Pages

Subscribe:

Friday, 14 March 2014

MBUNGE WA MORO KUSINI ALILIA FIDIA ZA WANANCHI WAKE KIDUNDA

 Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Inocent Karogeries akiongea kwenye warsha ya siku moja ya wadau  kujadili taarifa ya tathimini ya athari za  kijamii  na mazingira ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Ngerengere  hadi Kidunda pamoja na mtambo mdogo wa kuzalisha umeme na njia ya umeme kutoka Kidunda  wilaya ya Morogoro hadi Chalinze , warsha hiyo imefanyika katika hotel ya kitalii ya Nashera mjini hapa.

 Muu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Mecksadik akiongea juu ya mafanikio ya mradi huo  wa maji katika miko ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro, ambapo amesema wananchi wa Dar wanatumia zaidi ya lita peke yake wanatumia lita milioni 450 kwa siku.

 Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza  akiongea wakati wa warsha hiyo.

 Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akifungua warsha hiyo ambapo alisisitiza jinsi ya utunzaji wa mazingira ili kuhakikisha  maji yanapatikana kwa wingi katika mikoa hiyo ili kuepuka kutumia maji ya visima ambapo mengine hutumia gharama kubwa kuyatibu.

 Katibu mkuu wizara ya maji mwandisi Bashir Mrindoko akiongea wakati wa warsha hiyo.

 Mwenyekiti wa badi ya DAWASCO  Eva Sinale akiongea wakati wa warsha hiyo
 Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifutilia kwa makini ufunguzi wa warsha hiyo.

Wajumbe wa mkutano huo wakiwa makini kufutilia warsha hiyo.



Mbunge wa jimbo la Morogoro kusini Inocent Kalogeries ameitaka Serikali kuharakisha malipo ya fidia ya wananchi wa eneo linapotarajia kujengwa bwawa la maji la Vidunda ili kuondokana na kero hiyo.
Alisema hayo wakati wa warsha ya kujadili taarifa  ya tathimini ya athari za kijamii  na mazingira ya mradi  wa ujenzi wa barabara ya Ngerengere hadi Kidunda na mtambo wa  kuzalisha umeme na njia ya umemem kutoka kidunda hadi Chalinze .

Alisema kuwa mpaka sasa kuna kero hiyo kwa wananchi wake na kwamba wanakosa majibu wao kama wanasisas  juu ya fidia za wananchi hao.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na umuhimu wa bwawa hilo atahakikisha anawashawishi wabunge wa mikoa ya Dar, Pwani  na Morogoro kuhakikisha wanapigania bajeti ya  maji kuongezwa ili kusaidia ujenzi huo na fidia za wananchi hao kwa haraka.

Katibu mkuu Muhandisi Bashiri Mrindoko alisema kuwa fidia kwa wananchi hao ni bilioni 3.6 ambapo alidai kuwa ujenzi wa bwawa na barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe pamoja na umeme huo utagharimu kiasi cha dola za Marekani  milioni 160.

0 comments:

Post a Comment