Pages

Subscribe:

Tuesday, 3 September 2013

WAADHIRI WA VYUO VIKUU WASHAURIWA KUTUMIA TAALUMA ZAO JUU FULSA ZA TAASISI ZA KIFEDHA WAWEZE KUJIAJIRI

KATIBU tawala mkoa wa Morogoro Eliya Ntandu amewashauri wahadhiri wa vyuo vikuu nchini kutumia taaluma zao kuwafundisha wanafunzi  juu ya uwepo wa fursa mbalimbali za taasisi za kifedha zitakazowawezesha kujiajiri  kupitia mikopo, na kuzifahamu mbinu za uanzishaji  wa miradi yenye tija hasa ya  sekta ya kilimo.
 

Ntandu alitoa ushauri huo jana  wakati akiongea na wahadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali vilivopo mkoani Morogoro, kwenye mafunzo ya ujasiriamali, yaliyoshirikisha vyuo vikuu sita vilivyoko mkoani Morogoro liyoandaliwa na Uongozi wa benki ya CRDB Mkoa wa Morogoro.

Ntandu alisema kuwa tofauti na elimu inayotolewa kwenye mikutano, semina na makongamano, nafasi ya wahadhiri kufikisha elimu kwa wanafunzi na kubadilika ni kubwa sana hivyo hawana budi kuwaelimisha vijana namna bora ya kuondokana na umaskini kwa kujiajiri na kutengeneza ajira kwa kuzitumia taasisi za kifedha kama mabenki.

Katibu tawala huyo wa Mkoa aliwaasa wahadhiri hao kuwafundisha wanafunzi wao kuwekeza kwenye kilimo kutokana na fursa pana za ajira zilizopo katika eneo hilo, na umuhimu wa kilimo katika maisha ya kila siku.
Naye  Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoa wa Morogoro,Pendo Assey, alisema wameamua kuwafikia wahadhiri  kwa kuwaeleza namna watakavyoweza kutumia fursa zilizopo katika benki hiyo, na ikibidi kuboresha mitaala yao kuendana na mazingira ya fursa zilizopo.
Assey alibainisha kuwa kwa kuamini iwapo wahadhiri na wanafunzi watatumia vizuri fursa  hizo za mabenki, wanaweza kunufaika na kuwa mfano kivitendo na hata kuwawezesha kielimu na utaalamu wanafunzi wanaowategemea.
Alisema mafunzo  hayo ya ujasilimali kwa wahadhiri wa vyuo vikuu yanalenga kuwapa uelewa mpana wa  masuala uendeshaji wa  biashara  ndogo ,za kati na bishara kubwa  na hivyo kuwawezesha kuanzisha biashara zao  ili kuinua uchumi wao na hata kutoa mafunzo hayo kwa  jumuiya ya wanafunzi vyuoni  .

Mkurugenzi huyo alibainisha mafunzo hayo yamelenga pia kupunguza  tatizo la ajira kwa vijana  wanaohitimu  vyuo vikuu  ambalo limekuwa kubwa nchini,  na kwamba kupitia elimu  ya watakayopata  kwa walimu wao ,  watakuwa na uwezo wa kujiari wenyewe badala ya kusubiri
kuajiriwa.
Kwa upande wao baadhi ya wahadhiri waliopata mafunzo hayo, Prof Moses Warioba kutoka chuo Kikuu Mzumbe,  Dr. Lucy Chove kutoka chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Dk Said Masomo ambaye ni Mkurugenzi chuo kikuu huria kituo cha Morogoro na Ruben Mwakibula wa AMBIANCE, walisema mpango huo kutaleta ukombozi wa kiuchumi kwao na taifa kwa ujumla, kwani wanauwezo mkubwa wa kuwekeza na kubuni miradi  ya kiuchumi sambamba na kuahidi kufikisha elimu hiyo kiufasaha kwa wanafunzi wao.
Aidha wahadhiri hao waliishauri CRDB kufanya utafiti ili kujua elimu wanayotoa wahadhiri kama inawafikia watu wengi hususani wa vijijini na kwamba Mafunzo hayo yatasaidia kuwapa ujasiri  wahadhiri na wanafunzi kukopa  kwenye taasisi za fedha .
Mwisho.

0 comments:

Post a Comment