Pages

Subscribe:

Thursday 6 February 2014

NI DHANA POTOFU KUWA SHULE ZA KATA HAZINA UBORA

 Cheti cha mwanafunzi Petter aliyeshinda mashindao ya Nsha Afrika Mashariki kilichotolewa na manispaa ya Morogoro kama motisha kwa lengo la kuwatia moyo wanafunzi wanaofanya jitihada katika masomo yao.
 Meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo akikabidhi cheti kwa mwanafunzi Ali naye ni mshindi wa shindano hilo kwa SADEC ambaye amekuwa mshindi wa pili na kupewa 50,000 na cheti.
 Huyo ndiye Petter mwenyewe kutoka shule ya sekondari ya kata ya Tushikamane ambaye ni mshindi wa shindano hilo kwa Afrika Mashariki ambaye amepatiwa cheti na shilingi 200,000

Watendaji katika Manispaa ya Morogoro wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani.


Baada ya kupokea zawadi hiyo Petter aliomba serikali kuziangalia shule za kata kwa kuzipatia walimu wa masomo ya sayansi wa kutosha  pamoja na maabara.
Alisema kuwa shule nyingi za kata zinakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na walimu wa masomo ya sayansi pamoja na walimu wa masomo hayo.
Hata hivyo aliitaka jamii kuacha dhana potofu kuwa shule za kata hazina ubora na badala yake watambue ukuwa ubora wa elimu unatokana na juhudi binafsi za wanafunzi wenyewe.
Alisema kuwa siri ya kushinda kwake kumetokana na juhudi binafsi alizofanya kutafuta material kutoka sehemu mbalimbali pamoja na kushirikiana na walimu.
Alisema kuwa imefika wakati kwa wanafunzi kutobweteka na kuanza kuelekeza juhudi binafsi katika masomo kwa kutafuta material mbalimbali hata nkatika mitandao

0 comments:

Post a Comment