WATU
watatu wanaosadikiwa kuwa ni mjambazi wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani
Morogoro na wengine watatu wakitafutwa kwa
tuhuma za kumuuwa mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya Omega na kumjeruhi mwenzake
wakati wakilinda katika ghala la kampuni ya Coca Cola.
Kwa
mujibu wa kamnada wa Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile alisema kuwa tukio
hilo lilitokea Agosti 31 mwaka huu majira ya saa 9 usiku katika ghala la
kampuni ya Coca Cola iliyopo maeneo ya Mtawala manispaa ya Morogoro.
Shilogile
alimtaja mlinzi aliyeuwawa kuwa ni Elisha Simangwa Paulo (45) mkazi wa Msamvu na kwamba alifariki dunia papo hapo baada
ya kupigwa na kukatwakatwa kwa mapanga sehemu mbalimbali a mwili wake huku
mlinzi mwenzake Otto Oscal Chakala(45) mkazi wa Chamwino kujeruhiwa vibaya sehemu
ya kichwani na amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro akipatiwa
matibabu.
Kamanda
huyo alisema kuwa majambazi hao waliwavamia walinzi hao wakiwa lindoni kwa nia
ya kutaka kuiba fedha za kampuni hiyo ya Coca Cola lakini baada ya kurupushani
baina yao na walinzi na kusababisha kifo na majeruhi walitoroka kwa kuruka ukuta huku jambazi mmoja ambaye anashikiliwa na polisi inadaiwa
alipigwa na risasi na mmoja wa walinzi sehemu ya mguuni wakati wa kurupushani
hiyo.
Aidha
alisema kuwa polisi ilipata taalifa kutoka kwa raiya mwema kuwa mmoja wa majambazi aliyejeruhiwa natafuta
usafiri kwa nia ya kutoroka,ndipo walipomkamata eneo la msamvu huku akiwa na
silaha aina ya short Gun MV 65552 ambayo
walitoroka nayo kwa kumnyang’anya mlinzi.
Kamanda
Shilogile alisema kuwa jambazi huyo pia alikutwa na mapanga matatu pamoja na
nyundo huku Pipiki yenye namba za usajili T 169 BXM aina ya SanlG ikikamatwa
kutokana na kutumika katika tukio hilo na
kwamba hakuna mali iliyoporwa katika kampuni hiyo ya Coca Cola.
Pia
kamanda Shilogile alisema kuwa mmoja wa
majambazi hao anayeshikiliwa na jeshi la polisi awali alikuwa mlinzi wa kampuni
ya Omega na alifukuzwa ,na aliwahi kufanya tukio la ujambazi katika kampuni ya
Coca cola na kwamba kwasasa ana kesi mahakamani .
Shilogile
amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na kutoa taarifa pale wanapokuwa
na mashaka juu ya watu ambao hawaeleweki katika maeneo yao,na kumpongeza
mwananchi aliyefanikisha kukamatwa kwa baadhi ya majambazi hao na kwamba msako mkali
unaendelea kwa ajli ya kuwapata majambazi walitoroka.
Mama
mzazi wa marehemu Elisha Imanga,Roida
Simanga akizungunza na waandishi wa habari mjini hapa kwa huzuni alisema kuwa
amesikitishwa na tukio la kuuwawa kwa mwanae akiwa kazini na kuitaka serikali
kuchukua sheria kali dhidi ya watu wnaofanya uhalifu.
“Naomba
serikali na polisi kufanya kila njia kuwakamata na kuwachukulia hatua za
kisheria majambazi waliohusika na haya mauaji ya mwanangu,hapa nasubili
uchunguzi na kuruhusiwa na polisi ili nichukue mwili na kusafirisha kwenda
Njombe kwa ajili ya kuzika,”alisema mama huyo
Mwisho..
0 comments:
Post a Comment