Pages

Subscribe:

Monday, 12 May 2014

VIZEE VINAVYOKIUKA MISINGI YA MWALIMU NYERERE VISIENZIWE; MWIGURU

 Naibu katibu mkuu wa CCM Mwiguru Nchemba akipokelewa wilayani Gairo alipokwenda jana kwa ziara yake ya siku moja  wilayani humo.

 Nchemba akisalimiana na wananchi wa wilaya ya Gairo.

 Nchemba alipowasili katika ofisi ya CCM wilaya ya Gairo ambapo alikutana na kamati ya siasa ya wilaya hiyo kabla ya mkutano wa hadhara.

 
 Mkuu wa wilaya ya Gairo Khanifa karamagi akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ialani kwa Nchemba katika kikao cha kamati ya siasa.

 Nchemba wakati akielekea katika mkutano wa hadhara

 Nchemba akisalimiana na wananchi wa Gairo waliofurika katika mkutano huo


 Mwiguru akizungumza na wananchi katika mkutano huo wa hadhara.

 Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli akizungumza kabla ya kumkaribisha mwiguru katika mkutano wa hadhara Gairo.


Awali Mwiguru alipowasili katika ofisi za CCM akivalishwa skafu. 

habari zaidi soma hapa


NAIBU katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM Mwiguru Nchemba amesema wazee wanaofuta misingi ya kudumisha amani na utulivu wanchi alioacha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wataheshimiwa na kuenziwa na chama hicho na kwamba wale wanaokiuka wabezwe kwani hawana nia njema na nchi.

Mwiguru   ambaye pia ni naibu waziri wa fedha alisema hayo jana wakati wa ziara yake wilayani Gairo ambapo alifanya mkutano wa hadhara kuzungumzia kero kubwa ya maji inayokabili wilaya hiyo.

‘’ Wazee wote ambao wanafuata misingi ya baba wa taifa kudumisha amani na utulivu wan chi CCM itawaheshimu na kuwaenzi, lakini wale ambao wakati baba wa Taifa alikuwepo wakawa wanajificha kwa unafiki wao na sasa wameona kuwa hayupo wajitokeze na kutaka kuvuruga amanni na utulivu tulionao hatuwawafumbia macho’’ Alisema

Alitolea mfano mmoja wa wazee hao ni Jaji Warioba ambaye alipewa heshima ya kukusanya maoni ya katiba na kazi hiyo alishakamilisha lakini cha kushangaza bado kila kukicha anakaziania kuwepo kwa Serikali tatu jambo ambalo kamwe CCM halitakubali.

‘’ Huyo mzee ni waajabu kweli, alipewa kazi ya kusimamia ukusanyaji wa maoni ya katiba lakini sasa kila kukicha unamwona kwenye vyombo vya habari akililia serikali tatu, hana nia njema na serikali yetu , msimamo wa CCM ni serikali mbili tuu’’ alisema

Aliwataka vijana kutambua kuwa serikali tatu ni mzigo ambao haubebeki na kwamba watakaoumia ni watanzania kwa kuongezewa kodi mara dufu ya hivi sasa.

‘’ Kwa sasa tunahangaika kutafuta ajira kwa vijana, hizo fedha za kuendeshea serikali tatu badala ziende kwenye mambo ya maendeleo na  ili vijana waweze kupata ajira ‘’ alisema
Alisema kuwa kwa sasa  kwa sasa pato la taifa ni tririoni 7.7 na kati ya hizo tririoni 4 zinatumika kwa kulipa mishahara ya wafanyakazi  na zilizobakia ndio fedha za maendeleo.

‘’ Sasa hii serikali ya tatu ikija hizi fedha za maendeleo ndio ziachuhudumia huko na kwamba fedha za maendeleo tutegemee kwa wafadhili hiyo inaingia akilini kweli? Alihoji

Hata hivyo alisema watahakikisha inakuwepo sheria  itakayosimamia fedha za mfuko wa vijana ambazo zitakuwa zinatoka moja kwa moja  badala ya kupitia katika mifumo mingine ambapo mara nyingi imekuwa ikikwamisha.

Alifafanua na kusema  upo utaratibu wa kila halmashauri kutoa fedha za mfuko wa vijana ambao kwa asilimia kubwa hazifikii walengwa kama ilivyokusudia na kwamba sheria hiyo itasaidia kubana mfumo huo na hivyo fedha kufikia vijana moja kwa moja.




Wakati huo huo alisema
NAIBU waziri wa Fedha Mwiguru Nchemba ametangaza vita dhidi ya matajiri wanaokwepa kodi kwa kushirikiana na mawakala  na watumishi wa Serikali na kwamba ameomba kupewa taarifa ili aweze kupambana nao.
Mwiguru alisema hayo jana wakati wa ziara yake wilayani Gairo mkoani Morogoro alipokwenda kusikiliza kero ya maji kwa wananchi wa wilaya hiyo.
‘’ Tunaingia rasmi kwenye vita ya wakwepa kodi, kama kuna mawakala, watumishi  wanaoshirikiana na matajiri hao tupeni taarifa ili tuwashughulikie, hatuwezi kuzoza kodi kwa wauza vitumbua huku matajiri wanakwepa kodi’’ Alisema
Alisema wanaandaa sheria ya kufuta misamaha kwa ya kodi kwa watu ambao hawastahili sambamba na kuweka sheria bitakayosimamia kuziba mianya ya ukwepaji wa kodi.
‘’ Wapo matajiri ambao ikiwekwa kodi wanawatumia wananchi kulalamikia ili wafutiwe kwa kigezo cha kutokuwa na uwezo, sio watanzania wote hawana uwezo ambao labda ukiweza kodi kwenye simu washindwe kulipa, mbona milio ya simu wanakwatwa fedha lakini hawalalamiki , hii tumeshaibaini na sasa tutaishughulikia’’ Alisema
Hata hivyo alisema kuwa wanaangalia  uwezekano wa kupekela sheria ya usimamizi mzuri wa fedha za Serikali .
Kwa upande mwingine Mwiguru aliwatoa hofu wananchi wa Gairo atahakikisha wanapatiwa visima vya maji vya muda wakati wakisubiri mradi mkubwa  unaofadhiliwa na benk ya dunia ambao kwa sasa unasuasua kutokana na kuwepo na maji ya chumvi katika yvanzo vilivyokusudiwa kwaajili ya mradi huo.
Alisema kwa sasa amepata taarifa kuna maji yanayotoka katika mto uliopo jirani na mradi huo na kwa kuaznia watatumia kiasi cha shilingi milioni 300 za fedha za ndani kupata visima hivyo huku juhudi za kuhakikisha chujio la kuchuja maji ya chumvi zinaendela kufanyika.
Alisema tatizo la maji  ni ajenda tofauti na inatakiwa kushughulikiwa na kupewa uzito wa kipekee na kwamba isihusishwe na masuala ya kisiasa kama ambavyo wapinzani wamekuwa wakitumia mwanya huo kwa sasa.
Alisema serikali inatambua umuhimu wa maji kwa wananchi wake na ndio maana hata katika bajeti ya mwaka huu fedha nyingi zimeelkezwa katika miradi ya maji ili kuhkikisha wananchi wanaondokana na dhana hiyo.

 

0 comments:

Post a Comment