HATIMA ya Katibu wa taasisi na Jumuiya za Kiislam
Tanzania Shekhe Ponda Issa Ponda kupewa dhamana au kunyimwa itajulikana Septemba 17 mwaka huu katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa
wa Morogoro baada ya hakimu wa mahakama hiyo Richard
Kabate kushindwa kutoa kutoa dhamana hiyo jana kwa mdaia kuwa suala
hilo lipo kisheria zaidi na hivyo apewe muda kulifanyia maamuzi.
Hakimu mkazi Mfawidhi mkoa wa
Morogoro Richard Kabate alitoa kauli hiyo mahakamani hapo baada ya mwanasheria mkuu
wa serikali Bernard Kongola kuwasilisha hati ya kupinga dhamana ya mshitakiwa
huyo iliotolewa na mkurugenzi wa
mashitaka DPP.
Hatua hiyo ilikuja baada ya wakili
wa upande wa utetezi unaoongozwa na
wakili Juma Nasoro pamoja na Ignas Punge
na Bartlomelo Tarimo
Kuwasilisha maombi mawili la kuomba
mshitakiwa kupewa dhamana kutokana na kesi inayomkabili kuwa na dhmana,
sambamba na kuomba kupata maelezo ya mlalamikaji ili upande wa utetezi kuweza
kuanza utetezi ombi ambalo mwansheria mkuu wa serikali alisema kuwa
wamelikubali.
Hata hivyo baada ya mwanasheria mkuu wa serikali kutoa hati hiyo upande wa
utetezi ulipinga
hati hiyo kwa madai kuwa haikufuta taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kutoingizwa
katika file la mahakama sambamba na
kutoonyesha sahihi ya upande wa utetezi.
Wakili huyo upande wa utetezi alidai
kuwa kifungu cha 148 (4) cha mwenendo wa makosa ya jinai kilichotumika katika
fomu hiyo kupinga dhamana kinaanza kutumika pele tu hati hiyo inapowekwa katika
mafaili ya mahakama jambo ambalo alisema bado halijafanyika.
Awali mwanasheria mkuu wa serikali huyo
mbele ya hakimu mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro Kabate ,alidai mahakamani hapo kuwa mnamo Agosti 10 mwaka huu katika eneo la
Kiwanja cha Ndege manispaa ya Morogoro Ponda Issa Ponda aliwaambia “ndugu
waislamu msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za misikiti kwani
kamati hizo zimeundwa na Bwakwata ambao ni vibaraka wa CCM na serikali na
kama watajitokeza kwenu watu hao na watajitambulisha kwamba wao ni kamati
za ulinzi na usalama za misikiti,fungeni milango na madirisha ya msikiti
yenu na muwapige sana” na kwamba kauli ambayo ilikuwa ikiumiza imani za watu
wengine,na kwamba hatua hiyo ni kinyume cha agizo la mahakama ya hakimu
mkazi Kisutu Dar-es-salaam iliyotolewa na hakimu V. Nongwa tarehe
mei 9 mwaka huu ambayo ilimtaka ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani, ambayo ni
kinyume na kifungu cha sheria namba 124 cha mwaka 2002, shitaka ambalo alikana.
Katika shitaka la Pili lililosomwa
na mwanasheria mkuu wa serikali Bernard Kongola alisema Agosti 10 mwaka huu
katika eneo la Kiwanja cha Ndege manispaa ya Morogoro na mkoa wa Morogoro
waliwaambia waislam serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala vurugu
iliyotokana na gesi kwa kuwaua,kuwabaka, na kuwatesa wananchi kwa sababu
asilimia 90 ya wakazi wake ni waislamu lakini serikali haikufanya hivyo kwa
wananchi wa Loliondo walipokataa ,mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi ya
uwindaji baada ya kudai ni mali yao kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni
wakristu na kusema kuwa maneno ambayo yaliumiza imani za watu
wengine ambalo ni kinyume cha kifungu cha sheria 129 cha mwaka
2002shitaka ambalo pia mashtakiwa Ponda Isa Ponda alikana.
Aidha katika shitaka la tatu
ilidaiwa mahakamani hapo na mwanasheria mkuu wa serikali Bernard Kongola
kuwa mnamo Agosto 10 mwaka huu eneo la kiwanja cha ndege manispaa na mkoa wa
Morogoro mashitakiwa aliwashawishi waislamu kuwa serikali ilipeleka jeshi
Mtwara kushughulikia suala la vurugu uliyotokana na gesi kwa kuwaua,kuwabaka na
kuwatesa wananchi kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wake ni waislamu lakini
serikali haifanya hivyo kwa wananchi wa Liliondo walipotaka Mwarabu asipatiwe
kipande cha ardhi ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao kwa sababu
asilimia 90 ya wakazi wake ni wakristo” na mwanasheria kusema kuwa maneno
ambayo yalikuwa yakiumiza imani za watu wengine na kwamba kufanya hivyo
ni kinyume cha kifungu cha sheria namba 390 na kanuni ya adhabu
namba 35 cha mwaka 2002,
Hata hivyo Sheikh Ponda
alikana mashitaka hayo na kukiri kuwepo eneo la tukio tarehe ya tukio ambayo ni Agosti 10,
kukamatwa kwake pamoja na jina lake lililotumika mahakamani hapo.
Kesi hiyo imepangwa kutajwa tena
Septemba 11 mwaka huu, ambapo Septemba 17 ndipo yatatolewa maamuzi ya kupata
dhamana au laa huku wakili wa serikali adai kuwa upande wa mashitaka umeandaa
mashahidi 15 watakaotoa ushahidi dhidi
ya Ponda, DVD 2, kibali cha kongamano kilichotolewa na polisi pamoja na nakala
ya hukumu iliotolewa katika kesi ya jinai ya Sheikh Ponda iliotolewa
na hakimu mkazi wa mahakama ya
Kisutu Nongwa katika mahakama ya Kisutu.
Katika hali isiyo ya kawaida mshitakiwa huyo
alipofikishwa mahakamani alitumia njia ya usafiri wa basi la magereza tofauti
na watu walivyotarajia kwa helkopta kama ilivyokuwa awali.
Maelfu ya wafuasi wa Sheikh Ponda walifika katika
eneo la mahakama hiyo na kuanza kupiga kelele wakati mshitakiwa huyo akiingia
mahakamani na hata badae kuzingira
magari ya polisi na askari magereza
waliokuwa wakimsindikiza mshitakiwa huyo.
Pamoja na kuwepo kwa makundi makubwa ya watu
hao wakiwemo wanawake waliovalia ninja, polisi kwa kushitikiana na askari wa
magereza waliimarisha ulizni mahakamani hapo sambamba na kuweka uzio wa kamba kutpruhusu wafuasi hao kusogea eneo la
mahakama.
0 comments:
Post a Comment