Pages

Subscribe:

Thursday, 15 August 2013

KCB BENK YATOA KIFAA CHA KUPIMIA MOYO MORO




HOSPITALI ya rufaa ya mkoa wa Morogoro imepatiwa kifaa kikubwa cha CARDIAC MONITOR chenye thamani ya shilingi milioni 12 itakayosaidia kutoa mwongozo wa mapigo ya moyo na kubaini magonjwa mbalimbali
 Kifaa hicho kimetolewa jana na  Benki ya Kenya commercial bank KCB TanzaniaMkoani hapa.
                                                      
Meneja wa  KCB tawi la Morogoro   Hogla Laiser  alikabidhi mashine hiyo jana mkoani hapa kwa uongozi wa hospitali hiyo


Meneja huyo alisema waliamua kutoa mashine hiyo katika hospitali  hiyo kubainika kutokana na uongozi huo kujenga imani kwao kwa utunzaji wa vifaa mbalimbali vikiwemo vilivyotolewa Benki hiyo cha baby wamer chenye thamani ya shilingi milioni 7.3 walichopatiwa mwaka jana ambacho hadi sasa bado kipo katika hali nzuri.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Haruni Nyagori na daktari
mshauri wa watoto Dk. Horace Msaki walisema kuwa kifaa hicho kitasaidia kwa kiasi kikubwa kubaini matatizo hayo ya watoto.
Kwa kweli kifaa hiki ni muhimu sana kwa matumizi ya vipimo vya moyo kwa watoto, itasaidia kubaini matatizo mapema’’ Alisema Dk Nyogori.
Madaktari hao waliwataka  taasisi zingine kujenga tabaia ya kusaidia vifaa kama hivyo na vingine ili kuweza kupata huduma mbalimbali kwa ufanisi zaidi.

0 comments:

Post a Comment