Pages

Subscribe:

Tuesday, 27 May 2014

BILIONI 1.5 KUTUMIKA KWAJILI YA SHUGHULI ZA UPIMAJI WILAYA YA MVOMERO

 Waziri wa ardhi nyumba na makazi Anna Tibaijuka akiangalia mabango yalioshikwa na wanafunzi wakimpongeza kwa juhudi zake za kuwapimia ardhi katika kijiji cha Lukenge Tarafa  ya Turiani wilayani Mvomero  kijiji ambacho mwaka jana  yalitokea mapigano baina ya wakulima na wafugaji kugombea ardhi na kusababisha vifo vya watu sita , na sasa kijiji hicho kimefanywa ni cha kihistoria na cha mfano.

 Waziri Tibaijuka akizindua masijala ya ardhi ambayo itatumika kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali za masuala yote ya ardhi kwa kijiji hicho.

 Wanafunzi  walimpokea waziri huyo kwa mabango yenye ujumbe mbalimbali ulioashiria kushukuru waziri huyo na watumishi wa wizara hiyo kwa kuwapimia kijiji hicho.

 Waziri huyo akionyeshwa ramani mbalimbali za kijiji hicho ambazo kwa sasa zinapatikana kijijini hapo.

 Waziri Tibaijuka akionyeshwa ramani katika eneo la Mkindo pamoja na kupewa malezo ya alama za mipaka ya mawe yanayoweka kwa sasa ambayo ni mita moja kwenda juu tofauti na yale yaliozoeleka yanayojengewa chini, mawe hayo yanaokana kwa urahisi, yanatenganisha mipaka ya kijiji na kijiji na yanakuwa yameandikwa majina ya kijiji husika.

 Mwenyekiti wa kijiji cha Lukenge Sakayo Ole Kosiando akitoa maelezo kwa waziri huyo jinsi yeye alivyoanza kulima shamba la mfano la nyasi za malisho ya Ng'ombe ambapo aliahidi ifikapo Desemba mwaka huu atakuwa amepanda nyasi hizo ekari 10,000  kwaajili ya malisho ya ng'ombe zake ili kuepusha mifugo yake kuzurula hovyo na kuingia katika mashamba ya watu hali inayosababisha migogoro baina yao na wakulima, alidai wafugaji wenzake wanambeza hawataki kulima nyasi.

 Waziri Tibaijuka akitoa hatimiliki za kimila kwa wakazi wa kijiji hicho ambao wengi wao wamejiandikisha  umiliki wa watu wawili kama mke na mume kwa lengo la kuondokana na mfumo dume.

 mama na mwanae wakipokea hatimiliki yao ya mila kutoka kwa waziri huyo.

 Wanakijiji hao wakiwa katika picha ya pamoja na waziri huyo mara baada ya kupokea hatimiliki hizo.

 Waziri huyo akikagua shamba la mfano la mwenyekiti wa kijiji hicho Sakayo  alilopanda nyasi  za malisho ya mifugo.

 Wafugaji jamii ya wamasai wakimsikilia kwa makini waziri huyo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.

 


0 comments:

Post a Comment