Mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa wa Morogoro Harriet Sutta akiwa na katibu wake Nicodemas Tambo wakizungumiza juu matamko yanayotolewa na baadhi ya viongozi mkoani hapa kinyume na taratibu.
Mimi nazungumzia juu ya uchaguzi tulionao mbele yetu katika wilaya ya Gairo ludewa na Tungi Manispaa ya Morogoro, vijana washiriki kikamilifu kufanya kampeni za amani na utulivi na sio vurugu.
Kwa habari zaidi, soma hapa chini.
Kwa habari zaidi, soma hapa chini.
TAARIFA
YA UVCCM MKOA WA MOROGORO KWA WAANDISHI WA HABARI.
Ndugu zangu waandishi wa
habari Mliokusanyika Hapa ….
Kaka zangu na dada zangu
asalamu alekum….
Tumsifu yesu kristo……………
Awali ya yote, kwanza
nimshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema kwa kutukutanisha pamoja katika
siku hii ya leo ili tupate kuongea machache yanayoendelea katika Taifa letu na husani
katika chama chetu cha Mapinduzi CCM. Lakini Pia niwashukuru sana kwa kukubali
kuitikia wito wangu na kufika mahala hapa kwa wakati na kwa mda muafaka
Nawashukuruni sana, Na nawasahii muendelee na Moyo huo huo, mara zote
mkihitajika sehemu yoyote ile, Maana ninyi ni nguzo Muhimu saana katika kuupa
uma wa watanzania taarifa mbalimbali zinazoendelea katika Taifa lao.
Baada ya kusema hayo sina
Budi kuwaelezeni sasa kwa nini Nimekuiteni hapa, Siku chache zilizopita mnamo
Tarehe 2/02/2014 chama cha mapinduzi kiliazimisha Miaka 37 ya kuzaliwa kwake,
sherehe hizo zilifanyika katika Mkoa wa Mbeya
na kuongozwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Taifa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwa Naiba Ya jumuiya ya
Vijana wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro
(UVCCM ) ninachukua Nafasi hii Kumpokeza Mweshimiwa Dr. Jakaya Kikwete
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa kwa Hotuba yake nzuri alioitoa katika
kilele hicho cha maadhimisho ya sherehe hizo za kuzaliwa kwa CCM. Lakini pia
Kwa niaba ya UVCCM mkoa wa morogoro ninaomba yale yote alioyoyagiza Yatekelezwe
Haraka kwani ninaamini yatafufua uhai wa chama na Kukiimarisha zaidi lakini pia
kukiletea chama cha Mapinduzi Ushindi endapo yatatekelezwa kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa kabla ya
uchaguzi mkuu ujao.
Ndugu zangu waandishi wa
habari, Lakini pia nichukue nafasi hii kurekebisha baadhi ya mambo yaliojitokeza
katika Mkoa wetu wa Morogoro Hasa katika
Jumuiya yetu ya Vijana. Kumekumekuwepo
na Matamko mbalimbali yaliotolewa na baadhi ya viongozi wa jumuiya Yakihusishwa na Umoja wa Vijana Mkoa wa
Morogoro. Naomba ifahamike kua uvccm ni taasisi ambayo ina miongozo na mfumo
rasmi wa utekelezaji wa shughuli zake za kila siku. Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni za umoja wa
vijana Msemaji wa Jumiya ya Vijana mkoa wa Morogoro Ni mwenyekiti wa UVCCM MKOA
au Katibu Wa UVCCM Mkoa kama italazimika Mtu mwingine kusema basi ni kwa idhini
maalumu ya Mwenyekiti
Wahenga walisema “kila
panapotokea kosa lolote lile kuna jambo
la kujifunza” hivyo hakuna kosa lisilo na faida Kupitia haya yaliotokea katika Mkoa wetu
naomba pia iwe Fundisho kwenu waandishi
habari kila mkiitwa na Mtu yoyote anaetaka kuongea nanyi kama anaongea
nanyi kwa niaba ya Tasisi ni vema mkafwatalia na mkajiridhisha kama ni Msemaji
sahihi wa Tasisi Hiyo ili Kuepuka malumbano yasio na Tija
Kabla sijamaliza ningeomba
pia kuchukua Fursa hii kuwapatia pole wakazi wa wilaya ya Kilosa kwa mafuriko
yaliowapata ninaamini wapo katika wakati Mgumu hasa baada ya kuharibiwa makazi
yao, na kuharibiwa mali zao. Nichukue nafasi hii kuwatia Moyo na kuwahakikishia
serikali ya Chama cha Mapinduzi itahakikisha wanapatiwa stahiki zote anazotakiwa
mtu kupewa na serikali yake yanapotokea majanga kama hayo.
Lakini pia niyaombe
mashirika yasio ya kiserikali mashirika ya kimataifa na wadau mbalimbali wenye
uwezo kuendelea kujitokeza kwa wingi kwenda kuwafariji wana kilosa waliopatwa
na mafuriko hayo na kuwaapa misaada ya kila namna inayostahili.
Mwisho ninaomba Kampeni
zinazoendelea katika Mkoa wetu kata ya Tungi na Rudewa zifanyike kwa amani na
ninawaomba vijana wa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo mdogo kua
wastaarabu na waadilifu wajivunie kulinda misingi ya Taifa hili amani upendo na
mshikamano uchaguzi usiwagawe na kueneza chuki baina yao hivyo ninawasihi
washiriki kampeni hizo kwa amani na utulivu “wakubali kutofautiana kisera na
kwa hoja ” ila “wasikubali kufarakana” Vijana tunahitaji Uvumilivu wa kisiasa
ili tukomae katika siasa na Demokrasia ya kweli
Niwashukuru saana kwa
Kunisikiliza…..
Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Africa
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na Harriet Sutta
MWENYEKITI WA UVCCM MKOA
MOROGORO
04/01/2014
0 comments:
Post a Comment