrey Taiko alisema kuwa yeye
ni kada wa siku nyingi ndani ya CCm na kwamba kutoteuliwa katika nafasi hiyo
hakuwezi kumfanya akakisaliti chama na kwamba nafasi ziko nyingi anaimani
atapata nafasi zingine.
Naye Lusajo Mwambogo alisema kuwa atashirikiana vizuri
katika kumnadi mgombe huyo ili kuhakikisha CCm inashinda kwa lengo la kuletea
maendeleo kata hiyo ya Tungi.
Uchaguzi huo umekuja baada ya diwani wa kata hiyo Daud Mbao
kufariki dunia kutokana na kuugua kwa muda mrefu Ugonjwa wa Kisukari.
0 comments:
Post a Comment