Pages

Subscribe:

Sunday, 27 April 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00207GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.959 BMM AINA YA TOYOTA L/CRUISER 110 LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA FARAHAD ABDUL (26) MWARABU – MSIMAMIZI WA KAMPUNI YA KUCHENGUA DHAHABU YA PIRBAKISH MKAZI WA CHUNYA LILIPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA SEIF MOHAMED (27) MKAZI WA NZEGA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 27.04.2014 MAJIRA YA SAA 22:45 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAKONGOLOSI, KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, BARABARA YA MAKONGOLOSI/MKWAJUNI, WILAYA YA CHUNYA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WAWILI WALIJERUHIWA 1. FARAHAD ABDUL (26) DEREVA WA GARI HILO AMBAYE AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA RAYMOND SIKAONA (29) MFANYAKAZI KATIKA HALMASHAURI YA MJI MDOGO WA MAKONGOLOSI AMBAYE ALIKUWA ABIRIA NA AMELAZWA HOSPITALI YA  MWAMBANI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA JAPO KUWA AMELAZWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
KATIKA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA  SANGAMBI, TARAFA YA  KIWANJA, WILAYA YA  CHUNYA, MKOA WA MBEYA MTU MMOJA AITWAE JAPHET NZOWA (39) MFANYABIASHARA, MKAZI WA SANGAMBI AKIWA NA POMBE KALI[VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA  BOSS PAKETI 173 NA RIDDER PAKETI 60.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 28.04.2014 MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA SHOGA, KATA YA  SANGAMBI, TARAFA YA  KIWANJA, WILAYA YA  CHUNYA, MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JOHN DAWILO (29) MKAZI WA SHOGA AKIWA NA POMBE KALI[VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI AINA YA  BOSS PAKETI 61 NA RIDDER PAKETI 15.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 28.04.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:-
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

0 comments:

Post a Comment